Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1271 to 1280 of 2266.

  • 1 Dec 2020 in Senate: Bw. Spika wa Muda. Ningependa kukupa wewe kongole kwa sababu wewe ndiye Spika ambaye anatukuza lugha ya Kiswahili au lugha ya mama. Sisi Wapwani husema kwamba kuongea lugha ya kimombo kwa ufasaha haimaanishi unajua asili zaidi. Wewe ni mtu anayejua asili zaidi. Kwa hivyo, nakushukuru sana na pia kukupatia kongole kwa sababu hizi sheria zetu za hapa ndani ya Bunge la Seneti unazielewa na unaweza kuzitafsiri vilivyo kwa Kiswahili. Makosa yako ni kwa sababu hakuna binadamu aliye kamili. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from ... view
  • 1 Dec 2020 in Senate: Bw. Spika wa Muda, mimi naunga mkono kwa mara ya kwanza Mratibu wa Waliowengi ya kwamba watu waende likizo. Likizo ni kwa sababu ukifanya kazi kwa muda, binadamu yeyote lazima apate nafasi ya kupumzika, hususan wakati huu wa krismasi. Ni wakati wa kujumuika katika familia na watu wengi pia kuwa pamoja. Lakini katika ile hali ya kuwa pamoja tuweze kuzingatia haswa zaidi mambo ya Coronavirus disease (COVID-19). Tuangalie kwa sababu hili janga la COVID-19 limetokea katika Kenya ama ulimwengu mzima baada ya karibu karne nzima ya miaka 100. Bw. Spika wa Muda, hivi sasa Bunge la Seneti linaenda likizo na ... view
  • 1 Dec 2020 in Senate: Bw. Spika wa Muda, hakuna katiba iliyo kamili. Nataka kusema kinagaubaga kwamba hata BBI ikiwepo, sisi tutakao kuwa tunaendelea na hata tukishaenda--- Kwa vizazi vijavyo, hakuna katika ulimwengu mzima katika ambayo iko kamili. Kwa hivyo kama tunatafuta katiba ambayo iko asilimia mia moja, haitopatikana. Lakini kwa wakati huu ambao sisi ndio viongozi, ni sharti tufanye juhudi zozote ambazo mimi naunga mkono zaidi yaliyo ndani ya BBI. Yana uwezo ya kusaidia Wakenya kwa hivi sasa kuwaleta pamoja. Bw. Spika wa Muda, nikisema hivyo ni kwamba katika BBI tunaona hata katika maeneo Bunge mengine, hata Kauti ya Kilifi tunayo bahati ya kwamba ... view
  • 1 Dec 2020 in Senate: Bw. Spika wa Muda, pia nataka kuunga mkono Bunge la Seneti kwa kusimama kidete na ile “ Team Kenya ” ambayo ilifanya vilivyo usiku na mchana, kuwe na mvua ama jua. Hatawezekana ikiwa kama Wakenya watagawanyana. Tulisema kuwa haitawezekana. Kila kaunti ipate pesa yake na hatimaye tuliweza kupata. Kwa hivyo, yale mengine ambayo tunasema yataangaliwa pole pole halafu uhusiano mwema utaendelea na kila mtu atafaidika na pesa tutakazokuwa tunapigania ziwe zinaweza kwenda katika serikali zetu za mshinani. Bw. Spika wa Muda, la mwisho ni kwamba sisi katika hizi shamra shamra, tunasema kwamba Bunge la Seneti ni lazima pia liheshimiwe. Tunaona ... view
  • 24 Nov 2020 in Senate: Asante, Bw. Spika. KFS ni kiungo muhimu sana cha kuweza kusafirisha watu wanaoishi katika maeneo ya pande mbili za Kaunti za Kwale na Mombasa. Vile vile, ni kiungo kimoja pekee kinachoweza kusaidia watu wa biashara kupita na bidhaa zao. Bw. Spika, ni jambo la kusikitisha kuona kwamba kuna njama na mipangilio inafanywa kupitia Wizara ya Uchukuzi. Wana haja ya kutoa mamlaka yote ya KFS ili iwekwe pamoja na KPA, kiwe kiungo kimoja. KPA watakuwa na mamlaka ya kuifanya KFS badala ya kuwa na mamlaka yake tofauti, iwe kitu kimoja na iwe chini ya KPA. Sisi tunapinga mipango kama hii ambayo ... view
  • 10 Nov 2020 in Senate: I would like to inform him if he is ready to be informed. view
  • 5 Nov 2020 in Senate: Asante Bw. Spika. Ningependa kujiunga na wenzangu waliotangulia kuchangia Taarifa hii iliyoletwa na ndugu yangu mdogo, Sen. Anuar, Seneta mkakamavu wa Lamu. Katika sheria zetu za Kenya, hakuna mahali popote kumeandikwa ya kwamba Kizungu kitakuwa mbele ya Kiswahili. Tunavyoelewa, Kenya ina lugha mbili za kitaifa. Unaweza kuongea Kizungu au Kiswahili. Ni jambo la kusikitisha haswa ikiwa Katibu wa Kudumu anayeangalia mambo ya bahari anaweza kutamka maneno kama vile vijana wa Pwani hawajui Kizungu, na kwa hivyo hawawezi kupewa kazi kwenye meli au nyadhifa zozote zile. Hilo ni jambo la aibu. Bw. Spika, kwa mfano, mfanyikazi wako ndani ya nyumba haitaji ... view
  • 4 Nov 2020 in Senate: Asante sana, Bi. Naibu Spika. Kwanza, ninamshukuru sana ndugu yangu Sen. Khaniri kwa Ombi hili la kuhusu tamaduni zetu. Waswahili husema mwacha mila ni mtumwa. Hii ni kwa sababu huwezi kuwacha mila na desituri zako na kuheshimu za watu wengine. Haifai kujipiga kifua ukidhani wewe una uhuru wa kufuata tamaduni za watu wengine ilhali imeasi asili zako. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 4 Nov 2020 in Senate: Jambo la pili ni kuwasihi waheshimiwa Wabunge kukuza na kuhifadhi tamaduni zetu. Ikiwa nchi mzima inatuangalia sisi kama watu ambao tumeweza kufahamu mambo ya utamaduni, ni muhimu hili Bunge lichukue nafasi hiyo liwe kipau mbele kueleza mambo haya. Bi Naibu Spika, historia ya Bunge hili haijanukuliwa vizuri. Kwa mfano, hapa tuna kaburi la Mzee Jomo Kenyatta; mwanzilishi wa Taifa la Kenya. Katika mataifa mengine, makaburi ya waanzilishi wa mataifa yao, watalii huyazuru na kuelewa historia ya taifa hilo. Huko ndiko wao hufahamishwa vile kiongozi aliyekuwa wa kwanza kuanzisha nchi hii alikuwa anaishi namna gani, aliweza kuongoza nchi namna gani na ... view
  • 4 Nov 2020 in Senate: Asante, Bi. Naibu Spika. Sijui ni kwa sababu gani ile mic yangu leo inaonekana haifanyi kazi. Utanisamehe kwa hayo. Bi. Naibu Spika, pia mimi ningependa niunge mkono yote aliyosema Seneta wa Mombasa kuhusu ile kazi ambayo ni ya Kenya Maritime Authority, kazi ambayo iko katika eneo ya Pwani. Ijapokuwa ni shirika la kitaifa, kazi iliyo katika eneo la Pwani ni muhimu kuzingatia kuona kwamba ikiwa kutakuwa na mtu wa Pwani ambaye amefaulu ama ana haja na hiyo kazi na anazo qualifications, basi apewe hiyo nafasi. Mimi ningependa kuunga mkono hayo. Vile vile ningependa kuongezea kwamba kuna nafasi zingine nne ambazo ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus