20 Feb 2020 in National Assembly:
Pia, tunataka wavuvi wapewe vifaa mwafaka, sio kutumia tanga tu mtindo wa kizamani. Tunataka wapatiwe mashini ili wapate kwenda mbali zaidi kutafuta samaki wengi zaidi. Na zile sehemu zingine ambazo ziko Lamu, kama sehemu za Wito na Mpeketoni, wao pia wanaweza kufanya ukulima wa samaki. Wajengewe mabirika ya samaki. Na katika sehemu fulani za Bahari The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
20 Feb 2020 in National Assembly:
Hindi kunaweza kukatengezwa birika za kisasa zinazofanywa ndani ya bahari ili watu wavue pweza, kaa, majongoo, na kadhalika. Hivi vyote ni vitu ambavyo vinaweza kuusaidia uchumi wa Kenya. Nitakomea hapo kwa sasa bali tu naomba wakiangalia huku kwingine waangalie Lamu pia. Asante.
view
18 Feb 2020 in National Assembly:
Thank you, Hon. Speaker for giving me this opportunity to ask Question No. 002/2020…
view
18 Feb 2020 in National Assembly:
The Question is directed to the Cabinet Secretary for Lands. Following a land survey carried out by the Ministry in January 2019 and later reviewed on 20th August 2019 in Vumbe area of Lamu East Constituency, Lamu County, could the Cabinet Secretary provide the Report of the sub-division exercise and the number of plots arrived at? Thank you, Hon. Speaker.
view
10 Feb 2020 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Spika. Kwa niaba yangu, familia yangu na Kaunti ya Lamu kwa jumla, natoa rambirambi zetu kwa familia ya Rais wa Pili nakwa mwenzetu Gideon. Tutamkumbuka baba yetu kwa mambo mengi. Moja ni kuleta Wakenya pamoja na yale maziwa ya Nyayo tuliyokunywa. Pia, alianzishia watu wa Lamu
view
10 Feb 2020 in National Assembly:
ya Ksh.10 milioni na watoto wengi wakafaidika kwa masomo. Pia, alitupatia Naibu Wa Waziri ndugu yetu Mohamed Hashim na nyumba kuu hapa ikakuwa rahisi kufikia. Kulikuwa na wazee walioheshimika sana na wakipiga simu inashikwa. Pia tunakumbuka wazee wetu kama marehemu Maharus. Tutamkumbuka baba kwa mambo mengi. La, muhimu ni sisi viongozi…
view
5 Dec 2019 in National Assembly:
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Hoja hii.Ninatoa kongole kwa Mhe. K’oyoo kwa kuleta Hoja hii.
view
5 Dec 2019 in National Assembly:
Mafuriko yanaathiri sehemu nyingi za Kenya, Lamu ikiwa mojawapo. Kabla ya kutoa lawama, ningependa kushuru Serikali kwa jitihada zake lakini ukweli ni kwamba kazi ya ziada inafaa kufanyika. Maeneo ya Moa na Chalaluma huko Lamu yameathirika pakubwa na mafuriko.
view
5 Dec 2019 in National Assembly:
Mwaka jana, mafuriko yalitokea nakulikuwa na mipango ya waathirika kulipwa. Kamati ilipendekeza lakini mpaka leo, hawajalipwa. Yale yaliyotokea sasa yametokea zaidi mengine. Kila mwaka sasa yamekuwa yakitokea. Hawa wafugaji wanapata matatizo sana kwa sababu hali ya hewa imebadilika. Ikiwa si mafuriko ni ukame. Ukame unatokea na ninashukuru Serikali. Ilikuwa na jitihada kutumia shirika la Kenya Meat Commission (KMC). Ninashangaa kama hili Shirika linajua ramani ya Kenya kwa sababu walienda kaunti zingine zote wakaokoa wafugaji, wakachukua ile mifugo, wakachinja wakasaidia wale ambao hawana chakula, lakini Lamu hawakufika. Sijui ramani ya Lamu inakaa vipi, ni watu hawaielewi ama wanaona hawa ni wanyonge ...
view
5 Dec 2019 in National Assembly:
Ukienda Hindi, majirani zetu nasisi wenyewe, kuna jamii ya Somali na ni wengi. Na hata wa Ijara wanatoka kule wakija kwetu kutafuta malisho. Lakini wakati wa mavuno wanasahau sisi watu wa Lamu. Nataka hili Shirika lijue Lamu ni Kenya na inahitaji huduma zote zile zinapeanwa kwa Wakenya wengine. Hata kama namba za kura ni kidogo na hizi hesabu zimezidi kutuumiza, sisi ni Wakenya na kama vile inavyosemekana kila kura inahesabiwa, haiwezi kwenda mbili kama haijaanza na moja. Sisi ni Wakenya kule na matatizo yako. Naomba Serikali itutambue ili tusiseme tu watu waliotengwa siku zote.
view