Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1291 to 1300 of 2266.

  • 8 Oct 2020 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 8 Oct 2020 in Senate: Tumeona ajali nyingi zikitokea katika barabara ya kutoka Mombasa kwenda Malindi. Barabara hiyo haijakarabatiwa kwa zaidi ya miaka kumi. Hivi majuzi wanakandarasi walikuja hadi Mtwapa na kuanza kubomoa pande zote mbili za barabara kwa minajili ya kukarabati. Hata hivyo, hakuna barabara ambayo wanajenga bali ni kumwaga mchanga na seruji. Kitendo hiki kinasababisha ajali nyingi wakati magari yanabishana na kujaribu kukwepa mashimo na vilinduko vya mchanga na seruji. Barabara kama hizi zikiwa zinatengenezwa ni lazima watoe taarifa kuu katika mabango kuonyesha ni nani anayezijenga, ikiwa ni mkopo ni kutoka wapi na itachukua muda gani kukamilisha ujenzi. Barabara ambazo hunganisha maeneo mbalimbali ... view
  • 7 Oct 2020 in Senate: Jambo la nidhamu, Bi. Naibu Spika. view
  • 7 Oct 2020 in Senate: Bi Naibu Spika, nimemskia dadangu akisema kwamba elimu katika shule za msingi ni bure. Mimi nashanga kama sisi wengine tunafanya makosa kwa kulipa. Naomba afafanue ni shule gani ambayo watoto wetu walioambiwa warudi katika darasa la nne, tano ama sita--- Ni wapi, ili tujue? view
  • 7 Oct 2020 in Senate: Asante, Bi Naibu Spika. Sijui kwa nini jina langu linatokea katika hii kompyuta yetu halafu linazimwa ama linaondoka kwenye mtandao. Lakini hayo ni majaalio ya wale wenye technolojia ya kompyuta. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 7 Oct 2020 in Senate: Kwanza, ninamshukuru sana huyu ndugu yangu, Seneta wa Nandi kwa sababu ijapokuwa umri wake ni mdogo lakini ni Seneta mshupavu. Ni Seneta kijana ambaye amekomaa kabisa. Matamshi ninayosema hapa siku zote huwa ni mambo ya kumsifu. Jambo la elimu ni muhimu sana. Kwanza lazima tujiulize maswali. Rais mwenyewe aliwauliza Wakenya--- view
  • 7 Oct 2020 in Senate: “Bi Miradi” ninamuona ameketi hapa mbele yangu, nikiwa ninaongea na yeye anaongea. Akili yangu kidogo inatafshika. view
  • 7 Oct 2020 in Senate: Ninaomba yeye aniondokee itakuwa vizuri kwa sababu ana mwendo mzuri na umbo lake liko hivyo hivyo. view
  • 7 Oct 2020 in Senate: Namuona kiongozi wangu, James Orengo anatabasamu kwa hali ya juu sana--- view
  • 7 Oct 2020 in Senate: Kwa sababu alikuwa karibu na yeye na alikuwa hamuangalii; alikuwa anaongea na Petronilla hapo. Bi Naibu Spika, ikiwa Rais mwenyewe wiki iloyopita alituambia tuweze kutafakari sisi kama Wakenya na akasema si lini shule zitafunguliwa bali ni kwa njia ipi. Jambo la kushangaza ni kwamba hata siku saba hazijapita kutokea Rais aongee msemo huo, tunamuona Waziri Magoha ametangaza kwamba watoto warudi shule. Hili ni jambo la kusikitisha kwa sababu hivi sasa Rais hajasema kwamba ugonjwa huu wa COVID-19 umeisha au katika Kenya si janga tena. Hatuwezi kucheza karata na maisha ya watoto wetu. This is very serious. Tutaanza kuona makaburi ya ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus