Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1281 to 1290 of 2266.

  • 4 Nov 2020 in Senate: ambayo waliweza kumchukuwa mkurugenzi anayeitwa Francis Muraya. Wa pili ni mkurugenzi aliyechaguliwa katika Shirika la Kenya Maritime and view
  • 4 Nov 2020 in Senate: , anayeitwa James Njiru. Vile vile, kuna Katibu wa Kudumu katika State Department ambayo inahusika na mambo ya uvuvi na Blue Economy ambayo ni mambo ya samaki na bahari ambayo yanahusikana na ufuo wa Pwani. Nafasi hiyo, ikachaguliwa mtu anaitwa Michemi Ntiba. Bi. Naibu Spika, wa mwisho ni Katibu wa Kudumu ambaye tunaweza kusema anahusika na mambo ya Maritime Shipping ambaye anaitwa Nancy Garikithu. Bi. Naibu Spika, watu hawa wote niliowataja hapo watano, wanatoka katika eneo moja katika nchi yetu ya Kenya. Kazi zote tano zinahusikana na watu wa Pwani. Ni jambo la kukasirisha sana. Hivi leo, tumeona nafasi kama ... view
  • 4 Nov 2020 in Senate: Ndiyo. Ni sawa kwa Sen. Malalah kunieleza. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 4 Nov 2020 in Senate: Bi. Naibu Spika, mimi siruhusiwi kuongea tena? view
  • 4 Nov 2020 in Senate: Kwa hoja ya nidhamu, Bw. Spika wa Muda. view
  • 4 Nov 2020 in Senate: Asante, Bwana Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Ikiwa tuko kipaumbele kuongea habari ya mambo ya korona, ni lazima Bunge hili lenyewe liwezekutimiza hizo sheria za Korona. Nikasisitiza habari ya utamaduni tukasema kwamba Bunge lazima lichukue mkondo wa mbele kwa mambo ya utamaduni. Tukija upande wa Wabunge na Korona, unaweza kuona barakoa hii ambao nimeishika kwa mkono wangu wa kushoto ni ile ambao tulinunua nje kwa shilingi mia moja. Lakini kuna uzembe unaendelea hapa ndani ya Bunge. Barakoa hizi ni bandia. Hata barakoa zinazovaliwa na makarani wetu ni bandia. Ni vitambara ambavyo vimetengenezwa kule River Road na viweze kuzuia ... view
  • 4 Nov 2020 in Senate: sababu waheshimiwa Wabunge wanaweza kufa. Kwa mfano, Sen. (Dr.) Milgo, Sen. Farhiya, dadangu, Sen. Halake na wengine wengi wanaweza kufa tukichukulia ugonjwa huu kwa mzaha. Sisi sote tunaweza kufa kiholela. Tumendanywa kutumia hizi za Bunge ambazo ni bandia. Tumenunua kutoka nje na tumetumia kwa siku mzima, tunataka tupumue hewa safi. Tunataka kugeuza. Sasa hatuwezi kugeuza kwa sababu hizi barakoa tulizo nazo afadhali hizi kuliko zile ambazo hata hazina maana yeyoye na zimenunuliwa na Bunge letu. Bwana Spika wa Muda, asante sana kwa kuniruhusu kuongea kupitia hoja ya nidhamu. view
  • 3 Nov 2020 in Senate: Shukran Bi. Naibu Spika. Nataka kuchangia Taarifa iliyosomwa na Spika wetu kuhusiana na kesi iliyokua kortini. Jambo la kwanza ni kuwashukuru Maseneta ambao ni mawakili ambao waliweza kutuwakilisha katika kesi hii, hususan Sen. Orengo, Sen. Omogeni, Sen. Mutula Kilonzo Jnr., na mawakili wengine walioweza kuchangia. La muhimu katika hii ni kwamba tulipokuwa tukipeleka kesi hii Kortini, sote tulikua tumekubaliana kwamba kulikua na dhulma ambayo ilikua imefanywa na hatukupendelea katika zile sheria 24 ambazo zilipitishwa bila kuhusisha Seneti wala Spika wetu kuwa katika mahojiano kama hayo. Kipengele cha 110(3) katika Katiba yetu kiko wazi na kinasema kuwa kabla Bunge letu kukubaliana ... view
  • 3 Nov 2020 in Senate: Mswada ambao unaweza kupitishwa bila Seneti kuhusishwa. Ule uerevu waliokua wakifanya, Waswahili husema, “mwerevu hajinyoi.” Hata uwe mwerevu namna gani, huwezi kuchukua makasi ukajinyoa. Sheria kama hii ya kuzembea ama kutotii amri katika Katiba ndio sisi tunasema kwamba Mahakama imefanya jambo la muhimu kuweza kuurekebisha na kuweka sawa. Vile vile, nataka kuwapea kongole Majaji walioketi kusikiza kesi hii. Majaji hao wamefafanua kabisa na kueleza kila kitu kinaga ubaga kwamba, hamtachukua sheria kwenye mikono yenu na kufanya vile mnavyotaka. La mwisho ni kwamba, sisi tukiwa hapa Seneti, tunahitaji Wabunge wa Bunge la Kitaifa waweze kuelewa kwamba Seneti linahitaji kupewa heshima yake. ... view
  • 8 Oct 2020 in Senate: Asante, Bw. Spika. Ningependa kujiunga na wenzangu niseme Taarifa iliyoletwa na Seneta wa Mombasa, Sen. Faki, ni muhimu sana kwa uchumi wa taifa hili. Utaona ya kwamba wakati wowote Serikali ikifanya mipangilio ya kujenga barabara za pwani wanaangalia mabarabara ambayo inaenda maeneo ya utalii. Hawajali barabara zinazoenda sehemu ambazo watu wanaishi kwa wingi. Bw. Spika, ni aibu kubwa kwa Serikali kuona kwamba barabara ya Dongo-Kundu ambayo haijamaliza miaka miwili, tayari imeanza kuporomoka na kuwa na mashimo. Uporomokaji huu umetokana na kutokarabatiwa kwa hali ya ustadi wakati wa ujenzi. Maeneo ya Diani, South Coast na Mji wa Mombasa kumejaa watu wengi ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus