Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1301 to 1310 of 2266.

  • 7 Oct 2020 in Senate: katika hayo mashule ambayo watoto wetu watarudi na wapate madawati ya kisawa sawa, waweze kukaa na kuwe na social distancing? Ni elimu gani Serikali imeweza kuwafanyia hawa watoto wetu kuona ya kwamba mara tu wakirudi shule wameweza kuzingatia mambo ya kuweza kujitenganisha na kuweza kusoma wakiwa ndani ya darasa. view
  • 7 Oct 2020 in Senate: Bi Naibu Spika, kama ungenipatia dakika moja kumaliza--- view
  • 7 Oct 2020 in Senate: Kama ni amri yako unajua mimi siwezi kukupinga lakini nilikuwa nina mengi ya kuwaambia Wakenya. Asante, Bi Naibu Spika. view
  • 7 Oct 2020 in Senate: Bi Naibu Spika, nami pia naunga mkono Ripoti hii ya Kamati ya Afya. Ni jambo la kusikitisha na aibu kwa Wakenya ikizingaitiwa kuwa mama alipoteza maisha yake. Kabla ya mtu kufuzu kuwa daktari, yeye huapa kuokoa maisha. Hospitali hiyo haikupewa leseni kufanya vitu kama hivyo. Waliapa kuokoa maisha ya binadamu kwa kuwapa matibabu. Hawafai kuweka pesa mbele kiasi ya kwamba mgonjwa anayekwenda kupata matibabu anakaa kwa muda mrefu akiangaliwa tu. Hatimaye maisha yake yanakatika muda unavyozidi kwenda. Hospitali hiyo imekiuka kiapo cha kuokoa maisha wanachokula madaktari. Huu ni mwaka wa 2020. Kuna maswali tunayofaa kujiuliza sisi kama Wakenya. Je, ni ... view
  • 7 Oct 2020 in Senate: Huo ni ukweli. Ni jambo la kusikitisha kuongeza mishahara wa madaktari na kuwanyima wahudumu wa afya ilhali wao hufanya kazi pamoja. Vile vile, kuna wale wanaofagia na kusafisha wodi. Ni lazima wale wanaofanya kazi katika vituo vya afya wawe na vifaa wanavyohitaji. view
  • 1 Oct 2020 in Senate: Jambo la nidhamu, Bw. Spika wa Muda. view
  • 1 Oct 2020 in Senate: Bw. Spika wa Muda, je, ni haki kwa msomi kama Sen. (Dr.) Langat kukosa kuingia hapa kama umeketi bila kutoa heshima kuambatana na kanuni za Bunge hili. Anatakikana ainamishe shingo lake mbele yako ili kuonyesha heshima kwa Seneti na kwa wewe kama Spika wa kikao cha Bunge hili. Yeye amepita kiholela kama anayeenda Soko la Marikiti. Ni heshima gani hii? Tunataka utoe uamuzi kuhusu kitendo chake ambacho si cha heshima. view
  • 30 Sep 2020 in Senate: Asante Sana, Bw. Spika. Pia, mimi ningependa kujiunga na wenzangu, kuhusu swala hili la wale wanakandarasi ama wauzaji wa vyombo vidogo vidogo katika shule zetu. Bw. Spika, utaona ya kwamba malipo haya wanayopewa kutoka kwa Serikali ni duni sana ilhali wanakandarasi hawa hutia bidii yote wanayoweza kwa kile kidogo walichonacho kuweza kujifaa na pia kufanya biashara hii ya uuzaji wa bidhaa hizi kwa njia ngumu sana. Ni jambo la aibu kuona ya kwamba hivi leo baada ya hili janga la Korona kuweza kuliepuka - hata kama hatujaliepuka lote - ya kwamba, matokeo ya wakati huo mpaka The electronic version of ... view
  • 30 Sep 2020 in Senate: hivi sasa, Serikali haijachukua hatua mwafaka kuweza kulipa wanakandarasi ama hawa wauzaji wa vitu vidogo vidogo katika shule zetu. Wanaosoma katika shule hizo ni watoto wetu wala sio wa watu wengine ama kutoka nchi zingine. Hata kama kuna watoto wa kutoka nchi zingine, hao ni wanafunzi wanaotaka kukimu mitihani, ili waweze kuendelea. Ikiwa tabia kama hii itaendelea, na wanakandarasi hawa wakose kupeleka vifaa hivyo shuleni, basi shule hizo pia zitakuwa hazina uwezo wa kufundisha wanafunzi. Tunaweza kufahamu ya kwamba, kabla hujakuwa mwanakandarasi, kwanza kwa sababu unapeleka vitu vidogo vidogo, unaenda na kuweka nyumba na cheti cha kumiliki ardhi kama rehani ... view
  • 30 Sep 2020 in Senate: Asante sana, Bw. Spika. Nataka kuunga hii Petition ya huyu ndugu yangu, Sen. Mwaruma, Seneta wa Taita-Taveta kuhusikana na hili shamba la Msambweni ambalo liko katika Voi Constituency, Kaunti ya Taita-Taveta. Bw. Spika, shamba hili liko katika kijiji cha Mkamenyi ambacho kiko katika Kaunti ya Taita-Taveta. Historia ya shamba hili ni ya kusikitisha. Ijapokuwa kulikuwa na wenyeji pale, walichukuliwa kama wanyama na shamba hili likachukuliwa na kupewa mzungu kwa sababu zisizoeleweka, lakini iliepeanwa kama zawadi. Wenyeji wanaoishi katika hilo shamba sio wanyama. Bw. Spika, ni jambo la kusikitisha kuona kwamba si mara ya kwanza, ya pili na haitakuwa ya mwisho ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus