29 Jul 2021 in Senate:
Bi. Naibu Spika, ninaona kuwa unamjibu na kumweleza ndugu yangu, Sen. Sakaja, sawa sawa. Wakati nilipokuwa ninazungumza juu ya wafugaji, niliongea kwa heshima. Lakini kwa sababu ulikuwa unakata kuninyamazisha, ulisimama. Sasa ninaona umejibizana na Sen. Sakaja vizuri hadi mumeelewana ilhali hukukubali kuelewana na mimi nilipokuwa ninazungumza juu ya wafugaji wa mifugo, na wafugaji wa mifugo wanaojulikana Kenya nzima ni Wamaasai--- Bi. Naibu Spika, hii ni kwa heshima. Nilipotaja hivyo, ulisimama. Nilikuhisi nikakuambia kama nilikukosea kutaja hili jina la “Maasai,” basi uketi ili niweze kuendelea. Nilisema nitatumia jina “mfugaji”. Hivyo ingekuwa vizuri, kwa maana tungekuwa tumeelewana. Sasa wewe uliposimama ulifanya mimi ...
view
29 Jul 2021 in Senate:
Ni kwa sababu nimesikitika. Umempatia Sen. Sakaja nafasi nzuri ya kujieleza, ilhali hukunipatia nafasi nzuri ya kujieleza.
view
28 Jul 2021 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Kwanza nampa shukrani Sen. Were kwa kuleta Mswada huu wa uchapishaji wa taarifa na magazeti inayohusu yanayojiri katika serikali za kaunti. Ni jamabo lililokuja wakati unaofaa. Tunahitaji kuona kwamba sheria za kaunti zimeweza kukimu ili zisaidie watu walio nyumbani.
view
28 Jul 2021 in Senate:
Mara nyingi kumekuwa na ucheleweshaji wa kuchapisha taarifa katika serikali za ugatuzi. Imekuwa ni lazima waje Nairobi wapate kibali kutoka kwa mchapishaji wa Serikali ya Kitaifa ili taarifa zao zichapishwe katika gazeti la Serikali. Hivi sasa, tunasema kwamba pia kaunti ziwe na uwezo--- Ikiwa ndani ya serikali zao kuna mambo yanayo hijitaji kuchapishwa, itakua rahisi zaidi.
view
28 Jul 2021 in Senate:
Bw. Spika, hii ni sawa kabisa, na hakuna ukiukaji wa sheria. Mkondo kama huu unaweza kusaidia sana katika kaunti. Hapo kitambo kidogo tulipitisha kwamba kuwe na mkuu wa sheria katika serikali za ugatuzi ambaye ni county attorney. Tunapo ongea sasa, kuna wakuu wa sheria katika kaunti zote 47 Kenya. Hivi basi, ikiwa uchapishaji utapata kiongozi wa uchapishaji taarifa ambazo zitakuwa zinalemea kaunti 47, itakuwa ni sawa kabisa.
view
28 Jul 2021 in Senate:
Bw. Spika, imekuwa bora kuwa katika uchapishaji wa Mswada huu, kuna watu wengi wana njia nyingi za kufanya ukora ama ufisadi. Wanaweza kuleta mambo ambayo yanaweza kuchapishwa na hatimaye hayo mambo yawe ni uongo ama hayawezi kufanyika, ilhali yanapatikana katika lile gazeti.
view
28 Jul 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
28 Jul 2021 in Senate:
Adhabu imepeanwa. Ikiwa mtu atakiuka sheria hii ama kutakua na uchapishaji bila ruhusa ya yule anapeana ruhusa ya kuchapisha, basi huyo huenda akalipa zaidi ya laki nzima, ama awe na kifungo. Hii itakuwa onyo kali sana. Mswada huu ukipita utasimamisha wale ambao wana nia kama hiyo.
view
28 Jul 2021 in Senate:
Bw. Spika, tunaona kuwa mchapishaji wa gazeti la kaunti ni lazima awe amesoma. Lazima awe na shadaha ambayo inahusiana na uchapishaji wa magazeti ya Serikali. Hili hi jambo muhimu kwa sababu si kila mtu anaweza kuwa mchapishaji. Kila uchapishaji unakua na taaluma yake. Ni vizuri kwamba kutakuwa na mtu ambaye amesoma katika kila kaunti. Atakua na uwezo wa kupitisha uchapishaji wa taarifa yoyote ambayo itachapishwa.
view
28 Jul 2021 in Senate:
Bw. Spika, la mwisho kabisa ni uzuri wa Mswada huu ambao unaleta mwelekeo katika kaunti. Hakuna chochote kinaweza kufayika katika kaunti bila kuchapishwa. Wananchi watapewa taarifa ili wajue ni nini inayojiri na ni nini ilichapishwa na inahijati maono ya wananchi ili wajue ni njia gani watafuata katika siku za usoni.
view