Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1371 to 1380 of 2266.

  • 16 Jun 2020 in Senate: Jambo la nidhamu, Bw. Spika. view
  • 16 Jun 2020 in Senate: Asante, Bw. Spika. Upande wangu wa kushoto yuko ndugu yangu, Sen. (Eng.) Mahamud, ambaye ninamheshimu sana. Kwa bahati nzuri au mbaya, sijui kama leo amekosea au amepotea nji. Sisi tunaona kwa heshima kuu Sen. (Eng.) Mahamud ameketi asipotakikana kuketi kila siku. Kama hakuna nafasi upande ule, hata wewe unaona kuwa upande huu hauna hata mmoja aliyechukua nafasi ya upande ule. Lakini upande ule una mmoja wao ambaye ni ndugu yangu, Sen. (Eng.) Mahamud. view
  • 16 Jun 2020 in Senate: Bw. Spika, ninakuomba arudi upande ule iwapo kutakuwa na nafasi au aende kule kwingine ambako kuna nafasi ya watu wote kukaa. Ni muhimu upande huu tuketi sisi ambao ni wapinzani. view
  • 16 Jun 2020 in Senate: Bw. Spika, kwanza naunga mkono hii Petition . Kuna maswali fulani ambayo lazima yaulizwe. Wizara ya Ardhi imezembea katika kazi yake. Kwa mara nyingine tena, maovu yamechipuka. Tunafahamu kwamba uchumi wa Kenya unategemea sana ardhi ama mashamba. Biashara zote zinazohusiana na mambo ya ardhi zimesimama. Watu wa kuuza na kununua nyumba na mashamba hawawezi kufanya chochote. view
  • 16 Jun 2020 in Senate: Hali ya uchumi na pesa kuzunguka katika uchumi wa Kenya vimefungiwa katika ofisi za ardhi. Vile vile, mawakili ambao wanafanya kazi zinazohusiana na Ofisi ya Ardhi, mimi nikiwa mmoja wao, wamefunga ofisi zao na biashara pia zimelala. Hii ni kwa sababu Ofisi ya Ardhi haifanyi kazi. Kazi zote za mawakili na wale wanaouza na kununua mashamba zimelala. Wengine wana shida na pengine wanatafuta namna ya kupata pesa za kwenda kutafuta matibabu nje ya nchi. Hali imekuwa ngumu. view
  • 16 Jun 2020 in Senate: Wanafaa kuanza kutumia mtandao wa kisasa. Hata hivyo, ofisi hizo zinafaa kufunguliwa ili uchumi wa nchi uweze kuendelea. view
  • 2 Jun 2020 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda. Kwanza, nataka kumshukuru sana ndugu yangu na jirani, Seneta wa Kaunti ya Lamu. Hii Taarifa ina umuhimu wake hususan katika nchi nzima. Miaka nenda miaka rudi, tunaona ya kwamba ni lazima kuwe na gharika ambayo itapoteza binadamu. Tumechoka kupoteza Wakenya kila mwaka kwa sababu ya gharika. Ni jambo la kusikitisha kuona nchi zingine hazina maji lakini ukulima wao ni bora. Nchi kama hizi ni Israeli na Misri ambazo ziko katika jangwa na maji ya mvua The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be ... view
  • 2 Jun 2020 in Senate: huwa ni kama baraka kutoka kwa Mungu. Wanajua vile wanavyoyatega na vile yanawapatia mazao. Lakini ukija Kenya, nchi iliyobarikiwa na Mwenyezi Mungu na mchanga wake ni ule ambao watu wanaweza kupanda na kuzoa mazao ambayo yatawaangalia katika maisha yao ya usoni. Mtihani huo Serikali yetu imeanguka. Bw. Spika wa Muda, yale mafuriko yanaweza kutengenezwa kwa njia ambayo tuko na mabwawa ambayo yanaweza kuyatega yale mafuriko, lakini tunawacha kutega haya maji na yanakuwa gharika. Gharika inafanya mito kufurika, kuharibu mimea na kupoteza maisha ya binadamu. Haya ni mambo ambayo tunaona na ni aibu. Kila mwaka tunajua kwamba, itakapofika mwezi wa pili, ... view
  • 2 Jun 2020 in Senate: Ni lazima Serikali iwajibike kwa upande wa kuangalia mambo ya mafuriko. Ufisadi upo katika maofisi ambayo yanatakikana kutengeneza dams. Inafaa waache kufikiria matumbo yao badala ya kutengeneza vipeo ambavyo vinaweza kuzuia maji kusiwe na mudslides, mafuriko, ama mito kuvunja viungo vyao. Hata madaraja yetu yote yameharibiwa na mafuriko. view
  • 2 Jun 2020 in Senate: Bw. Spika wa Muda, la mwisho ni kwamba, lazima Serikali yetu iwajibike kwa sababu Wakenya wamechoka kupoteza watoto, akina mama na familia zao kwa mambo ya mafuriko kila mwaka. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus