Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1161 to 1170 of 2266.

  • 18 May 2021 in Senate: Ulegevu wa huduma za sheria katika hizi korti umekithiri. Yote haya yanaletwa na hili janga la homa ya korona au COVID-19. Hususan, mawakili wanapata shida kutafuta tarehe ya kesi zao kusikizwa kupitia kwa matandao. Sio kama zamani ambapo mawakili wangeenda kortini, kuorodhesha kesi na kutetea wateja wao mara moja. Wakati huu, kesi zinalegea na haki za wananchi kucheleweshwa. Kama tunavyojua, ikiwa haki itadidimia kwa mwananchi, ni sawa na kusema mwananchi amenyimwa haki. Kumnyima mwananchi haki yake ni makosa. Katika Kaunti ya Kilifi, kesi za mashamba ndizo zinachelewa zaidi. Imekuwa vigumu sasa kwa watu kuwania na kuzuia cheti cha dharura. Sasa ... view
  • 18 May 2021 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda. Je, kuna haki katika msemo wa ndugu yangu ya kwamba ‘wakati Serikali ya Jubilee ilikuwa ikifanya kazi’? Hiyo ni kumaanisha kwamba hivi sasa haifanyi kazi ama inafanya kazi. Nakumbuka kuwa ndugu yangu, Sen. Cherargei, ni mwanachama sugu ambaye yuko katika hili Bunge la Seneti kupitia kwa tikiti ya Jubilee. Leo akiwa hapa anatoa matamshi kama hayo. Je, ni haki kusema kuwa chama ambacho kinatawala, yeye akiwa mmoja wao, hakifanyi kazi? view
  • 18 May 2021 in Senate: Asante sana, Bw. Spika. Ningepemda kujiunga na stetimenti hii ambayo imeletwa na ndugu yangu, Sen. Mohamed Faki wa Mombasa. Kama tunavyoelewa, Kenya iko katika radar au map ya ulimwengu. Matumaini yangu ni kwamba watu wengi sana katika Kenya, hususani wakiwa ni wakrsito, wameweza kwenda kule. Hii ni kwa maana ile ndio kama maka yao kwenda kuona pale Yesu alizaliwa, makalio yake, na aliishi vipi pande hizo zote za Jerusalem. Tunaona kwamba, kukiwa na uhusiano bora katika yale maeneo baana ya Waisreaeli and Filistini huenda kukawa na Amani na maendeleo. Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba Israeli hivi leo inachukuwa mkondo ... view
  • 18 May 2021 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 18 May 2021 in Senate: Lakini tunaona ya kwamba baada ya yeye kuondoka wale waliochukua utawala katika upande wa Israeli ikiwamo huyo Waziri Mkuu aliyepo sasa, haiandamani na yale mambo ambayo yaliwekwa ya amani wakati ule. Kwa hivyo, hata kama Yasser Arafat alikiuka haki za watu, wale walioko kama viongozi ni muhimu waweze kukaa, kuongea na kuona ya kwamba kila wakati wanapotumia zile zana zao za vita wanaokufa ni raia sio wanajeshi. Hii ni kwa sababu wanajeshi wanajua mbinu za kujitetea. Hii hasara ambayo Israeli inapeleka saa zote kwa Wapalestina ikome. Kama alivyosema ndugu yangu Sakaja sisi tunaketi katika kile kitengo cha juu sana katika ... view
  • 18 May 2021 in Senate: Asante sana, Mhe. Bwana Spika wa Muda. Kwanza ninampongeza huyu Paulo Kiprotich. Hali wanayoipitia watu hawa wa Torobeek si nzuri. Kwa mara nyingi tumekuwa tukiona Wakenya wanagawanyana kwa sababu ya msingi kama huu. Si haki ikiwa kila mtu hapa anaishi kama Mkenya kuweza kudharau Wakenya wengine. Ninasema hivi kwa sababu hawa kama alivyosema Sen. Cherargei, pia ni Wakenya. Wanatakikana kutambuliwa na serikali na sheria. Tunajua kuna wale watu wanaitwa Wadorobo ambao wanaishi huko kwenye milima na misitu. Lakini katika miaka na vikaka, hao hawajaharibu ule msitu. Ikizidi zaidi wanautunza. Ni jambo la aibu hivi leo kuona ya kwamba ni Serikali ... view
  • 18 May 2021 in Senate: Bw. Spika wa Muda, ardhi ni kitu muhimu sana katika nchi yetu ya Kenya. Watu wengi wamekuwa wakitengeneza hati milki bandia. Kama kuna zile tunaita stakabadhi za bandia, ziko nyingi sana kupita kiasi ndani ya Kaunti ya Kilifi. Watu wengi sana wamepata taabu kuweza kufurushwa katika mashamba yao kwa sababu mtu amekuja na cheti. Watu wameishi hapo zaidi ya miaka arobaini ama sabini. Watoto wamesoma, mababu wamekufa na wamezikwa hapo. Kila mtu amezikwa hapo na kuna makanisa na shule watu wanaenda. view
  • 18 May 2021 in Senate: Bw. Spika wa Muda, nipatie dakika moja niweze kumaliza kwa hisani yako. view
  • 18 May 2021 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda kwa imani yako. Nilikuwa naweza kumaliza tu kwamba familia ya Mzee Charo Abaha hivi sasa ziko kule mwendo wa panya. Zote zimeweza kufurushwa katika ardhi zao ambazo wameishi miaka na vikaka hali ikiwa ni madharau matupu ambayo yameendelea. Wale watu waliowafukuza ni watu ambao wako na stakabadhi za bandia. Tunasema ya kwamba Serikali lazima ichukue hatua itetee watu hawa ambao ni wanyonge, wako chini na wameishi katika ardhi hiyo. view
  • 18 May 2021 in Senate: Bi. Spika wa Muda, shukrani kwa kunipa nafasi hii. Nataka kusema ya kwamba ametamka akisema ya kwamba siku zinazokuja hapo mbeleni. Hiyo ni sawa kabisa, tumemuelewa. Lakini kitu kizuri Sen. Cheruiyot angesema ni siku za usoni. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus