Shariff Athman Ali

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 161 to 170 of 257.

  • 4 Jul 2018 in National Assembly: Ndio, Mhe. Spika wa Muda, nimekubali anifahamishe mahali ambapo ameona kwamba nahitaji kufahamika. view
  • 4 Jul 2018 in National Assembly: Asante Mhe. Spika wa Muda. Ningependa nifahamishe mwenzangu aangalie vizuri vile Mswada unasema. Hakuna mahali ambapo unasema kwamba The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 4 Jul 2018 in National Assembly: mtu atalazimika, lakini Mswada haujawekwa wazi. Hofu yangu ni kwamba kumewekwa utaratibu wa kusema kwamba ni maswala ya pesa, ardhi, bondi na kadhalika. Moja ya hizi. Ningeomba kwamba, katika hizi kuwe na kufahamika kwamba kutakuwa na maridhiano. Ndilo neno ambalo nataka liwepo hapa, kwa sababu tunapowacha wazi ni kuonyesha kwamba ni mtu atachagua mwenyewe. Lakini inafika wakati kulingana na hali tunavyoiona, wale wahusika wakuu wenye mamlaka au majukumu ya kuendesha haya inafika wakati wanakwenda na maamuzi yale wanayotaka wao. Haya tumeyaona yakifanyika katika nchi yetu. Mtu anakwenda na maamuzi, anasema ni hivi, ilhali kuna namna nyingine ya kusuluhisha swala lile. ... view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Hoja ya nidhamu, Mhe. Naibu Spika wa Muda. view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwa kuwa Kiswahili ni lugha ya kitaifa, naomba kisitumike kwa njia isiyo. Ni makosa kutumia lugha ya Kiswahili kwa namna ambayo sivyo na kuiharibu. Asante. view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia mjadala huu muhimu ambao unaangazia masuala ya afya ya Wakenya. view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Naibu Spika wa Muda, kabla ya kuendelea, nilikuwa nimeomba hoja ya nidhamu kuhusiana na suala hili nzima. Hoja hii inaonekana imetia hamasa wengi na wangependa kuchangia lakini naona muda haupo nasi maana umetupa kisogo. Pengine kupitia utaratabu wa Bunge hili, Sheria za Bunge, Kifungu Nambari 97(4), ningeomba muda wa kuongea pengine upunguzwe kutoka dakika kumi hadi tano ili wenzetu wengine nao waweze kupata fursa ya kuchangia ikiwa itawezekana. Naibu Spika wa Muda, ningependa kumpongeza Mhe. Ali kwa fikira ya kuleta Hoja hii hapa.Vile vile, ningependa kumpongeza kwa ule utafiti ameweza kufanya kikamilifu kuhusiana na suala nzima la afya katika nchi ... view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: watasaidika namna gani. Kama nilivyosema, kuna umuhimu wa kuangalia suala hili na kuliangazia kwa undani kabisa. Tatizo ni nini na limesababishwa na nini? Naibu Spika wa Muda, Hospitali ya Mombasa kwa hivi sasa hakuna asiyejua kwamba inapokea wageni kupitia kila sehemu katika masuala ya matibabu. Iwe ni wageni kutoka Lamu, Kilifi ama sehemu tofauti, wote huenda Hospitali ya Mombasa. La kusikitisha ni kuwa Bunge hili likikaa kugawanya pesa za mashinani ama za kaunti ama kugawanya pesa katika Bajeti yake kila mwaka, sijaona mambo haya yakifikiriwa. Jambo ambalo ningependekeza tunaposubiri ujenzi ambao umependekezwa wa hospitali nyingine kule Mombasa, tayari hospitali hii ... view
  • 27 Feb 2018 in National Assembly: Asante Mhe. Spika wa Muda. Ningependa kuungana na wenzangu kumpongeza Mwenyekiti wa Kamati hii pamoja na kamati yake kwa kazi nzuri ambayo wameifanya. Tunalolizungumzia leo hapa ni Mswada muhimu sana katika nchi yetu. Unahusiana na barabara zetu, mipangilio ya Serikali na utaratibu wa kuinua hali ya barabara zetu nzuri. Kitu muhimu ambacho nataka tufahamu kwanza ni kujua umuhimu wa barabara katika nchi yetu na katika ulimwengu kwa ujumla. Vile vile, nataka tufahamu katika nchi yetu ya Kenya ni hatua gani tumepiga katika suala nzima la barabara. Kwa kweli, mbali kwamba tutaipongeza Serikali ilioko kwa juhudi zake bado kuna matatizo ambayo ... view
  • 27 Feb 2018 in National Assembly: yanaonekana kupitia kwa wanakandarasi wanaopewa kandarasi hizi ama kupitia wale wahusika wanaopewa kuendesha jambo hili. Mhe. Naibu Spika wa Muda, utakubaliana nami kwamba barabara ni muhimu sana katika nchi yetu ya Kenya kwa sababu inarahisisha usafiri na vile vile inainua uchumi wa sehemu yoyote ambayo kuna barabara nzuri. Tutaweza kufaidi vipi mambo kama haya katika hili suala nzima? Tatizo liko Serikalini au wahusika vile nilivyosema? Tatizo liko kwa wahusika na kandarasi. Mhe. Naibu Spika wa Muda, Serikali inatumia pesa nyingi sana katika sekta hii ya barabara. Bilioni za pesa zinatumika kila mwaka tunapopanga Bajeti ya nchi. Mbali kwamba bilioni za ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus