28 Feb 2024 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Naibu Spika.
view
14 Feb 2024 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie. Kwanza, ningependa kumpongeza Mbunge Mwakilishi wa Wanawake wa Kaunti ya Nairobi, Mhe. Esther Passaris, kwa kuleta Hoja hii. Pia, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwa katika Eneo Bunge langu la Lamu Mashariki, hakujawahi kutokea mauaji kama haya ya kinyama. Wanaume wetu ni wastaarabu; hawaui wanawake. Nachukua nafasi hii kuwapongeza wanaume wote wa Lamu Mashariki. Ni kweli Lamu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor
view
14 Feb 2024 in National Assembly:
Mashariki inakumbwa na shida nyingi sana, lakini, alhamdulilahi, tunashukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwa kwetu hatujashuhudia mauaji ya wanawake. Hivi leo tunalia na Wakenya wengine. Si sawa wanawake kuuawa. Pia si sawa sisi kulaumu tu Serikali. Kwa maoni yangu, tunazo sheria nyingi kuhusu jambo hili, lakini hazitumiki. Jambo ambalo nataka kutilia mkazo sana ni namba ile ya dharura ya 1195. Wakenya wengi hawajui kuwa kuna namba ya dharura inayoshughulikia maswala haya. Namba hii hutumika masaa 24, na pia inapigwa bila malipo. Unapopatikana na tatizo lolote kama la ubakaji, ukipiga namba hii, unapata nusra na watu wa kukusaidia hata kama ni kwa ...
view
7 Dec 2023 in National Assembly:
Asante, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi ili nichangie Hoja hii.
view
7 Dec 2023 in National Assembly:
Asante, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi ili nichangie Hoja hii.
view
7 Dec 2023 in National Assembly:
Suala la ugaidi lina utata sana. Halina dini wala kabila. Nimetoka Lamu, ambayo imekuwa katika vyombo vya habari mara nyingi kwa sababu ya mambo ya ugaidi. Wengine wamekuwa kwa vyombo vya habari kwa sababu ya utaalamu fulani, lakini sisi saa zote tukitajwa kwa habari ni kwa sababu ya mambo ya ugaidi. Eneo Bunge langu linaathirika sana na mambo ya ugaidi. Suala hili likizungumzwa, tunazungumza kutoka ndani mwa roho zetu kwa sababu ni mambo ambayo tunajua yanatuathiri. Kuna mtu mmoja ambaye ameuawa leo. Ninatoa pole zangu, kisha niendelee kuchangia Hoja hii.

Katika eneo Bunge langu, Lamu Mashariki, tumeathirika kiuchumi. Watu wanaoishi katika Wadi za Basuba na Kiunga wanaathirika sana kwa upande wa kupeleka chakula. Saa hii kuna mafuriko ambayo yamesababisha shida ingine. Usafiri ni shida kwa sababu ya magaidi. Wanaweka Improvised Explosive Devices (IEDs) kwenye barabara. Mtu akitoka Wadi ya Hindi kwenda Basuba hadi Kiunga, ni lazima atumie pikipiki kwa sababu barabara haitumiki saa hii. Hii imesababishwa na masuala ya ugaidi. Barabara iko lakini haitumiki kabisa.

Ninashukuru Serikali kwa sababu imeamua kuweka lami hiyo barabara. Saa hii haitumiki. Njia ya usafiri inayotumika ni pikipiki. Unalipa Ksh7,500 kubeba vifungu viwili vya unga ndio ufike sehemu hiyo. Eneo hilo lote la Basuba na Kiunga limeathirika kwa sababu maendeleo hayafanyiki. Ukitaka kupeleka mradi kule, unaambiwa haufanyiki kwa sababu ya utovu wa usalama. Yote yanatajwa kwa sababu ya mambo ya ugaidi.
view