Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1151 to 1160 of 2266.

  • 14 Jul 2021 in Senate: Ungenipatia dakika moja nimalize kwa hisani. view
  • 14 Jul 2021 in Senate: Asante, Bi Spika wa Muda. Kwa ukarimu wako mimi nasalimu amri. Wale watu ambao wanateseka zaidi ni waendeshaji wa boda boda. Ni heri kuwe na sheria ambayo itaweza kufuatwa ili wakati wakiwa wanavuka pale kwenye kizuizi, polisi wawache kuchukua hongo kutoka kwao. view
  • 14 Jul 2021 in Senate: Asante Bi Spika wa Muda. Mimi nikiwa kama mmoja wa wale watu ambao walikuwa Jaji na tukaweza kustaafu, ni jambo la kusikitisha sana. Tunajua koti sio jengo ama nyumba. Koti ni hakimu. Hata akiwa mahali popote, yeye bado ni hakimu. Ukimpatia Jaji hema na kiti chake cha kuketi na meza, hiyo imetosha; hiyo ni koti. Kwa watu wa Kericho ni jambo la aibu na kusikitisha kuona ya kwamba ikiwa Serikali ilkubali ama kuachilia koti kufungwa na watu wa Kericho kukaa bila mahakama, ni jambo la kusikitisha. Kuna mambo mengi sana ambayo yalikuwa yanatokea wakati nilikuwa Jaji. Nilikuwa ninapata malalamishi kwamba, ... view
  • 14 Jul 2021 in Senate: Hao wahalifu wakishikwa wanapelekwa jela na kurundikwa. Hawaendi kotini. Hii jambo ambalo lazima tulitafakari. Ni muhimu hatua ichukuliwe mara moja kuona ya kwamba Koti ya Kericho imefunguliwa. Asante. view
  • 7 Jul 2021 in Senate: Bw. Spika, kwanza namshukuru ndugu yangu, Seneta wa Kaunti ya Mombasa, Sen. Faki, kwa kuleta ombi hili la wafanyikazi wa KUSCO. Wafanyikazi 171 sio wachache. Tusiangazie wafanyikazi hawa pekee yao. Wafanyikazi hao wanafamilia; mabibi, ndugu, watoto na watoto wa ndugu wanaowategemea. Familia za kiafrika, watu hutegemeana na kushirikiana sana. Mara kwa mara wafanyikazi wengi huwa wanaishi hata na watoto wa ndugu pasi na familia yake. Familia za kiafrika ni kubwa. Wafanyikazi 171 ni nambari kubwa. Mfanyikazi mmoja anaweza kuwa anategemewa na watu zaidi ya mia moja. Ni kosa kubwa kwa wafanyikazi wa KUSCO kukosa kulipwa ridhaa zao. Wizara ya Leba ... view
  • 7 Jul 2021 in Senate: na hatimaye kuhakikisha wafanyikazi wote 171 wameshughulikiwa na wakuu wa kampuni ya KUSCO wameshikwa na kulazimishwa kuwalipa pesa za wafanyikazi hao. Pesa za wafanyikazi 171 sio kidogo. Hiyo ni zaidi Kshs12 milioni. Hizo sio pesa kidogo hasa kwa wakati huo. Pesa hizo ziko na faida yake. Ikiwa zitalipwa, basi wale wakurugenzi na kila mtu lazima ashurutishwe alipe pesa hizi. Asante, Bw. Spika. view
  • 7 Jul 2021 in Senate: Asante Bi Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii. Ningependa kumsifu ndugu yangu Sen. Khaniri kwa kuleta Hoja hii kuhusiana na mambo ya Korona. Tunaelewa ya kwamba ni karne kuanzia sasa ambapo ugonjwa huu haukuwa katika ulimwengu. Lakini karne hii imeleta maradhi aina ya Korona ambayo imeleta huzuni katika familia nyingi sana, sio katika Kenya pekee yake lakini katika ulimwengu mzima. Hatari ambayo Serikali yetu haijazingatia ni kwamba haijatia mkazo vile inaweza kuzingatia jinsi watu wa Kenya wanaweza kuishi ili waweze kuepukana na hili janga la Korona. Tumeona ya kwamba Wakenya wengi wameweza kupoteza kazi. Kazi zilikuwa zikifanywa kuanzia asubuhi ... view
  • 7 Jul 2021 in Senate: Bi. Spika wa Muda, la mwisho ni kwamba, hapo awali tulikua na kamati ya kuleta ripoti maalum. Tukiweka mkazo zaidi na njia maalum, nafikiria kuwa Wakenya watapendelea Seneti kuwapatia njia mwafaka ya kutumia hizi dawa na kupunguza ufisadi katika serikali za ugatuzi. Itawafaa Wakenya. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 7 Jul 2021 in Senate: Asante. view
  • 18 May 2021 in Senate: Shukran, Bw. Spika wa Muda. Kwanza, ninampa kongole Bw. Kevin Ndobo Macharia, wakili ambaye ameleta hili ombi. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus