30 Sep 2020 in Senate:
Bw. Spika, sijui kama ni kwa sababu ya sintofahamu za Sen. Sakaja na Sen. Kinyua kutamka maneno kama hayo. Taarifa hii. ambayo imesomwa na Sen. Mwaruma kutoka Taita Taveta inahusikana na mkoa wa Pwani. Sehemu ambayo imetajwa ni Msambweni na Kamheni ambayo iko Taita Taveta. Aliyepewa shamba ni askari jeshi wa kizungu ambaye ametajwa hapa na Sen. Mwaruma. Kuna Ripoti ya Truth, Justice and Reconciliation Commission (TJRC) ambayo ilitaja watu ambao walipewa ardhi ya Pwani. Kama Sen. Kinyua hajui, chanzo cha Lake Kenyatta anakijua. Tuliuliza tinga tinga, tukapewa watu. Kama hiyo si zawadi, sijui kama kuna zawadi nyingine tena. Ni ...
view
30 Sep 2020 in Senate:
Bw. Spika, tunajua kuwa ni nia ya Serikali kuona kwamba kila Mkenya amepewa nafasi ya kuishi pahali pake. Watu wa Mswambweni ambao wameleta hii Petition hapa Seneti wasichukuliwe kana kwamba hao si Wakenya. Hawa ni Wakenya na wako na haki ya kuleta swala lolote ndani ya Bunge la Seneti. Ni matusi hadi saa hii kuwa wao walikuwa wanaketi ndani ya ardhi eka mia moja hamsini kuambiwa wachukue eka thelathini na tano. Kama kuna matusi ni mtu The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard ...
view
30 Sep 2020 in Senate:
kukuambia ulikuwa na ardhi eka mia moja na hamsini na leo unaambiwa uchukue eka thelathini na tano na uende zako. Kudharauliwa inafaa kukoma ama ifike mwisho. Hili swala la ardhi ni swala chungu sana na si swala la kuchukuliwa mzaha jinsi Sen. Sakaja anasema mwambie aseme ni nani na nani walifurushwa. Anafaa kujua kila siku mimi huenda police station kutoa Waghiriama ambao wameshikwa na kuwekwa ndani. Wengine hushikwa na kufungiwa katika police cell na wengine wanatupwa katika yard za askari. Askari wa Kilifi hawana kazi yoyote saa hii isipokuwa kungoja service ya
view
30 Sep 2020 in Senate:
waende wakafukuze watu katika mashamba yao. Wakiambiwa kuna wezi mahali fulani wanasema gari haina mafuta ya kuenda huko. Lakini wakiambiwa ni kuenda kutoa Waghiriama pale ndani na kuwaweka watu wengine, hiyo nafasi ya kuenda uko na petrol inapatikana. Mimi naunga mkono Sen. Mwaruma vile amesema. Kamati ambayo itapewa jukumu hili, the StandingCommittee on Lands, Environment and Natural Resources ambayo inaongozwa na Sen. Mwangi, lazima ishurutishe kwamba watu Hao wapewe ardhi yao yote ya eka mia moja na hamsini. Asante, Bw. Spika.
view
30 Sep 2020 in Senate:
Jambo la nidhamu, Bw. Spika.
view
30 Sep 2020 in Senate:
Bw. Spika, kanuni za Bunge hasituruhusu kusimama au kuingia hapa unapozungumza. Nimemuona ndugu yangu Sen. Linturi ambaye ni shemeji wangu kutoka Meru, akiingia ukiwa bado umesimama, akapita na kuketi. Amevunja moja ya kanuni za Bunge la Seneti. Ningeomba uchukue hatua mwafaka ya kumrekebisha Sen. Linturi ama aombe msamaha kwa kitendo chake hicho.
view
24 Sep 2020 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Kama kuna eneo ambalo limeonewa tokea Uhuru hadi leo, ni Pwani. Haki za watu wa Lamu zimezoroteshwa. Ninataka kumuunga mkono ndugu yangu mdogo Sen. Loitiptip kwa swala hili. Sisi tunajua watu wanaoishi Lamu ni Waamu na Wabajuni. Lakini ukienda Lamu, utaona mashamba yao yanamilikiwa na watu wengine. Watu hawa wana stakabadhi bandia walizopata kutoka kwa Wizara ya Ardhi. Bw. Spika, ninataka ndugu yangu Sen. Mwangi ambaye ni mkakamavu na Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi kuangalia kwa undani usimamizi wa LKBMU. Tunajua upeo wa baharini ni wa burudani. Lakini utaona upeo ulio katika ziwa la Kenyatta umetolewa stakabadhi ...
view
24 Sep 2020 in Senate:
Bw. Spika, shukrani. Swala hili linaweza kutatuliwa vizuri kama ile Ripoti ya Ukweli, Haki na Maridhiano itatolewa na kuwekwa wazi kwa wakenya wote. Tunasikia vuguvugu tu, lakini ikitolewa wazi kwa wananchi, nina hakika iko na majina, maeneo ambayo yanachukuliwa kupitia njia ya dhulma. Ninaongea nikijua historia ya Kenya, kwamba mashamba hususan ya Pwani yalichukuliwa kwa njia ya dhulma. Taarifa kama hii Seneta wa Lamu ameuliza ni muhimu kuona ardhi iliyochukuliwa kwa njia ambayo ni kinyume na sheria, kuonewa na kupokonywa, imerudishiwa wenyewe. Hadi leo, watu wanaenda kufukuzwa katika mashamba yao na kuambiwa kwamba, shamba limepeanwa. Shamanba limepeanwa kwa nani ilhali ...
view
24 Sep 2020 in Senate:
Tume ya Ukweli, Haki na Maridhiano iliandika Ripoti zamani, na hadi sasa Serikali bado haijaiweka wazi. Ripoti ya Tume hiyo inafaa kuwekwa parwanja ili kila mtu aisome na ajue ni nini iko ndani yake, na ni kwa sababu gani Serikali haitaki kuifichua.
view
24 Sep 2020 in Senate:
Hoja ya nidhamu, Bi. Spika wa Muda.
view