Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1251 to 1260 of 2266.

  • 16 Feb 2021 in Senate: Mzee Haji alikuwa mtu wa msimamo kabisa hususan katika ugavi wa fedha zinazoiendea serikali zetu za ugatuzi. Wakati tulikuwa na mjadala kuhusu ugavi wa fedha mwaka jana, Mzee Haji aliniita kando na akaniambia, ‘Hivi ni vita na ikiwa kuna tashwishi zozote, wewe usiwache sababu iliyokuleta hapa; kutetea watu wa Kaunti ya Kilifi. Kufa nao na kuwa na msimamo nao wala usibanduke hata kidogo’ Maneno aliyonena Mzee Haji yalinipa nguvu sana. Ijapokuwa tulionekana kama watu wanaokosa kueleweka, ilikuwa ni kwa sababu ya msimamo tuliochukuwa. Ikiwa Mzee Haji anaweza kuchukua msimamo kama ule, itakuwaje sisi wengine kama vifaranga tusiweze kuchukua msimamo? Bi. ... view
  • 10 Feb 2021 in Senate: Asante sana, Bi. Naibu Spika. Kuna msemo uliosemwa na Wahenga zamani kwamba ukiona cha mwezako kimenyolewa, chako anza kutia maji. Jambo hili la kuvunjiwa nyumba na Wakenya kuitwa maskwota, yaani mahali ulipokaa kwa muda mrefu kuwa si kwako, ni jambo ambalo limetendeka sana hata upande wa Pwani. Ni kitu cha kusikitisha kwamba katika makabila yote 45 sasa, Wanubi ni watu ambao tunajua kwamba wanaishi katika sehemu za Kibera na Kibos. Ijapokuwa sio wengi, inajulikana kwamba ni Wakenya wanaoishi na heshima zao kama vile jamii zingine za Kenya zinavyoishi. Kitendo cha unyama kilichotendewa Wakenya wenzetu kilikuwa cha kuhuzunisha sana. Kilionyeshwa katika ... view
  • 10 Feb 2021 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 10 Feb 2021 in Senate: na kujionea. Waangalie ikiwa ni kweli wale watu wameishi pale kwa zaidi ya miaka 90. Ikiwa ni kweli, Shirika hilo liweze kurejesha makao yale kama yalivyokuwa hapo awali. Asante. view
  • 9 Feb 2021 in Senate: Asante sana, Bw. Spika. Kwanza najiunga nawe kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa vile tumeweza kurudi kutoka likizo ya Krismasi na mwaka mpya kwa buheri wa afya. Kulikuwa na mambo mengi hatari yaliyotendeka. Tulikuwa na mazishi na wengine kama sisi ambao Mwenyezi Mungu ametupa baraka na huruma ya kuweza kuona mwaka huu tukiwa na afya njema, twashukuru sana. Tunashukuru sana pia vile vile kwa makaribisho yako kwamba tumerudi na wote tukionekana kwamba tuko buheri wa afya. Bw. Spika, nataka kuunga mkono orodha ambayo imepeanwa ya Maseneta ambao watahusikana katika Kamati ya Bunge la Seneti ya kuweza kuendesha ratiba. Nafikiri The electronic version ... view
  • 9 Feb 2021 in Senate: hawa Maseneta wote ni watu ambao wamefaulu katika nyadhifa zao kwa muda wa miaka mine. Wameweza kudhibitisha umahiri wao katika kazi zao. Jambo la muhimu ni kwetu sisi sote kuzingatie mambo ya wananchi. Wananchi wa Kenya wako na imani sana na Bunge la Seneti kwa sababu ya hoja na miswada ambayo imeweza kuletwa mbele ya Seneti na kujadiliwa kwa kina. Maseneta ni viongozi ambao wanajiheshimu. Sisi si watu ambao tunaweza kupigana mandondi mbele ya wananchi. Tumejiwekea heshima na ninatumaini tutaendelea hivyo. Nataka niwapatie pia kongole Maseneta kwa kuweza kuweka kielelezo cha kwamba kama mnataka Bunge liheshimiwe, basi nyinyi muwe kama ... view
  • 9 Feb 2021 in Senate: mtafaruku, pengine watu wanaweza kuanza kupigana na maisha kupotea na pengine kujeruhiwa. Kwa hivyo, tunasema ya kwamba tuwe wa kwanza kama kielelezo. BBI si jambo mpya kwetu sisi kwa sababu tuliweza kufanyia Katiba yetu marekebisho na tukapata Katiba mpya mwaka wa 2010. Sasa ni mwaka wa 2021 ambapo tunaongea juu ya BBI. Baada ya miaka 11, mambo mengi sana yamegeuka na yanahitaji kugeuzwa na kuona ya kwamba nchi hii kutakuwa na amani, upendo na watu wakiishi kwa furaha baada ya kupiga kura. Bw. Spika, kusitokee jambo mbaya ambalo litafanya mimi nianze kuchukia huyu kwa sababu ni wa kabila la Kalenjin, ... view
  • 17 Dec 2020 in Senate: Mr. Speaker, Sir, it looks like we do not have 10H with us. Document 10E and 10G. If 10H can be availed to us, it will be much better. view
  • 17 Dec 2020 in Senate: Asante Bw. Spika. Kwa upande wa mashtaka, kuna stakabadhi zimetolewa hapa. Ingekuwa vizuri kama wanaweza kufafanua zaidi, kwa upande wa mashtaka. Je, yule aliyeshtakiwa Bw. Gavana, alipewa nafasi ya kusikizwa? Kama alipewa nafasi hiyo, je alipopeleka stakabadhi zake zilichukuliwa ama hazikuchukuliwa? view
  • 17 Dec 2020 in Senate: Kwa upande wa gavana, je alipewa nafasi hususan na Kaunti kuweza kupeleka hizo stakabadhi? Na hatimaye kupewa fursa nzuri sana ndani ya Bunge la Kaunti kujitetea kama hivi walivyojitetea hapa. Nafikiria pande zote mbili wangefafanua, ingekuwa vizuri kwetu sisi. Asante. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus