28 Jul 2021 in Senate:
Ninaunga mkono Mswada huu.
view
14 Jul 2021 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Kwanza, ninamshukuru Sen. Kasanga kwa Taarifa yake. Katika nchi nzima ya Kenya, tunajua hakuna familia ambayo imekosa mtu mwenye akili punguani.
view
14 Jul 2021 in Senate:
Sote tuliyo hapa tuko na majukumu ya kuangalia familia zetu na wengine wako na akili punguani. Mimi nina mtu wa karibu mwenye akili punguani.
view
14 Jul 2021 in Senate:
Mara nyingi, Serikali imekuwa ikitilia mkazo zaidi mambo ya hospitali. Hivi juzi, imetilia mkazo zaidi upande wa virusi vya korona. Imetilia mkazo pia upande wa cancer . Hiyo ni sawa kabisa. Lakini kwa upande mwingine, Serikali imelegeza mkono hususan kwa watu wenye akili punguani. Hapa nchini, ni hospitali chache ambazo zinatoa matibabu kwa watu wenye akili punguani. Ninavyoelewa mimi, zipo hospitali mbili tu ambazo zinajulikana sana kwa kutoa matibabu kwa wagonjwa wa aina hii. Katika sehemu ya pwani, Hospitali ya Port Reitz ndio inajulikana sana. Ukija Mji wa Nairobi, ni Mathari National Teaching and Referral Hospital. Hospitali ya Serikali iliyoko ...
view
14 Jul 2021 in Senate:
Jambo la kusikitisha ni kwamba hivi leo ukiambiwa kwamba mtu wako amepatikana na akili punguani na ameambiwa aende Port Reitz utashangaa ukienda pale, ukiona vile wale watu wenye akili punguani wanavyoishi. Wanawekwa katika hali dhaifu ya kwamba hata pengine kama ulikuwa umeenda pale na huna akili punguani kama vile alivyosema huyu ndugu yangu Sen. Mutula Kilonzo Jnr., sisi sote kama binadamu inafika wakati ambapo akili zetu zinapungua, basi ukifika pale utashikwa na akili punguani kwa sababu ukosefu wa vifaa na hali ya udhaifu. Bw. Spika, ninaona ya kwamba ingekuwa vizuri ikiwa Serikali itahakikisha ya kwamba kila kaunti iwe na uwezo, ...
view
14 Jul 2021 in Senate:
Bw. Spika, kuna lugha ile ambayo unaweza kuitumia ikawa lugha ya fasaha. Ukisema ya kwamba yule ni mtu mwendawazimu, hiyo ni matusi kwa yule mtu ama jamii ile iliyo na yule mgonjwa mwenye akili punguani. Akili punguani ni neno ambalo limetambuliwa katika kutumia lugha ya Kiswahili kwamba mtu akiwa akili yake haiko timamu, basi anaitwa mwenye akili punguani; haitwi mwendawazimu. Kumuita mtu mwendawazimu ni kumdharau. Ni kama vile ndugu yetu yule ambaye hayupo hapa sasa Sen. Mwaura; kuna majina tofauti tunaweza kumuita. Lakini sasa tunamuita mtu mwenye ulemavu yule hawezi kujisaidia. Huwezi kumuita nguchiro, ambalo ni jina la kumdharau mtu. ...
view
14 Jul 2021 in Senate:
Ningependa kumsifu sana ndugu yangu Murkomen kwa sababu leo amejaribu sana.
view
14 Jul 2021 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda. Kwanza nataka kumpatia kongole ndugu yangu Sen. Cherargei wa Kaunti ya Nandi kwa hilo Ombi lake kuhusiana na wale askari ambao wanaegeza usalama wakati wa jioni. Utaona kwamba sasa hivi vitu vinawekwa pale kama chuma za kuzuia magari hata imekuwa tena sio kuzuia magari pekee yake, lakini pia wanazuia watu. Mara nyingi umeona kwamba vijana wetu ambao huwa wanaketi katika maeneo hususan wale wanatafuta riziki ambao wanaipata wakati wa jioni watu wametoka kazini wanaenda The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained ...
view
14 Jul 2021 in Senate:
nyumbani. Wakati wakishashukishwa mahali katika kituo cha basi, wanachukua boda boda na kwenda nyumbani. Utakuja kuona kwamba boda boda ndio watu wanapewa shida zaidi sana na hivi vizuizi barabarani. Mtu amebeba abiria na anaambiwa kila safari atakayopita katika hicho kizuizi ni lazima awache Kshs50 akienda na akirudi. Utapata kwamba kama safari yake ilikuwa leo atengeneze Kshs200 atakuwa na Kshs100. Pengine ana familia ya kuangalia na ile piki piki ameikodisha na inahitaji petroli. Mwenye hiyo piki piki pia anataka kitu hapo ndani. Sasa unapata ni hasara tupu vijana ambao wanafanya kazi ya boda boda. Bi. Spika wa Muda, tunasema kwamba hivi ...
view