Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1181 to 1190 of 2266.

  • 11 May 2021 in Senate: huridhishwa sana kwa sababu wale wanyama wa Tanzania wa kike huwa wanavuka mto nakuja Kenya. Wanapata mimba na kurudi kwenda kuzalia huko kwao. Hatusemi kwamba wao wanakuwa wengi kwa kuwa wengine huwa wanabaki huku, na ndio jinsi ya watu wanaoishi pamoja kuweza kuelewana na kuishi kama ndugu na dada. view
  • 11 May 2021 in Senate: Bi. Naibu Spika, tumeona katika mipaka hiyo kuwa sio wanyama pekee yake. Katika maeneo tofauti ya mipaka kuna jamaa ambao wanaishi pamoja. Tukiangalia upande kama Pwani, ukitaka kwenda Tanga ama Dar es Salaam unaweza kupitia maeneo ya Horohoro ama Lungalunga. Hiyo ni mipaka ambayo jamaa wa Kidigo katika Jamii ya Mijikenda wanaishi, humu nchini na vile vile upande wa Tanzania kupitia sehemu za Tanga na Dar es Salaam. Ikiwa wanyama wanashirikiana na binadamu kuketi pamoja, biashara zetu pia zinaweza kuwa pamoja. Tukija katikati tuko na eneo ambalo liko na Wataita na Taveta, ambao wako Voi na ni wengi. Nao pia ... view
  • 11 May 2021 in Senate: Vile vile, tuko na eneo la Namanga. Ukitoka hapa Nairobi utapita eneo la Namanga. Kule kuna Wamaasai. Bi. Spika wa Muda, nakusifu kwa sababu wewe ni mmoja wao. Ikiwa mnaishi kwa amani upande wa Namanga Kenya na upande ule mwingine. Hatuwezi kujua tofauti kwa sababu majina yanafanana. Vile mnaishi na tabia zinafanana. Ukienda upande wa Namanga kule Tanzania, Wamaasai wanaoishi kama ndugu. Kwa hivyo, ni jambo ya kufurahisha ikiwa Rais wa Tanzania anaweza kuja hapa na kutueleza kwamba wanyama wanashirikiana, binadamu wanashirikiana na mipaka iko pamoja. Sisi tunaishi kama ndugu na hatuwezi kugeuza Maisha kwanzia sasa na milele. La muhimu ... view
  • 11 May 2021 in Senate: Bi. Spika wa Muda, katika Hotuba yake, alisifu Bunge la Seneti na Bunge la Kitaifa akisema kwamba ni jambo bora aliyoiona. Ni kwamba tunaongea Kiswahili ambacho ni cha kufurahisha sana. Kama alivyokuwa akisema Kiogozi wa Walio Wengi, alijaribu kuongea lakini katikati akageuza; ni kama maji yalizidi unga. Akasema kwamba angependelea kuongea kwa lugha ya Kiingereza, lakini hiyo ni mojawapo ya tafakari zetu. Kiongozi wa Walio wa Wengi amejaribu sana. Ni mara yangu ya kwanza kusikia akiongea Kiswahili. Ni kizuri lakini labda alikuwa na hofu ya kukosea. Nina matumaini makubwa ya kwamba kwa vile sasa tuko na ile Hotuba yake katika ... view
  • 11 May 2021 in Senate: Bi Spika Muda, ningependa kuongeza zaidi kuwa isikuwe ya mwisho. Katika Kanuni za Seneti, ikiwa tunaweza kuruhusu mtu aanze kwa lugha ya Kiswahili ama Kiingereza na hawezi tafsiri neno katika lugha ya Kiingereza ama Kiswahili aweze kulisema kwa lugha yoyote. Kwa mfano katika sentensi anaweza kusema ‘ goodmorning ’ ikiwa hawezi kusema ‘habari ya asubuhi.’ Hufai kukosolewa kwamba view
  • 11 May 2021 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 11 May 2021 in Senate: umefanya makosa. Kuna ule uoga ya kwamba nikiongea hivi naweza kuongea makossa, kwa hivyo, afadhali niongee Kiingereza. Tukirekebisha taratibu zetu za Bunge, inaweza kuwa vizuri zaidi kwa sababu itapeana nafasi kwa Seneta yeyote ambaye ana uwezo wa kuongea, hatumaye akiona hataweza kumaliza sentensi kwa lugha ya Kiingereza anaweza kutumia lugha ya Kiswahili. Katika Bunge la Tanzania inakubaliwa kuanza kwa lugha ya Kiswahili kisha kutumia maneno ya Kiingereza. Tukirekebisha taratibu zetu itakuwa sawa. view
  • 11 May 2021 in Senate: Mwisho ni kumsifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aligusa jambo la janga hili la COVID-19. Alisema kuwa sisi kama majirani tunaoishi na kufanya biashara pamoja, tunashirikiana kwa mambo mengi. Ikiwa ushirikiano huo utaendelea, ni vizuri kulipiga vita janga hili pamoja. Kenya imeendelea mbele zaidi kupiga vita hili janga ya COVID-19, lakini upande wa Tanzania, kidogo walienda pole pole. Jukumu letu ni kutia maanani Hotuba ya Rais ya kwamba wamekubaliana kuanzisha--- Nilifurahi sana nilipoana kwamba wote waliokuja katika ziara hii na kuingia Bungeni kusikiza Hotuba ya Rais walikuwa wamevaa barakoa wote. Hiyo ni ishara kuwa wao pia wana juhudi ... view
  • 11 May 2021 in Senate: Nashukuru Mwenyezi Mungu kwa sababu sisi tulitilia maanani hapo awali na tukasema ya kwamba tutapigana na Korona mpaka tuone ya kwamba tumeishida ama vile wanavyosema, ule mzunguko tumeunyorosha. view
  • 11 May 2021 in Senate: Bi. Spika wa Muda, nataka nitie mkazo ya kwamba ile Hotuba ya Rais ilikuwa ya maana sana. Nilifurahishwa sana wakati aliposema akiwa huko Tanzania aliweza pia kutambua ya kwamba majina yetu huwa yanafanana. Sio ya wale Maasai peke yake lakini pia akatuambia ya kwamba kwa sababu yeye anatoka sehemu za kisiwani huko Zanzibar, kuna majina kama ya ndugu yetu ambaye tuko naye hapa, Sen. Mwinyihaji Faki. Alisema kuwa jina hilo pia linatoka katika kisiwa cha kule sijui ni Pemba ama ni Zanzibar. Huko nako ndiko wako na majina kama hayo. La mwisho--- view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus