Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1201 to 1210 of 2266.

  • 4 May 2021 in Senate: Maseneta wengi wamechaguliwa na wengine wameteuliwa. Lakini, sote tumepewa majukumu na wale tunao wawakilisha hapa ndani ya Bunge. Kule nyumbani kuna sitofahamu ya watu ambao hawawezi kuelewa. Kwa Kiswahili tunasema ya kwamba ‘mto au maji hufuata mkondo’. Lazima tujukumikie waliotupa mamlaka haya ya kuja kuwawakilisha ndani ya Bunge kwa kusema, kuyanakili na kuyatimiza. view
  • 4 May 2021 in Senate: Watu wa nyumbani walipiga kura nakupitisha Mswada huu. Kwa hivyo ni jukumu langu kama kiongozi wao ndani ya Bunge pamoja na dada yangu, Sen. Zawadi, kuwakilisha na kutetea haki zao hapa ndani. Ndio sababu ninasimama hapa nikisema ya kwamba niwajibu wetu kupitisha Mswada huu. Ndio sababu ninasema ninaunga mkono. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 4 May 2021 in Senate: Watu waliweka vidole vyao Kenya nzima katika fomu ambazo zilikuja na kuthibitishe ya kwamba wanaunga mkona Mswada huu. Katika ulimwengu mzima, hakuna Katiba iliyo sawa. Nina maanisha ya kwamba sisi kama wakoloni wa Uingereza, wako na Katiba Nzuri. Lakini sio hao pekee, Waamerika wako na Katiba pia. Lakini, Waingereza waliotutawala hawana Katiba. Wao wanaiita kwa Kizungu un-writtenConstitution . Katiba ya USA ambayo imekuwa ikiwaongoza kwa miaka mingi, mara kwa mara imeweza kufanyiwa--- Jambo la kushangaza ni kwamba ile un-written Constitution ya Uingereza inawaezesha kujitawala. Katika Mswada huu, kuna kasoro kidogo ambayo imeweza kutendeka. Ndio sababu watu wengi wamesema kuigeuza italeta ... view
  • 4 May 2021 in Senate: ni ingine. Kwa hivyo, akuwe ndani ya ofisi ya Jaji Mkuu na JSC iachiwe uchapakazi wakutafuta, kuangalia au wakiona kama mwenzao ako na shida ama amepatikana na hatia waandika kwa Rais ili ateua jopo lake analolifikiria kama Tribunal ya kumwangalia jaji na hatimaye chochote kitachotoka hapo kipelekwe kwa Rais na hatua ichukuliwe. Lakini, kwa hivi sasa, hatuoni umaarufu au haraka ya kugeuza sheria kama hiyo. Naibu Spika, kuna mambo mazuri ndani Mswada huu. Jambo la kwanza, kunayo faida ya kuona ya kwamba ugatuzi ndani ya serikali za mashinani umekithiri. Kwa sababu hiyo, kuna bahati ambayo imetoka. Kuna wengine wameweza kupata ... view
  • 4 May 2021 in Senate: Bi. Naibu wa Spika, ninaposema hivi, isibainike kwamba pengine Sen. Orengo anapinga. Vile ndugu yangu, Sen. Wetangula, alitangulia kusema, itafika wakati ambapo The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 4 May 2021 in Senate: yeye pia atapiga kura. Siwasemei lakini nina hakika kwamba kura yao itakua ya kupitisha huu Mswada. view
  • 4 May 2021 in Senate: Kuna tamaduni mbalimbali hapa Kenya. Zingine ni mbaya na zingine ni nzuri. Mimi ninatoka upande wa Pwani na katika tamaduni zetu, mtu angekufa angepakwa jivu ili kuhifadhi mwili. Siku hizi, kuna vyumba vya kuhifadhi maiti ambako mtu akifariki, mwili unapelekwa kuhifadhiwa kwa siku kadhaa. view
  • 4 May 2021 in Senate: Tamaduni zingine kama za kutahiri watoto wa kike zimepitwa na wakati. Kwa hivyo, hii sheria pia ‘haijaketi’ bali ‘inatembea. Mara kwa mara, tunataka kugeuza. Hata sheria yoyote ulimwenguni lazima igeuzwe kuambatana na wakati. Wakati huu ambapo ni sisi tuko, tugeuze tunachoweza kugeuza. Kile tusichoweza, kitageuzwa na watakaokuja nyuma yetu. view
  • 4 May 2021 in Senate: Langu ni kuunga mkono nikisema kwamba tupitishe huu Mswada. Asante. view
  • 13 Apr 2021 in Senate: Shukran, Bw. Spika. Kwanza ningependa kutoa kongole kwa niaba yangu na ya watu wa kaunti ya Kilifi kwa ndugu yangu, Sen. Abdulkadir Haji, hususan watu wa Garissa kwa kumchagua Sen. Abdulkadir Haji kama Seneta wa Garissa bila upinzani wa aina yoyote. Sen. Abdulkadir Haji ni kitinda mimba wa Seneti. Kawaida ya sisi watu wa Pwani na Wakenya kwa jumla, huwa tunasema kwamba kitinda mimba ni mtoto wa mwisho anayependwa na kila mtu. Ninahakika kwamba tumeshaona vile watu wamekupokea katika Seneti na wamekua na imani na upendo kwako. Usibwage morale ya watu wa Garisaa kama Seneta wao. Wapee heshima vile Sen. ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus