24 Mar 2021 in Senate:
Jambo la mwisho ni kwamba mochari zetu zinaanza kuwa na uzito wa kuweka maiti. Hivi sasa, ushauri ni kuwa maiti zifukiwe mapema iwezenekanavyo. Tukiendelea kuzika mapema, tutakua kama ndugu zetu Waislamu ambao mtu akifakiri leo, anazikwa hiyo siku, kulingana na wakati aliofariki. Tungependa kuwaambia ndugu zetu Wakristo kwamba hakuna haja ya kuweka mwili ikiwa mtu amefariki kutokana na COVID-19 ama kuzingatia taratibu za sheria za Wizara ya Afya. Lazima Serikali ichukue mkondo wa mbele kuona kwamba imeweza kuleta dawa za kutosha.
view
24 Mar 2021 in Senate:
Ninaunga mkono Hoja hii.
view
24 Mar 2021 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda. Kwa niaba wa watu wa Kilfi, na kwa niamba yangu, ningependa kutoa rambirambi zangu za dhati kwa watu wa Tanzania. Watu wa Tanzania wamekumbwa na jonzi juu katika maisha yao. Kama tunavyojua, Rais John Pombe Magufuli alijulikana kwa vitendo. Kwa sababu hiyo, ni Rais aliyependwa na wengi. Alipendwa na watu kwa sababu ni mtu aliyekuwa anasimama na wanyonge na maskini kabisa wa Tanzania. Nakumbuka nikimwona akienda kwa fundraising ya kanisa. Yeye mwenyewe ndiye alikuwa anatembea na bakuli akiwaambia watu wachange ili kanisa lipate kujengwa. Ni jambo la kupendeza sana, na ni mfano wa kuiga. Alikuwa ...
view
24 Mar 2021 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, nikimaliza, tunakumbuka kuwa wakati alikuwa anasafiri kuzungumza, alienda kila mahali Tanzania. Alienda Zanzibar, Pemba, Unguja, Dodoma, na Mwanza. Kote alikoenda, watu walimpenda sana. Saa zile alikuwa anafanya mkutano, alikuwa anamwita mama ama mzee amwambie ni shida gani zipo katika eneo hilo. Mara The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
24 Mar 2021 in Senate:
tu yule mama au mzee alisema, alikuwa anachukua hatua papo hapo. Ni jambo ambalo hatujaona likitendeka na marais wote wa Afrika. Vile vile, kwa mambo ya kupigana na ufisadi, yeye alikuwa kipaumbele. Kama ulikuwa umefanya mambo ya ufisadi, (Dkt.) John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikuwa hana huruma. Alikuwa anakufuta saa iyo hiyo hata akiwa kwa barabara au kukuambia kwamba akirudi tena, kazi yako itakuwa imeisha. Huo ndio mwelekeo ambao tunataka hata Rais wetu afuate. Mambo ya ufisadi yamekithiri zaidi hapa Kenya. Ikiwa tutauiga mfano huo, hata sisi tutaweza kuendelea.
view
24 Mar 2021 in Senate:
Bi. Spika wa muda, tunataka kurejesha tena maombi yetu kwa watu wa Tanzani ili wawe na nguvu na kumtakia Rais Bi. Suluhu aweze kuongoza nchi hiyo kwa usawa na haki kama vile alivyofanya mtangulizi wake.
view
23 Mar 2021 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Mambo ya kisheria lazima yachukue mkondo wake na taratibu za kisheria kufuatwa. Katika mchakato huu, jambo kubwa sana ni kwamba hili ni jambo litakalokuwa sharia ambazo zitatumika katika siku za usoni kusaidia Wakenya. Ningependa kumpa kongole dada yetu, Sen. Agnes Kavindu Muthama, aliyekuja hapa. Yeye ni mama mkakamavu sana. Amedhihirisha wazi kwamba anaweza kuingia katika ulingo wa siasa, kumenyana na wanaume na kuwabwaga. Kongole sana dada yangu kwa kuja hapa Bunge la Seneti. Hili ni Bunge lenye uzoefu mkubwa katika taratibu zake za Bunge. Majadiliano hapa huwa makali na tunakosana lakini ...
view
24 Feb 2021 in Senate:
Shukrani,Bw. Spika. Nimesimama kuambatana na Kanuni ya Kudumu No.48(1), kuomba Kauli kutoka kwa Kamati ya Usalama wa Taifa, Ulinzi na Mahusiano ya Kimataifa kuhusu ukatili wa maofisa wa kituo cha polisi cha Bamba kilichomo eneo Bunge la Ganze. Kauli inahusu kupigwa kwa mfanyibiashara maarufu Mama Kadzo Karisa Kalu mbele ya wafanyikazi wake na mali yake kuharibiwa. Bw. Spika, katika Kauli hiyo, Kamati ya Usalama wa Ndani inapaswa kueleza: (1) Sababu za ukatili wa polisi wa Kituo cha Bamba katika eneo Bungle la Ganze, ambao ulisababisha kupigwa kwa mama Kadzo Karisa Kalu na kuharibiwa kwa mali yake. (2) Ni lini mama ...
view
24 Feb 2021 in Senate:
Asante Bi. Naibu Spika. Ni jambo la kusikitisha kuona mama anayeitwa Jacklyn Mugure akipoteza maisha yake kwa risasi. Mambo ya risasi au bastola The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
24 Feb 2021 in Senate:
kutolewa na askari mara moja, askari walio na furaha ya kupiga watu risasi, triggerhappy police officers, ni jambo ambalo linatendeka kila siku. Hivi majuzi, tafakari zetu hazijatulia, sehemu ya Eastleigh, mama alikua ameketi na watoto wake vizuri sebuleni katika nyumba yake iliyo floor ya tatu au ya nne. Lakini askari aliyekua anatembea chini alitoa bastola akapiga risasi juu kisha ikamuua mtoto wa miaka sita au saba aliyekua anaendea shule alipokua akicheza na ndugu zake katika
view