26 Sep 2019 in National Assembly:
Tunajua Lamu iko Kenya. Sijui kwa nini sheria hizi zipangiwe wengine lakini si sisi. Kuna mipango mizuri ambayo Serikali inafanya, kwa mfano watoto wa msingi wote waende sekondari, lakini hii haiwezi kufanyika Lamu. Inanipatia uchungu sana. Ninaomba Kamati ijue jambo hili na kutafuta suluhisho. Saa hii najipanga kuleta petition .
view
26 Sep 2019 in National Assembly:
Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda.
view
25 Sep 2019 in National Assembly:
Asante, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii niweze kuchangia na kumuunga mkono Mheshimiwa Martha.
view
25 Sep 2019 in National Assembly:
Hili ni jambo la maana sana. Kama alivyosema Mheshimiwa Jaldesa, ni mama pekee anayeweza kufikiria jambo kama hili. Lakini pia ninawashukuru wale Waheshimiwa wanaume ambao wameunga mkono kwa sababu wameusikia ule uchungu wa mama. Kunahitajika muda wa kukaa na mtoto anapojikuta kwenye mazingira mapya. Kuna mambo mengi ambayo yule mama anahitaji kumuhudumia yule mtoto vizuri. Anastahili atafute shule nzuri na amkaribishe nyumbani. Kuna mambo chungu nzima yanayohitaji muda. Akipewa nafasi hiyo ataweza kuungana na yule mtoto vizuri. Kwa hiyo, ninaunga mkono hapo.
view
25 Sep 2019 in National Assembly:
Pili, ninaomba mashirika yanayohusika na jambo hili yawe yanafuatilizia kwa makini wahakikishe kwamba Watoto hao wameingia kwenye mikono mizuri yenye usalama. Nchi nyingine huchukulia masuala ya watoto kwa uzito mkubwa. Kwa mfano, kuna mtoto ambaye alizaliwa nje ya nchi, na amekuja Kenya. Tulishangaa kuona serikali ya kigeni ilimtuma afisa wa watoto kusafiri mpaka Chundwa, ambayo iko Lamu Kusini, kuja kuangalia kama yule mtoto yuko kwenye mazingira mazuri. Lakini, sisi Kenya hatufanyi jitihada zozote za kufuatiliza na kujua iwapo mtoto kama huyo yuko salama. Yule mtoto alikuwa ni wa Uingereza. Afisa wa watoto alitumwa kuja kuhakikisha kama mtoto yule anakaa vizuri ...
view
25 Sep 2019 in National Assembly:
Watoto wa Kenya tunawapenda lakini kuna wengi ambao wana matatizo mbalimbali. Mimi nimesomea Lamu Kusini. Serikali imesema watoto wakitoka shule ya msingi waende wote kwenye shule za sekondari lakini kuna sehemu nyingine kule Lamu Kusini, kama wadi ya Basuba, ambako hakuna shule.
view
25 Sep 2019 in National Assembly:
Tulipopiga kelele, shule moja ndiyo imefunguliwa. Shule nne mpaka sasa hazijafunguliwa kwa miaka minne sasa, ilhali watoto wa Kenya wanalindwa na Katiba lakini bado wana matatizo mengi.
view
25 Sep 2019 in National Assembly:
Dadangu Mheshimiwa Jaldesa pia amegusia suala la madawa ya kulevya. Inafaa atoe mfano wa Lamu. Katika nchi hii, Lamu ndiyo imeathirika zaidi kutokana na utumizi wa madawa ya kulevya. Watoto wenye umri wa miaka 11 wanatumia madawa ya kulevya. Wanadanganywa. Mara nyingi hawajiingizi kwenye matumizi ya dawa za kulevya kwa hiari yao. Kuna maneno ambayo nikiyasema watu hapa wataniangalia mara mbilimbili. Hata hivyo, watu wengine huwadanganya watoto wanaojulikana kama lover boys; kwamba madawa hayo yatawasaidia kuongeza nguvu za kiumu ilhali ni uongo. Kwa hivyo, wanazitumia mwishowe wanajipata wako hapo bila kusaidika. Ni muhimu kuwachunga watoto wetu wote. Kuna changamoto nyingi ...
view
25 Sep 2019 in National Assembly:
Serikali ilisema watu waache kutumia mifuko ya plastiki na hivi sasa hatutumii mifuko hiyo. Mtu akifanya hivyo anafanya kwa siri sana. Inafaa tukijitolea tufanye hivyo pia kuhusu ulanguzi na matumizi ya madawa ya kulevya. Tujisukume zaidi ili tuwachunge watoto wetu. Ahsante.
view
10 Sep 2019 in National Assembly:
Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Naunga mkono moja kwa moja maana usalama wetu ndani ya ndege ni muhimu sana. Sheria ziko nyingi. Hii leo kampuni nyingi zinazingatia zaidi mambo ya usalama. Kuna laini ndefu. Usalama huanza pale wageni wakiingia ndani ya ndege, mizigo ikichukuliwa na hata tukiwa ndani ya ndege. Usalama unatakikana katika nyanja zote hata ndege inapopaa. Kutoka ndege ikipaa angani mpaka inaposhuka usalama unahitajika wakati wote. Mtu akianza kuleta shida ya usalama, captain au rubani wa ndege ana haki… Amepewa jukumu na sheria. Hata kama ni nani amebebwa humo ndani, yeye ndiye captain, yaani rubani. Anayo haki ...
view