11 May 2021 in Senate:
Bi Spika wa Muda, shukrani kwa kuniongoza. Nakumbuka alisema kwamba kule pia kuna majina ya Kikamba. Hata Kilonzo ama Musyoka, tunawezapata majina kama hayo. Sen. Mutula Kilonzo Jnr. anajua zaidi. Bi. Spika wa Muda, nawe pia unaelewa zaidi. Kwa hivyo, wale ambao tunaishi kama ndugu ni hususan kuona ya kwamba tunajisaidia wakati kama huu wa hili janga la Coronavirus disease (COVID-19). Kiswahili chetu ni lazima tukidumishe na tujivunie. Sio kwamba kama hujui Kiswahili ama Kizungu basi wewe sio Mkenya, kwa sababu hizi ndizo lugha zetu mbili za kitaifa.
view
11 May 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
11 May 2021 in Senate:
Nataka nikome hapo na tumsifu sana Bi. Spika wa Muda kwa hii Hoja. Naunga mkono ama ku- second . Siwezi kujua kama ‘ second’ ni kuunga mkono ama ni kufanya nini. Pia mimi nimetumia jina la Kizungu. Asante Sana, Bi Spika wa Muda. Nina second.
view
11 May 2021 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, kwa heshima na taathima, kulingana na Kipengele 105(1) cha Kanuni za Kudumu za Seneti, naomba mjadala huu uahirishwe. Naomba aliyekuwa Mkuu wa Sheria, Sen. Wako, aniunge mkono.
view
6 May 2021 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, allow me to support and second the Senate Majority Leader on the names provided to the Senate. Senators who have been named here, starting with Sen. Sakaja all the way down, are quite capable of investigating this matter of the Governor of Wajir County. Let me single out Senators like Sen. Linturi who is basically doing his masters on impeachment of governors. I believe his knowledge up to now will go a long way in helping this Committee. We also have a senior counsel here in the name of Sen. Omogeni who is a renowned lawyer. We ...
view
4 May 2021 in Senate:
Bi Naibu Spika, kama ni kutafsiri, hiyo sio hoja ya nidhamu.
view
4 May 2021 in Senate:
Ama kwa sababu tunaunga mkono ndio sasa imekuwa---
view
4 May 2021 in Senate:
Bi Naibu Spika ninaunga mkono Mswada huu. Kipengele cha kwanza cha Katiba kinasema kwamba- “Mamlaka yote makuu ni ya wananchi wa Kenya na yanaweza kutekelezwa tuu kulingana na Katiba hii” Hii inamaanisha Mkenya yeyote pahali popote alipo amepewa jukumu la kuambia aliyemchagua ni kitu gani anatakikana kutafuta, kusema au kuwakilisha katika Bunge.
view
4 May 2021 in Senate:
Hoja ya nidhamu, Bw. Spika. Taratibu za Bunge la Seneti zinaeleza kwamba huwezi kumtaja yeyote ambaye hayuko ndani ya Bunge au hajaitwa Bungeni na hawezi kujitetea. Je, ni haki kutusi au kutumia lugha isiyofaa kwa viongozi wa Kenya, hususan Baba, Raila Odinga, na kiongozi wa Taifa la Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta? Ni haki kwa kijana ninayemjua na kumpenda sana, ndugu yangu, Sen. Cherargei, Seneta shupavu sana wa Kaunti ya Nandi, kutumia lugha kama hiyo anapojadili ugeuzi huu wa Katiba? Je, kitendo kama hicho ni sawa?
view
4 May 2021 in Senate:
Kipengele cha pili kinasema ya kwamba Wakenya wataamua utawala wao kupitia kwa wale wanao wachagua ndani ya Bunge.
view