Ruweida Mohamed Obo

Parties & Coalitions

Born

1978

Telephone

0722222784

All parliamentary appearances

Entries 221 to 230 of 439.

  • 8 Oct 2019 in National Assembly: Wale wanaoenda kufanya kazi kule wanafaa watengeneze jina la Kenya. Kuna wengi wanaotaka hizo nafasi, wamekaa mitaani na hawajazipata. Wakitengeneza jina la Kenya, wataiuza Kenya na wengine watapata nafasi ya kuenda kule. Kuna matatizo lakini pia kuna watu walio na matatizo. Kwa mfano, kama umeenda kufanya kazi, nenda na ile kazi yako ilivyoandikwa kwenye mkataba lakini ukienda kule na kufanya kazi tofauti, wewe umetumia tu njia ya kufika kule kisha ufanye kazi zako. Kwa mfano, kuna wengine wameenda nchi za Arabuni kisha unasikia wanauza pombe na serikali ya kule hairuhusu. Hata kama hairuhusiwi, itakuwa hatia. Utajitafutia shida mwenyewe kisha uanze ... view
  • 8 Oct 2019 in National Assembly: Pia nimeona Kamati ikisema kwamba inataka sasa kazi zipitie kwa Wizara ya Leba ili isije ikaleta shida ikawa kaunti zingine hazipati nafasi. Saa hii kama sisi watu wa Lamu, mila za kule wengine zawashinda lakini sisi hazitushindi. Saa hii tunapata hizo nafasi za kuenda kule. Zikija kwa Wizara, isije wakapea wengine na sisi tukazikosa. Wale ambao hawawezi mila za kule wasiende. Wale wanaoweza waende. Kwa sababu ni mila za Kiislamu, wengine zinawashinda. Kwa mfano, wanataka wavae hijab ama mtandio, wakifika kule lakini wengine wanataka kuvaa nguo zao. Kama zile ndizo zinaleta shida, afadhali wasiende na watafute nchi zingine ambazo mila ... view
  • 2 Oct 2019 in National Assembly: Asante, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii. Naunga mkono Mheshimiwa Nyoro kwa Mswada huu. Ni kweli kwamba ufisadi unamaliza nchi yetu. Unasababisha maendeleo mengi yasifanyike katika nchi yetu ya Kenya. Maendeleo mengi ambayo yaweza kufanyika na ikasaidia walalahoi hayafanyiki kwa sababu ya ufisadi. view
  • 2 Oct 2019 in National Assembly: Nchi yetu ya Kenya inaonyesha ina nguvu maana waporaji wanapora kwelikweli na nchi bado imesimama. Lakini njia hii tunayoenda kama hatutachukua mikakati mizuri ya kuondoa ufisadi, basi nchi itasambaratika. view
  • 2 Oct 2019 in National Assembly: Ninataka niongee kidogo kuhusu ufisadi Lamu. Ni muhimu Serikali au vitengo vinavyoangalia ufisadi viangalie Kaunti ya Lamu vizuri. Hii ni kwa sababu kaunti yetu imetengwa na hatutaki iwe imetengwa siku zote au tujiite kaunti iliyotengwa siku zote. Tunataka ifike wakati tuseme na sisi kaunti zingine zije ziangalia Lamu kimaendeleo. view
  • 2 Oct 2019 in National Assembly: Nawaomba wanaohusika waimulike Lamu vizuri maanake pesa zinangia kama vile za view
  • 2 Oct 2019 in National Assembly: na Equalisation Fund. Pesa hizo kama hazitachungwa vizuri, basi hizi kaunti ambazo tunahesabu kwamba zimetengwa zitakuwa tena hakuna hilo jina la kusema tumetengwa. view
  • 2 Oct 2019 in National Assembly: Matatizo mengi tunayopata Lamu ni kwa sababu ya ufisadi. Kila tatizo unalolitaja Kenya, halikosekani Lamu. Kama shirika linalohusika au wale wanaohusika wataangalia ufisadi, tutasonga mbele sana. Utashangaa na inashangaza, sisi tuna pesa ya bursaries ambayo inapitia The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 2 Oct 2019 in National Assembly: mikononi mwa Wabunge lakini pesa hizi wale wanyonge hawapati. Mtoto akimaliza shule ya msingi na awe anaenda shule ya upili inafaa apata pesa za kumwezesha kuendelea na elimu yake. Akipata alama ya C+, anapata nafasi ya kuingia chuo kikuu na hapo tunafanya michango ilhali pesa zipo, kisha tunakaa hapa tukizungumzia ufisadi. Najua hapa tukisema itauma lakini ukweli ni mchungu. Sisi pia hapa lazima tuwaangalie wale wanyonge maanake saa nyingine mtindo huu wa Kenya unafanya sisi Wabunge tuangalie mahali kuna kura nyingi. Pengine huyu mnyonge hana kura nyingi kwao na hapo anakosa ile nafasi ya kupata bursary . view
  • 2 Oct 2019 in National Assembly: Tumefanya michango mingi na hadi sasa tunaendelea kuchanga pesa. Michango hii inasababisha hata wengine wetu kutafuta njia ambazo sio za kawaida kutafuta pesa. Michango hufanyika kwa sababu ya ugonjwa, elimu na kadhalika. Ingekuwa vizuri kama pesa za bursaries zingetumwa kwa shule za upili ili wanafunzi wote wanasome bure. Lakini wengi wetu tukiambiwa jambo kama hilo tutakataa. Shida ziko na zinasababishwa na mienendo hii. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus