23 Feb 2021 in Senate:
Bi. Spika, amenipa habari hiyo lakini badala ya kusikiliza anaendelea kuongea. Sasa ni kama alikuwa anaingia tu katikati.
view
23 Feb 2021 in Senate:
Pole, Bw. Spika. Ni ulimi unateleza lakini si kumaanisha hivyo. Kumekuwa na kuingiliana kwingi sana kutoka kwa Sen. Pareno ambaye yuko hapa karibu nami.
view
23 Feb 2021 in Senate:
Pole, Bw. Spika. Ni ulimi unateleza lakini si kumaanisha hivyo. Kumekuwa na kuingiliana kwingi sana kutoka kwa Sen. Pareno ambaye yuko hapa karibu nami.
view
23 Feb 2021 in Senate:
Hoja iliyoletwa na Sen. Were ni sawa kabisa. Tunataka hatua kali zaidi ichukuliwe ili mchezo kama huu usiendelee katika Jamhuri ya Kenya.
view
23 Feb 2021 in Senate:
Hoja iliyoletwa na Sen. Were ni sawa kabisa. Tunataka hatua kali zaidi ichukuliwe ili mchezo kama huu usiendelee katika Jamhuri ya Kenya.
view
17 Feb 2021 in Senate:
Bw. Spika, singependelea kumuingilia katikati Sen. Olekina. Lakini, je ni sawa akiketi katika Bunge hili akiwa tupu ama ikiwa nguo alizovaa hazijakamilika kulingana na mila za Kimaasai? Ninaambiwa hapa na mama ambaye ni Mmaasai---
view
17 Feb 2021 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, protect me .
view
17 Feb 2021 in Senate:
Nauliza tu kama ni haki kwa yeye kuvaa nguo za Maasai nusu. Mgongo wake wote uko wazi ilhali wale Wamaasai ambao tunawaona kule nje huwa wanavaa wakijikinga kabisa. Je, hii ni heshima?
view
16 Feb 2021 in Senate:
Shukrani, Bi. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii. Najiunga pamoja na maseneta wenzangu kutoa rambi rambi zangu kwa familia ya Mzee Haji. Nina imani kubwa kwamba ndugu yangu, Noordin Haji, ataweza kuiweka familia pamoja sisi tukiiombea familia yao wakati huu wa majonzi ili waweze kupita janga hili la kumpoteza baba yao.
view
16 Feb 2021 in Senate:
Kule nyumbani kwetu kuna msemo kuwa mti mkubwa ukianguka, vifaranga vya ndege, hubabaika kwani havijui vitaenda wapi. Lakini nina imani kwamba familia ya mzee itakuwa pamoja wakati huu mgumu sasa na katika siku zijazo. Mimi na familia yangu tunatoa rambi rambi zetu kwa familia ya Mzee Haji ambaye alikuwa kama babangu. Vile, Mzee Haji alikuwa rafiki na mwandani wangu wa karibu Sana, yapo maneno mengi sana ambayo nilizumgumza na Mzee Haji kama mwandani wangu ambayo yalinipatia faida sana katika kujiimarisha katika Bunge hili la Seneti katika muhula uliopita na wa sasa.
view