Ruweida Mohamed Obo

Parties & Coalitions

Born

1978

Telephone

0722222784

All parliamentary appearances

Entries 201 to 210 of 439.

  • 13 Nov 2019 in National Assembly: zote. Kwa mfano, kuna watu wanaofanya kazi kwa Jeshi. Kwa hivyo, wanaofanya kazi kule wana matatizo mengi kwa sababu ya ukosefu wa vitu kama barabara, maji na hospitali. Wanaofanya kazi kule ni wenu pia; wateteeni maana wanapoenda kule, pia wao wanapata shida hizo. Nilienda kuona Jeshi kule. Wana shida. Zile sehemu ni ngumu. Ukienda kuwaona askari wanaokaa kule na kulipwa sawa na walio kwingineko, pia nao wanapata shida. Kuna sheria zimewekwa kwamba, walimu wapelekwe kokote kwa sababu Serikali inataka tujumuike pamoja kama Wakenya. Walimu wakitolewa Lamu kupelekwa sehemu zingine, imekuwa sawa. Lakini wa sehemu zingine wakipelekwa Lamu, wanakimbia. Hawawezi kuishi ... view
  • 13 Nov 2019 in National Assembly: Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nimeamka kuunga mkono Mswada huu. Kama unavyojua, uongozi huja na kwenda. Leo tuko hapa na siku nyingine tutakuwa kwingine. Lakini maisha huwa magumu kule nje baada ya kuja hapa. Hii ni kwa sababu ukishakuwa kiongozi na kuja hapa Bungeni, hata wakati uko nyumbani, wananchi wanakufuata hata kama hawakukuunga mkono. Lakini wao huja kukwambia shida zao na kusema wamejuta. Lakini kama wewe ni kiongozi, lazima uwe pale kuwasaidia kwa matatizo yao. view
  • 13 Nov 2019 in National Assembly: Kwa hivyo, yale matatizo yote tunapata saa hii na wale ambao walitutangulia bado wanafuatwa, hata kama pengine ni kwa kiwango kidogo. Sasa kama walitoka hapa na hawakuangaliwa vizuri, hii inaleta matatizo zaidi. Wengine mpaka hukimbia, kuhama miji na kukaa sehemu zingine. Wanakaa mafichoni na kujificha. Kwa hivyo, Mbunge akiwa hayuko mamlakani angalao ile hadhi yake iwe inapendeza. Haipendezi na kukufurahisha kumwona Mbunge pengine amefunga kioo cha nyuma cha gari na mfuko wa nailoni. Huwa inaogopesha sana ukiona mambo kama hayo. view
  • 13 Nov 2019 in National Assembly: Kwa hivyo, ni vizuri waangaliwe ndiyo wasiaibishe Bunge. Yule Mbunge anapaswa kuwa na pesa kidogo ya kumshikilia yeye na familia yake ili kutimiza matatizo madogo madogo. Pia, pengine mawazo mengi huleta magonjwa. Kwa hivyo, hii pesa inaweza kumsaidia ndiyo ajisukume. Naunga mkono waangaliwe vizuri na kuwe na mipango mizuri. Ahsante kwa aliyeleta Mswada huu. view
  • 13 Nov 2019 in National Assembly: Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. view
  • 7 Nov 2019 in National Assembly: Asante Mhe. Spika. Naunga mkono. Usalama ni muhimu. Tushirikiane tusonge mbele. Mbali na kule South Africa, hapa Kenya ukosefu wa usalama unachangia mambo mengine ambayo hayatusaidii. Kwa mfano, kwenye shughuli ya kuhesabu watu, wakazi wa Lamu tumeathirika sana kwa sababu ya hali mbaya ya usalama. Maafisa wahusika hawakuenda kuhesabu watu katika sehemu nyingine wakihofia usalama wao. Hivyo basi, watu wa Lamu County tunaonekana kuwa wachache. Tuko wengi lakini kwa sababu ya ukosefu wa usalama maafisa wahusika hawakuenda katika sehemu za Msitu wa Boni kama vile Sadan na Vumbe kuhesabu watu. Kuna sehemu nyingi ambazo watu huenda mashambani kulima. Maafisa wa view
  • 7 Nov 2019 in National Assembly: hawakufika huko kuwahesabu watu. Kisha wakasema watu wa Lamu ni wachache zaidi Kenya. Hiyo inaenda kutuathiri sana. Kihistoria, Lamu tumekuwa na maeneo Bunge mawili. Tunatishiwa na hiki kiwango cha watu. Tuko taabani na matatizo mengi. Hayo maeneo Bunge mawili yakiondolewa, itatuathiri zaidi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 7 Nov 2019 in National Assembly: Ni muhimu kuunga usalama mkono. Asante. view
  • 30 Oct 2019 in National Assembly: Asante, Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia nafasi hii nami nichangie Hoja hii. Mwanzo, ningependa kumshukuru Mhe. John Wambugu kwa kuleta Hoja hii muhimu nasi tuichangie. Tukitunga sheria ya kuwafanya asilimia 100 ya wanafunzi wanaotoka shule za upili kwenda vyuo, itakuwa jambo la muhimu sana na itakuwa msaada kwa Wakenya wote. Tunajua changamoto nyingi tunazozipata na vijana wanaharibikia hapo katikati. Kenya kuna nafasi nyingi za kazi ambazo vijana wanaweza kujishughulisha nazo. Nafasi na kazi ziko nyingi na husababisha Serikali kuchukua watu kutoka nchi zingine. Vijana wetu wakipelekwa katika vyuo hivyo kujifunza taaluma mbali mbali, ili wapate ajira na kuzongesha Kenya mbele. ... view
  • 30 Oct 2019 in National Assembly: wanajaribu kupeleka watoto katika National Industrial Training Authority (NITA) lakini kuna wengi wa kupelekwa ambao wako kule mashinani. Twajua hatari iliyoko kule Lamu. Vijana wengi wakimaliza shule za upili na wakose ile hamu au wavunjike moyo, wanaingilia matatizo mbali mbali ambayo yanajulikana. Inaleta utovu wa usalama katika nchi yetu ya Kenya tunayoipenda. Kwa mfano, inajulikana kwamba kule Lamu, vijana wengi wameingia katika mihadarati. Hatua hii ikichukuliwa, itapunguza pakubwa vijana kushiriki mihadarati kwa sababu hawana kazi ya kufanya. Tunapenda mambo kama haya lakini inakuwa ngumu kuyatekeleza kule Lamu. Wanafunzi walio katika shule za upili wanavuka kuenda kwenye vyuo vikuu. Lakini hata ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus