2 Oct 2019 in National Assembly:
Utashangaa katika Bunge hili, kuna Wabunge wa sehemu zingine ambapo mambo yanafanyika. Unashangaa kwa mwaka mmoja mtu amejenga madarasa arobaini na sehemu zingine madarasa yakizidi ni manne. Wengine bado wanasoma chini ya miti au wanakalia mawe.
view
2 Oct 2019 in National Assembly:
Tunawaomba Mkaguzi wa Vitabu vya Serikali na EACC wapitie kila sehemu na wawe na bidii zaidi ndio waokoe Kenya kwa maana pesa zinafika na zipo lakini shida ziko pale pale miaka nenda miaka rudi. Kwa mfano, tutasikia pesa za barabara zimetoka. Pengine kama kwetu Lamu East, Ksh98 milioni zitatolewa kujenga barabara. Hiyo barabara baada ya mvua kidogo itaharibika. Sasa tutamlaumu Rais Uhuru? Maanake hapa nchini Kenya kila pahali tunaenda wanamlaumu Rais Uhuru. Kwa nini viongozi wengine wasichukue hayo majukumu ama wahusika wa EACC? Hao ndio wanasababisha Rais kulaumiwa. Wakifanya kazi nzuri na kila mahali kunga’re, Rais hatalaumiwa.
view
2 Oct 2019 in National Assembly:
Huko Lamu tatizo kubwa ni mihadarati kwa sababu ufisadi ndio unachangia pakubwa. Ukiangalia roadblocks kutoka Malindi mpaka Lamu ni zaidi ya kumi. Pia kuna zingine nyingi lakini mihadarati hupita na watoto wanatumia. Hii yote imesababishwa na ufisadi. Ardhi pia iko na changamoto sana lakini ni matumaini yetu kwamba, tume tuliyochagua itafanya kazi nzuri. Tamaa ikizidi ndiyo inaleta haya matatizo. Hivi sasa, huko Lamu kunapimwa na utasikia watu wametoka kaunti zingine ili wapatiwe ardhi. Ile ardhi ya Lamu iko na wenyewe. Kabila zote zilizoko Lamu zina haki kwa sababu ni ardhi yao. Lakini wanaotiririka kutoka kaunti zote hadi Lamu wajue Kaunti ...
view
2 Oct 2019 in National Assembly:
Serikali inahitaji stakabathi na hawana. Napongeza Wizara ya Elimu kwa jambo moja ambalo ni kuwa wanataka kutumia skills ambazo zitasaidia watu.
view
2 Oct 2019 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda.Tuna masikitiko makubwa. Kile KFS imetufanyia ni ya aibu. Ukiangalia ile picha au video ambayo ilionyeshwa, lile gari lilikaa karibu dakika kumi na tano ilhali hakuna hatua za haraka zilichukuliwa. Hilo linadhihirisha udhaifu mkuu. Kampuni ya feri ingelikuwa na wapiga mbizi. Inadhihirisha wazi kuwa walioko hawana moyo
view
26 Sep 2019 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii nami niuchangie Mswada huu. Elimu ni sekta muhimu sana. Nimekuwa hapa tangu saa nane na nusu nikingoja nami nipate nafasi nichangie. Nimekuwa na dharura muhimu; dadangu yuko hospitali katika chumba cha upasuaji lakini nimesema acha nikae hapa nami nipate hii nafasi. Hii ni kuonyesha umuhimu niliokuwa nao wa kuchangia Mswada huu. Ripoti nyingi za Kamati ya Elimu zikiletwa huzungumzia mambo mazuri sana. Kamati ya Elimu na Utafiti huleta ripoti nyingi ambazo zinazungumzia mambo mazuri sana na mikakati mingi ya kuboresha elimu. Nimeipitia Ripoti hii na ina mambo mengi muhimu ...
view
26 Sep 2019 in National Assembly:
Ukiniruhusu kunukuu, wanasema kwa lugha ya kimombo every child has a right to
view
26 Sep 2019 in National Assembly:
. Lakini ni masitikiko kwamba Kaunti ya Lamu kwa muda wa miaka mitano, shule nyingi zimefungwa. Hakuna shule za chekechea, msingi na upili. Huu Mswada ni mzuri lakini tunapitishia Wakenya wengine ambao ni bora. Masikitiko sio kwamba sijafanya kazi yangu kama Mbunge. Nimejaribu. Nimeuliza Maswali na nikajibiwa na niakambiwa nipitie kwa wizara na nimepitia huko mara nyingi. Nikienda, ninaambiwa suluhisho itatolewa Jumatatu. Siku hiyo nafika na kuambiwa suluhisho itatolewa jumafulani. Nimeenda mara nyingi lakini ni kama hawataki kutoa suluhisho. Nimeambiwa niandike maombi na nimeandika. Ni kama kuna sehemu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes ...
view
26 Sep 2019 in National Assembly:
zingine ambazo zina Wakenya bora. Ingekuwa bora kama kungekuwa na mobile school ndio watoto wasome.
view
26 Sep 2019 in National Assembly:
Hata mbinu za kisasa kama televisheni ama tarakilishi zingetumiwa ndio mtu akiwa Nairobi asomesha wale watoto. Jamii ndogo ya marginalised community iliyotengwa ya Basuba, Boni ana Aweer mpaka sasa hawana shule ya chekechea. Kila wakati nikienda kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknologia, nasukumwa kwa Wizara ya Usalama. Nimetafuta suluhisho na sipati. Simwoni mwenyeketi wa kamati lakini anajua shida zangu. Nimeng’ang’ana lakini sipati suluhisho. Sijui wamelengea nini hawa watoto maanake Katiba inasema lazima wapatiwe haki zao. Mimi nasikia uchungu nikiketi hapa kupitisha Mswada mzuri uende kwingine lakini kwetu haufiki.
view