16 Sep 2020 in Senate:
Bi. Naibu Spika, upande wa pwani tungependa kuona wale wanaotambuliwa kama Mekatilili wa Menza, aliyepigania Uhuru wakati ule. Imekuwa utovu wa nidhani katika Serikali, kwamba hawawezi kutambuliwa baada ya kufariki miaka mingi iliyopita. Alikuwa mama wa kwanza katika upiganiaji wa Uhuru, aliyepiga Mzungu kofi na akafungwa. Alifungwa katika jela ya Kisii lakini kwa ujasiri wake alitoka na kutembea kwa miguu mpaka akarudi nyumbani, Kilifi. Watu kama hawa hatuwezi kuwasahau katika historia ya nchi yetu. Mama kama Mepoho alikuwa mpiganiaji mkubwa wa Uhuru. Mwaka jana, tulipoteza bibi ya aliyekuwa kiongozi wa Pwani wa kisheria wa hali ya juu sana; bibi wa ...
view
16 Sep 2020 in Senate:
Asante, Bi Spika wa Muda. Cha kwanza ni kuwa, kufunga hospitali, hususan maeneo ambayo yanaweza kusaidia akina mama na watoto, ni makosa kisheria.
view
16 Sep 2020 in Senate:
Pili, Gavana Oparanya kutoa amri ya kufunga hizi hospitali na kuwaambia wafanyakazi waende leave ya wiki mbili amekiuka sheria. Kulingana na sheria, hana mamlaka hata kidogo kutoa amri kama hiyo.
view
16 Sep 2020 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, tunamuuliza Gavana Oparanya, katika sheria zote za Kenya na Katiba, ni kipengele gani kinampa yeye uwezo wa kufunga kaunti ama kuamrisha kaunti zote 47 ndani ya Kenya zifunge?
view
16 Sep 2020 in Senate:
Ndugu yangu ni mwanasheria shupavu na alikuwa katika lile Bunge ambako Gavana Oparanya alikuwa ndani ya Serikali kama waziri. Gavana wangu pia alikuwa Waziri katika hiyo Serikali. Ninamwambia ndugu yangu asifuate sheria hiyo iliyotolewa na Gavana Oparanya kwa sababu haina msingi wa kisheria katika Kenya.
view
16 Sep 2020 in Senate:
Katibu wa Muungano wa Wafanyikazi nchini Kenya, Bw. Atwoli, husema kuwa tabia kama hiyo ni ‘ushenzi kabisa.’ Hiyo ni tabia yenye utovu wa nidhamu. Gov. Oparanya akae akijuwa kwamba amri hiyo aliyotoa Wakenya wanailaani zaidi. Kama ni Wakristo wanasema, “Ashindwe Shetani.” Ashindwe! Hii ni kwa sababu hata mbele ya Mwenyezi Mungu yeye amekosea. Mungu mwenyewe alisema: “Nyinyi mtaendelea kunisifu na wale walio na imani watapona wakienda hospitalini.” Hivi leo amepuuza amri hiyo na anajifanya yeye ndiye kila kitu katika kaunti. He is nothing! Hawezi kuendesha kaunti zote kenya. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. ...
view
16 Sep 2020 in Senate:
Yeye kama Mwenyekiti wa CoG abaki hapo; wakae wakizungumza wakinywa Kahawa, na hayo yamalizikie hapo. Mambo ya kusema kwamba anaweza kuingilia hata Bunge la Seneti kutuambia jinsi ya kugawa pesa---
view
16 Sep 2020 in Senate:
Ninasikitika sana kwa mtu kama yeye aliyekuwa kule ndani ya Ikulu. Sijui kama alikuwa ameshikwa na usingizi ama hakuwa kwenye mkutano ule, lakini tulikiona kile kiwiliwili chake pale ndani. Hivi leo anatoka pale baada ya kupewa Kshs50 billioni ambazo tulikuwa tumeziomba. Si yeye bali sisi tulikuwa tumeziomba kama Bunge la Seneti. Alitoka pale na kuleta sheria zake akisema kuwa kaunti zifungwe. Unafunga kaunti kama nani? Haitawezekana.
view
16 Sep 2020 in Senate:
Kukiwa na Gavana yeyote katika kaunti 47 nitakubaliana na Sen. Mutula Kilonzo Jnr., kwamba tumuite hapa atuambie na akicheza, basi atajua kazi ya Seneta ni gani. Tutamfurusha kutoka mamlaka.
view