18 May 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
18 May 2021 in Senate:
Ni hayo peke yake nilikuwa nataka kusema. Lakini la muhimu zaidi ni kwamba nataka nimpatie kongole sana Sen. Cheruiyot kwa ujasiri wake wa Lugha ya Kiswahili. Ameongea Kiswahili mufti ambacho hata mimi nimekipenda.
view
18 May 2021 in Senate:
Seneta wa Kericho, keep it up. Hiyo ni shining hapo. Asante, Bi. Spika wa Muda.
view
18 May 2021 in Senate:
Bi Naibu Spika wa Muda, kama ingekuwa mtihani wa Kiswahili, nafikiria ndugu yangu Sakaja, ama wale wanaomuita “Saks” kama mimi, ningekuwa nimempatia asilimia 99 juu ya mia moja. Ameongea Kiswahili sanifu ambacho kimeeleweka katika kuchangia katika huo mjadala wa kuhusikana na Mhe. Suluhu, Rais wa Muungano wa Jamhuri ya Tanzania, ilikuwa jambo la kutabasamu. Ninafurahi sana na ningependa kumhimiza, aendelee na moyo huo huo. Endelea na Kiswahili hicho hicho na nina hakika kila mtu katika Kenya leo amekuskia ukiongea Kiswahili, tena sio kile Kiswahili cha sheng, ni Kiswahili mufti. Asante Bi. Spika wa Muda.
view
11 May 2021 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, the people of Kilifi vote yes.
view
11 May 2021 in Senate:
Bi Naibu Spika, asante sana kwa kunipa fursa hii. Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa uwezo wa kuketi hapa kama Maseneta na kujadiliana na hatimaye kupitisha Mswada huu wa Constitution of Kenya (Amendment) Bill, 2020. Nina uhakika kwamba tutakapoenda kwa kura ya maoni, kazi tuliyofanya hapa imeonekana na kila mtu katika taifa letu la Kenya. Nimefurahi kwamba Maseneta wamendeleza majadiliano kwa hali ya ungwana bila kukosana na hatimaye kupiga kura na kupata muelekeo. Tumewaonyesha Wakenya muelekeo wa kufuata. Tutazidi kuwa himiza Wakenya mashhinani kupitisha Mswada huu utakapo pelekwa kwa kura ya maoni mashinani.
view
11 May 2021 in Senate:
Shukran, Bi. Naibu Spika. Kwanza, natoa shukran kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan. Tuna mshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia kwa sababu tunawazia jambo muhimu ambalo alileta. Kitu cha kwanza, tunawapa kongole watu wa Tanzania kwa sababu katika historia ya nchi hiyo, kutoka wapate uhuru mpaka sasa, ni Rais wa kwanza mwanamke katika Muungano wa Mashariki ya Kati. Bi. Naibu Spika, sisi kama watu wanaotoka sehemu ya Pwani tunajua kuzungumza Kiswahili. Lakini, Rais wa Muungano wa Jamhuri ya Tanzania aliweza kuongea Kiswahili safi. Nilipokisikiliza, nilisema hata kama tunatoka maeneo ya Mombasa, Kilifi ...
view
11 May 2021 in Senate:
Bi. Naibu Spika, tunaelewa kwamba mipaka yetu na Tanzania imekuwa imara kwa miaka na miaka nyingi na itaendelea kuwa hivyo. Hatujui lakini tunaambiwa katika lugha ya dini kwamba maisha na maisha tutaendelea kuwa majirani. Rais Suluhu alituambia kuwa ikiwa wanyama wanaweza kuishi kama ndugu na kutembea pamoja--- Alitupatia mifano ya kwamba ikifika mwezi fulani mwakani, wanyama wa kiume
view
11 May 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view