Ruweida Mohamed Obo

Parties & Coalitions

Born

1978

Telephone

0722222784

All parliamentary appearances

Entries 211 to 220 of 439.

  • 30 Oct 2019 in National Assembly: Bwana Naibu wa Spika, nimetafuta Katiba ya Kiswahili lakini nimekosa. Katiba ambayo nimepata ni ya Kiingereza. view
  • 30 Oct 2019 in National Assembly: Nimegoogle nikashindwa. Haikuja. view
  • 30 Oct 2019 in National Assembly: Ni kweli, Bwana Naibu wa Spika. Hata baba alisema Kiswahili kilianza Pate. Akatoa historia yote mpaka kikakufa huko Congo. Lakini kilipata ugonjwa hapa Nairobi. Makala ya 53 (b) ya Katiba inasema ni haki ya kila mtoto kupata elimu ya bure. Makala ya 55 (a) inasema kuwa Serikali ina jukumu la kuhakikisha vijana wapate elimu na ujuzi. Basuba The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 30 Oct 2019 in National Assembly: Ward haijakuwa na shule ya chekechea, ya msingi au ya sekondari kwa miaka mitano. Huu ni ukweli. view
  • 30 Oct 2019 in National Assembly: Asante, Bwana Naibu wa Spika. Mheshimiwa Sankok, hivi karibuni utapata Standing Orders za Kiswahili ambazo zitakusaidia. Tulikuwa pamoja katika Kamati kwa hivyo utasaidika hivi karibuni. Itabidi usome Kiswahili zaidi na Kiswahili kitukuzwe. Nimeng’ang’ana na kuuliza maswali lakini hatujapata majibu mpaka leo. Hii itatusaidia sana. Hiyo asilimia ya wanafunzi wanaotoka shule za msingi na kujiunga na shule za upili bado haijatimia. Bado sisi kule Lamu tunavutwa nyuma. Naomba Serikali na wahusika waangalie Lamu kwa sababu sisi pia ni Wakenya. Sera nzuri zinawekwa lakini tutakuwa watu wa mwisho kufikiwa nazo. Kama vile Serikali inajitolea pakitokea shida katika shule hapa Nairobi, nao waje ... view
  • 30 Oct 2019 in National Assembly: Asante Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii ili niunge Hoja ya kuidhinisha Toleo la Kiswahili la Kanuni za Kudumu za Bunge la Taifa. Mwanzo, ninachukua nafasi hii nimwombee Mungu na nimpongeze Hayati Rais wa Kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta. Yeye ndiye aliyetoa amri Bunge la Kitaifa litumie Kiswahili. Kwa sababu hiyo, kama hangetoa amri, saa hii hatungekuwa tukiunda hizi Kanuni. Ni vyema tumtambue na tumwombee Mungu amweke pahali pema. Pili, ningependa kuzungumzia kidogo kwamba hili Bunge limekuwa likitumia Kiswahili kwa zaidi ya miaka 60. Ni kushukuru wewe kwa sababu baada ya hii miaka, sasa tuna hizi Kanuni za Kudumu. ... view
  • 8 Oct 2019 in National Assembly: Ahsante, Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi ya kuchangia. Suala la ardhi ni suala tata sana, na ni donda sugu. Limetatiza kaunti nyingi. Inatatiza sana kuona watu ambao wameishi katika ardhi kwa muda wa zaidi ya miaka 200 wakifurushwa. Kwenye ardhi hiyo, kuna nyumba na visima. Serikali inakuja na kufanya view
  • 8 Oct 2019 in National Assembly: bila ya wakazi kujua. Barabara inapitishwa hapo. Kule Lamu watu wamekatiwa mnazi na kufidiwa Kshs3,000, ilhali mnazi huo kwa mwaka mmoja unakupatia zaidi ya hizo Kshs3,000. Kwingineko kwenye kaunti hiyo hiyo, gogo la stima kupitia shambani mwake amelipwa Kshs500,000. Kwa hivyo, unashangaa ni njia gani zinatumika ndiyo watu wengine walipwe zaidi na watu wengine wanyanyaswe. Ahsante Mhe. Spika. view
  • 8 Oct 2019 in National Assembly: Asante, Bi Naibu Spika wa Muda. Nimepitia pendekezo la Ripoti ya Kamati. Mwanzo ningependa kuipongeza Kamati kwa kazi yao nzuri. Ripoti inasema kuna shida na mojawapo ni kwamba wale wanaoenda kufanya kazi nje ya nchi au Arabuni wanapitia njia za mkato. Ninajua sababu hiyo ni kutokana na njaa. Kama hawapati kazi hapa, inabidi waache makwao waende wafanye kazi sehemu zingine. Jambo hilo The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 8 Oct 2019 in National Assembly: liko. Kuna mwimbaji aliyesema kuwa watu waacha kwao kwa shida za kilimwengu. Kama kungekuwa na kazi kwetu, watu hawangewacha makwao, wangefanya kazi hapa. Kuna sababu ya wao kuenda kule. Nafasi ziko kule na nafasi hizo tunafaa tutilie mkazo tuzipate. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus