17 Dec 2020 in Senate:
Asante, Bi. Naibu Spika. Hakuna makosa yeyote kwa wakili Nyamu kutupatia sheria zilizowekwa hapo mbeleni ambazo zinaweza kuweka ushawishi mwema kwa Bunge letu la Seneti kufikia uamuzi wa haki. Sioni shida yeyote, Anaweza kuwapatia stakabadhi hizo akiendelea kuongea ili wazipitie. Sio lazima asome yote, lakini pale mahali ambapo alikuwa anataka kusema. Aende kwa ile aya ambayo anataka kusema aiseme, aiwache hivyo, apatie mwenzake aifafanue tu kidogo alafau awachie hapo. Hii ni kwa maana wakati mwengine tunaweza kupita mpaka. Asante, Bi. Naibu Spika.
view
16 Dec 2020 in Senate:
Thank you, Mr. Speaker, Sir. Normally when a lawyer is cross- examining and he asks you a question, just say ‘yes’ or ‘no.’ I believe the witness should do so instead of trying to be evasive from whatever angle. It does not save time. Could you be kind enough to guide the witness to reply with a ‘yes’ or ‘no’ answer? That is exactly what the witness should do. I do not think we need any extra issues.
view
16 Dec 2020 in Senate:
Bi, Naibu Spika, nilikua nimesimama hapo awali. Nilitaka kusema kwamba, ushahidi ambao--- Mshahidi mwenyewe ajiangalie katika yale yalioandikwa pale, ndio aweze kutuambia. Wakili amepitwa kidogo kwa sababu akijaribu kuuliza atashindwa ule wakati wa kuuliza maswali. Kwa hivyo, ni vizuri angojee mshahidi atoe ushahidi wake. Akimaliza, yeye atapata nafasi nzuri sana ya kumweleza kwamba amefanya makosa hapa na pale. Hio itakua sababu nzuri ya yeye kumsaidia mteja wake.
view
1 Dec 2020 in Senate:
Asante Bi. Naibu Spika. Kitu cha kwanza, ni jambo la kusikitisha yale ambayo yalifanyika huko Kapkatet ambapo mtu ambaye hakuwa amefariki alipelekwa pahali pa kuekwa maiti. Huu mgomo ambao unakuja Jumatatu wa madaktari ni kwa sababu madaktari wanafanya kazi katika hali ngumu, ilhali mishahara yao ni ndogo. Kuepukana na mgomo kama huu ni muhimu kwa sababu huu wakati wa COVID-19 ni wakati mgumu kwa wananchi. Ikiwa madaktari hawataweza kupatikana ama watajitenga kando, wale watu ambao watakua wanalindwa katika zile mashine watakua wapi? The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report ...
view
1 Dec 2020 in Senate:
Ni jambo la kutafakari sana kuona kwamba madaktari wetu wasiende kwa mgomo na waweze kuitwa haraka kuanzia sasa, kabla ya hiyo siku ili waweze kuafikiana kuweza kuepusha vifo vya Wakenya wengi wakati huu wa janga la COVID-19. Nataka kujua Kamati ya Seneti ya Afya itachukua hatua gani kuona kwamba hao madaktari ambao walifanya hicho kitendo wameweza kuadhibiwa ya kutosha ili iwe mfano mzuri kwa hospitali zingine zisifanye kitendo kama hiki. Asante.
view
1 Dec 2020 in Senate:
Nina hoja ya nidhamu, Bw. Spika wa Muda.
view
1 Dec 2020 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, kwa unyenyekevu, taadhima na imani kuu tulionayo juu yako, tunataka hii hoja ya nidhamu, kwa sababu tunaenda likizo, ndipo tukaongeza muda kidogo ili tueleze matumaini yetu katika Bunge letu la Seneti kama alivyosema Mratibu wa Walio Wengi Katika Seneti---
view
1 Dec 2020 in Senate:
Ninigependelea badala ya dakika mbili - kwa vile tumebaki wachache - tupate kama dakika saba ama nane kila mtu.
view
1 Dec 2020 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda. Nina imani na uhakika kwamba utakubaliana na mimi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view