3 Aug 2021 in Senate:
wanauza na kupata pesa kisha kuwaacha maskini wananchi wa Kaunti ya Taita Taveta. Katika Mswada huu, sasa tumepata uganga. Ukitibiwa na mganga na upone, huu ndio uponyaji sisi kama Wakenya katika taifa letu.
view
29 Jul 2021 in Senate:
Bi. Naibu Spika, kwa hisani yako, nipe dakika tatu nimalize. Mimi ni mmoja wa wale Maseneta ambao walikuwa jaji katika hili koti ambalo lilikuwa lina jihusisha na hili jambo la wafanyikazi.
view
29 Jul 2021 in Senate:
Bi. Naibu Spika, kwanza namshukuru dada yangu, Sen. Dullo, kwa kuuliza swali hili. Uzito wangu ni kwamba mimi ni mmoja wa Kamati ya Leba. Lakini uzito ambao unanifanya niongee ni kwa sababu ninaangalia ripoti hii ya mama mlemavu ambaye tangu azaliwe, hajakuwa sawa na wamama wengine ambao wanaweza kujitafutia lakini alipata kibarua mahali kama hapa. Tegemeo lake kubwa lilikuwa kumuona Sen. Dullo ili amweleze masaibu yaliyomkumba ili apate msaada na yamefika hapa. Bi. Spika, tunataka wafanyikazi walemavu waendelee kupata kazi. Jambo la kusikitisha ni kwamba wamefanya kazi miaka mingi pale ndani zaidi ya miaka kumi lakini leo wameambiwa waende nyumbani. ...
view
29 Jul 2021 in Senate:
Bi. Naibu Spika, kwa ruhusa, nasema ukweli kwamba ijapokuwa mimi ni Memba wa hii Kamati, sikubaliani na hii ripoti. Ndio sababu nimesema nitapata nafasi nanitasema. Siwezi kupiga makofi kwa sababu mtu amepoteza kazi na mimi ninaweka kidole na kusema ni sawa. Maoni yangu ni kwamba, afadhali uamuzi kama huu urudi tena katika Bunge la Seneti kwenye Kamati tuchunguze vizuri ili hao watu wapate afueni na warudi kazini.
view
29 Jul 2021 in Senate:
Bi. Naibu Spika, hoja yangu ya nidhamu ni kwamba yule aliyeleta kauli ile ni Sen. Olekina. Amelileta kauli hii kwa uchungu sana kuhusiana na Wamaasai ambao anawakilisha hapa. Tunaelewa kwamba Wamaasai wanapenda--
view
29 Jul 2021 in Senate:
No, no. Nataka kuongea---
view
29 Jul 2021 in Senate:
Je ni haki kwa yule mwenye kutoa kauli ambaye ni Mmaasai---
view
29 Jul 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view