13 Apr 2021 in Senate:
Asante, Bi Spika wa Muda. Jambo la kwanza nataka kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa sababu ya uwezo wake alioufanya mpaka hivi leo tumefikia kilele cha Ripoti hii. Safari hii ilikuwa ni ya kutoka mbali. Tuliweza kupigania hizi pesa za
view
13 Apr 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
13 Apr 2021 in Senate:
ugatuzi ambazo zinakwenda katika serikali zetu za mashinani. Hatimaye zile kaunti ambazo zilikuwa zinapoteza ziliweza kupata ile pesa na kuongezwa tena zingine juu mojawapo ikiwa zile serikali za ugatuzi za jimbo letu la Pwani. Kulingana na Katiba ya Kenya Kipengele cha 96, kinapatia mamlaka ama majukumu ama uwezo Bunge la Seneti kuweza kutekeleza wajibu huu. Watapigania na kutetea kuona ya kwamba pesa zinazokwenda katika serikali za ugatuzi kote mashinani katika serikali 47 zimeweza kwenda bila uharibifu wa aina yeyote ama kupotea. Maseneta walio hapa walisimama kidete. Ningependa kuwashukuru sana kwa sababu ilikua hali ya vuta nikuvute, lakini mwishowe tulifaulu.
view
13 Apr 2021 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, hii Ripoti inasema kwamba Serikali isicheleweshe hizi pesa kwenda kwa Serikali za ugatuzi. Hizi pesa zinahitajika kupeleka madawa, maendeleo na vitu vingi ambavyo vinaweza kurahisisha maisha ya watu wa kaunti kuwa bora zaidi. Pesa hizi zina maana sana. Vile vile, ningependa kutoa onyo kwamba wote ambao wanahusika kuangalia hizi pesa wazitumie kwa usawa; zisitumiwe ovyo au kwa njia ya ufisadi. Hizi pesa ni muhimu kuleta miradi mbali mbali katika serikali za kaunti. Kupitia serikali za ugatuzi, barabara zinatengenezwa, hospitali zinapata dawa, na kina mama wanapata njia ya kwenda kwa shughuli zao mbali mbali. Hizo shughuli zote ...
view
24 Mar 2021 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Pia mimi naunga mkono Hoja hii kwamba tuangalie ratiba ya vikao vya Seneti. Tumeona kwamba janga la korona limetushika. Hakujawahi kutokea janga kama hili la korona katika ulimwengu kwa zaidi ya karne moja. Kwa hivyo, ni jambo ambalo lazima tulizingatie zaidi.
view
24 Mar 2021 in Senate:
Tumeona ya kwamba tumepoteza madaktari wa ngazi za juu kwa ugonjwa huu wa COVID-19 ambao bado tunawahijati katika nchi hii. Ukiangalia idadi ya wale waliofariki katika ulimwengu ni madaktari, wauguzi, na wanafanya kazi hospitalini. Hao ndio walioathirika sana na ugonjwa wa COVID-19.
view
24 Mar 2021 in Senate:
Bw. Spika, hatuwezi kukosea tukisema kwamba ugonjwa huu umeleta hasara katika Mabunge yetu mawili; Seneti na pia Bunge la Taifa. Ugonjwa huu umechukua wenzetu na kuwapeleka mbele za haki. Hii inamaanisha kwamba ugonjwa huu uko. Wakati mwingi utaona kuwa tunajaa na tunaketi karibu sana. Hii inapinga amri za Wizara ya Afya zinayosema watu waweke social distance.
view
24 Mar 2021 in Senate:
Jambo la pili ni kwamba kumekua na upungufu wa dawa zinazokuja. Hivi sasa, chanjo zilizofika ni kama milioni moja. Taifa hili lina watu millioni 48. Ukileta chanjo milioni moja, hii ni kumaanisha Wakenya 47 hawatapata chanjo. Kadri tunavyoendelea mbele ndio kupoteza watu wengi kupitia hili janga. Ni muhimu kisisitiza zaidi kwamba Serikali wagundue mbinu za kutafuta hizi chanjo ili zikuje na zisaidie Wakenya wetu.
view
24 Mar 2021 in Senate:
Bw. Spika, tunaelewa kwamba sasa kuna korona mpya kwa jina new COVID-19
view
24 Mar 2021 in Senate:
ambayo inachukua masaa 36 ukisha ambukizwa. Tunashukuru Mwenyezi Mungu kwa kumwokoa ndugu yetu Sen. Wako. Hii kwa sababu yeye alifahamu na alienda hospitali mapema, akapata hewa na aliweza kuokoa maisha yake. Lakini, ni wangapi ambao wanaweza kufanya hivyo? Ugonjwa wa COVID-19, na COVID-19 variant hatuzitatui vizuri sana.
view