Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1341 to 1350 of 2266.

  • 16 Sep 2020 in Senate: Bi. Spika wa Muda, Bunge la Seneti linafaa kusheshimiwa kwa sababu ndilo linapeleka pesa katika serikali za mashinani. Waswahili watakwambia huwezi kuketi na kunyelea sinia ambalo unakulia. Yeye anatukana Seneti sasa lakini wakati ule walitaka pesa waliomba wapewe Kshs310 billioni. Wakati huu sisi tumewapa Kshs360 billioni. Yeye sasa anatakikana kusifu Bunge hili kwa sababu--- view
  • 16 Sep 2020 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Mimi pia ninaunga mkono Taarifa iliyoletwa na Sen. Faki. Kenya Ports Authority (KPA) imekua tegemeo kubwa kwa watu wa Pwani lakini tukichukua Usimamizi wa Bandari na kuichanganya na Shirika la Reli na Shirika linalohusika na bomba la kusafirisha mafuta, ni ukiukaji wa sheria. Ni jambo la kusikitisha kwamba Rais wa Jamhuri ya Kenya anaendelea kugandamiza watu wa Pwani, hususan kiuchumi. Watu wametegemea sana Usimamizi wa Bandari. Ukienda Mombasa leo, utapata kwamba watu wengi ni hohehahe kama mayatima. Hukana uchumi wa aina yoyote unaongeza mapato kwa wananchi wa Mombasa unaoendelea. Si wafanyibiashara ... view
  • 16 Sep 2020 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda. Shirika la Reli limefilisika. Lilifilisishwa na Wakenya waliokuwa katika mamlaka wakati ule. Sijaona hata mtu mmoja akipelekwa mahakamani kuwa kulifilisisha shirika hilo. Leo utapata kuwa Shirika The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 16 Sep 2020 in Senate: la Bandari linachukuliwa na kuchanganywa na shiriki ambalo lina na madeni ambayo haliwezi kulipa hadi sasa hiv linazama. Je, tutafufua shirika la reli ikiwa tuliunganisha na shughuli za Bandari? Hivi sasa Standard Gauge Railway (SGR) imeleta umasikini ndai ya Pwani. Imefilisisha barabara yote kutoka Mombasa hadi Nairobi. Hakuna biashara inayoendelea kutoka Mombasa hadi Nairobi. Nikimalizia kabisa---- view
  • 15 Sep 2020 in Senate: Bw. Spika siku ambayo Sen. Malalah alishikwa na kutiwa ndani ya gari aina ya Subaru ya rangi ya kijani, nilikua kwa nyumba yake. Nilikua hapa jana katika hili Bunge la Seneti, nikamuona Sen. Malalah akilia hapa mbele ya Maseneta wenzangu. Leo hii tukiambiwa kwamba Sen. Malalah alikua analia machozi ya mamba, ilhali aliweza kueleza kinaga ubaga sababu ya yeye kulia na kwa sababu gani anataka kuliwa na mamba--- Kwa hivyo, ikiwa tutachukua swala la kwamba alijitia ndani ya Subaru mimi sikujua kuwa Sen. Malalah alikua anafanya mzaha. Je, ni sawa kwa Sen. M. Kajwang’ kusema kwamba Sen. Malalah anapenda kukaa ... view
  • 8 Sep 2020 in Senate: Asante, Bw. Spika. Nakubaliana na uamuzi uliofanya, lakini nilikua nataka kukuomba jambo moja. Ombi langu ni kuwa, Mwenyekiti wa StandingCommittee on Justice, Legal Affairs and Human Rights anafaa kuwa mmoja wa wenyekiti watakaokua katika mkutano na Standing Committee on National Security,Defence and Foreign Relations, wakati Inspector-General of Police atakuja hapa. Ombi la pili ni kuwa, mimi nilikua ndani ya hiyo nyumba--- The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 4 Aug 2020 in Senate: Asante, Bw. Spika. Ni jambo la kusikitisha kwamba tuko na kitengo ambacho kinahusika na urekebishaji wa hivi vidude au vipopolipo. view
  • 4 Aug 2020 in Senate: Vipopolipo. Bw. Spika, leo katika Bunge la Seneti mitambo yetu haifanyi kazi vilivyo. Ingekuwa heri kwetu ikiwa unaweza kutoa uamuzi ya kwamba hivi vilolopipo au vipopolipo pamoja na mitandao hii virekebishwe vifanye kazi mara moja. Waambie warekebishe mtambo huu. view
  • 4 Aug 2020 in Senate: On a point of order, Mr. Speaker, Sir. view
  • 4 Aug 2020 in Senate: Asante, Bw. Spika. Je, nikosa Seneta yeyote kuongea kuhusu matisho kwa Seneta mwenzake? Ni haki kwa Kiongozi wa walio wengi katika Seneti kuuliza swali kama hiyo? view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus