Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1321 to 1330 of 2266.

  • 23 Sep 2020 in Senate: Asante, Bw. Spika. Mimi ninataka kuenda sambamba na ile taarifa ya Sen. (Dr.) Mbito. Utalii ni muhimu sana kwa taifa hili. Vijana wengi katika vyuo vya utalii walipendelea sana kusomea utalii kwa sababu ilikua ni biashara kubwa na ilichangia pakubwa nafasi za kazi. Lakini hivi sasa ukiangalia, utaona ya kwamba wamepoteza nafasi hizo. Katika eneo la Pwani, utalii wote umekufa. Utapata watu wameketi katika mitaa kwa sababu hawana la kufanya. Wanaenda kwa mambo ya mjengo na mambo mengine ambayo si ya utalii. Ninaishtumu Serikali kwa sababu jambo lolote kwao linalohusu kuhusu eneo la Pwani ni bahari na starehe kubwa katika ... view
  • 23 Sep 2020 in Senate: Kuna Ronald Ngala Utalii College ambayo imemaliza karibu miaka saba bila kukamilika. Jambo la kusikitisha ni kwamba Serikali inajua hivyo. Ndugu yangu Najib Balala ambaye ni Waziri wa Utalii na Wanyama wa Pori anafahamu kwa sababu anaishi katika eneo hilo. Urithi atakaoacha ni kuhakikisha kwamba Ronald Ngala Utalii College imekamilika ili vijana wa maeneo ya pwani wasomee hapo ili wapate kazi. view
  • 23 Sep 2020 in Senate: Kuna hoteli za Wazungu kama kule Malindi. Maeneo ya utalii yamezoroteka. Watalii wanakuja lakini wengi wanakwenda katika nyumba za watu binafsi. Hiyo inafanya Serikali kukosa ushuru. Wale wanaohusika na utoaji wa kodi za utalii wanafaa kujua kuna mabwenyenye wanaoleta watalii kutoka ng’ambo na kusema ni wageni wao. Wakiwa huko, wanafanya safari zao kisirisiri na kutoka malipo kwa wenyeji wao bila kutoa ushuru ambao unasaidia Serikali kuendeleza mambo ya utalii. Nasisitiza kwamba wasimamizi wa mambo ya utalii wachunguze watu wanaofanya Serikali kutopata ushuru. view
  • 23 Sep 2020 in Senate: Utalii wa nyumbani ni wa maana sana. Ada inafaa kupunguzwa ili wananchi wa Kenya wenye mapato ya chini waweze kwenda kufurahia mandhari ya pwani na kila mahali ambapo watalii huzuru hapa nchini. view
  • 17 Sep 2020 in Senate: Asante, Bw. Spika. Ningependa kuunga mkono Taarifa hii. Kazi ya wanajeshi wa Taifa letu--- view
  • 17 Sep 2020 in Senate: Asante sana baba yangu kwa kunipatia wasia huo. Uliyoyasema ni kweli kabisa. Tangu utotoni tunajua kwamba wale ambao hubeba bunduki ni askari ili kutulinda sisi. Tukiona waliova nguo za kijani kibichi, tunajua ni wanajeshi wetu ambao hulinda mipaka yetu na kuhakikisha usalama wa nchi. Ninashukuru sana kwamba katika maeneo ambayo baba yangu, Sen. Haji, ameweza kutembea, ameona maswala kama hayo yakiendelea. Lakini hapa Kenya, ni mara ya kwanza kihistoria kuona wanajeshi wakihusika na mambo ya kuuza ng’ombe. Hata Wakenya wenyewe watashangaa sana wakiwaona wanajeshi wakiuza ng’ombe. Tabia kama hii tumeona hivi majuzi. Wale walio katika vyuo vya kijeshi wanapewa makazi ... view
  • 17 Sep 2020 in Senate: mnataka huu uuzaji wa ng’ombe na nyama ufanywe na wanajeshi?” Kama kulikuwa na majadiliano kama hayo, hatuyaoni wala kuambiwa. view
  • 17 Sep 2020 in Senate: Ninapinga zaidi. Asante. view
  • 16 Sep 2020 in Senate: Asante Bi. Naibu Spika. Pole nilikuwa naongea na Kiongozi wa Walio Wachache, Sen. Orengo. Najiunga na ndugu yangu Seneta Sakaja kwa kumsifu na kuwatakia faraja familia iliompoteza Papa shirandula. Tunajua alikuwa mcheshi Sana na watu wengi karibu Kenya nzima iliweza kumtambua. Ni mtu aliweza kuleta tabasamu na furaha wakati wa jioni watu wakipata burudani zao ama wakiwa wanastarehe nyumbani mwao na familia zao. Bi. Naibu Spika, tukisema hivo tusisahau viongozi wengine. Bi. Naibu Spika, kelele imezidi upande huu. view
  • 16 Sep 2020 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus