26 May 2020 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Kama kuna kitendo kilichofanywa na Serikali cha kuumiza husuan watu wa Pwani na uchumi wao ni miradi wa SGR. Hivi sasa, hakuna uchumi wa eneo la Pwani. Huo ndio ukweli wa mambo. Kabla ya mradi huu, Mombasa ilikuwa na biashara na nafasi ya kazi nyingi. Serikali ilianzisha mradi huu na ikawa na deni. Leo hii deni hili ni mzigo kwake. Serikali yenyewe inaona shida kuilipa. Tukiangalia hayo maagizo yaliyotolewa na Wizara ya Uchukuzi kwamba watu wasitumie malori na watumie SGR kusafirisha mizigo yao hayaungwi mkono na sheria yoyote ya Kenya. Kusema ...
view
26 May 2020 in Senate:
kukubiliana tukadhani jambo hili lingepata suluhisho ya kudumu. Ni unafiki kuona kwamba hakufuata makubaliano yetu. Wakati huu SGR inaendelea kubeba mizigo ikiwakandamiza watu wa Pwani. Jambo la mwisho ni upande wa uhalifu. Ikiwa mimi sina kazi, sipeleki lori, watoto wangu wamefukuzwa shule, wale mabarubaru ambao wako kwa nyumba watafanya kazi gani? Hapo ndipo chanzo cha uhalifu. Kaunti za Mombasa, Kilifi, Malindi, Kwale na Taita Taveta kuna visa vingi vya uhalifu. Hii ni kwa sababu vijana wadogo wamekosa kazi. Wazee wao wako nyumbani wakingojea chakula kutoka kwa Serikali, hususan wakati huu wa homa ya COVID-19. Serikali inajaribu kulisha watu, lakini watu ...
view
26 May 2020 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda. Ninakubaliana mia kwa mia kwamba kilimo ndio uti wa mgongo na pia ninawashukuru ndugu zangu, Sen. Khaniri na Sen. Cherargei, kwa kuleta Taarifa hii hapa. Itakuwa jambo la aibu kuona kwamba mwaka nenda mwaka rudi, nchi yetu inakumbwa na janga la njaa. Kila siku kila uchao, tukilala na tukiamka, tunaagiza chakula kutoka nje ilihali nchini yetu inajulikana kama nchi ya ukulima. Tunavyoelewa ni kwamba, ni kweli kabisa nchi yetu ni ya ukulima lakini Serikali lazima iwajibike kuona kwamba wanachukua mazao kutoka kwa wakulima na kuweka katika maghala. Vile vile, Serikali pia isaidie wakulima kwa njia ...
view
26 May 2020 in Senate:
Ingekuwa vyema iwapo wakulima wa nanasi, maembe na kadhalika, huko Magarini, wangepata msaada wa kutosha ili kujikimu na hata kusaidia watu wengine. La kusikitisha zaidi ni kwamba, katika kaunti za Kilifi na Tana River, tulibarikiwa na mradi wa Galana-Kulalu. Leo, ni aibu kwamba ufisadi uliingia katika mradi huo. Rais mwenyewe alipoanzisha Serikali, walikuwa na matumaini makuu kwamba Kenya haitakuwa na njaa tena. Angalia Galana-Kulalu iko wapi leo? Wameiua kwa sababu ya ufisadi. Mradi wa Galana-Kulalu ulichukua ekari kubwa sana; dunia mzima katika eneo la kaunti za Kilifi hadi Tana River. Hata hivyo, utaona kwamba---
view
26 May 2020 in Senate:
Asante Bi. Spika wa Muda. Kumalizia tu ni kwamba, lazima tukabiliane na ufisadi wa mazao, kama walivyosema Sen. Khaniri na Sen. Cherargei katika Taarifa yao. Huu ni wakati mgumu na tunapaswa kuona wakulima wamepata faida kutoka kwa mazao yao.
view
26 May 2020 in Senate:
Hoja ya nidhamu Bi. Spika wa Muda.
view
26 May 2020 in Senate:
Singependa kumwingilia dada yangu Sen. Kihika katika Mswada wake ambao ni muhimu sana. Lakini, nilikuwa naomba ungefanye uamuzi. Kuna Seneta wengi hivi sana, zaidi ya saba ambao wako katika ukumbi ule uko nje. Hapa ndani tukiangalia, kuna nafasi nyingi ambazo wanaweza kuja wakakaa hapa, kwa upande huu an upande ule. Je, ni haki ikiwa wale Seneta wataketi kule ilhali nafasi iko ndani ya Chumba cha Seneti? Badala ya kuenda na list, kama mtu amechelewa, hata kama nusu saa, badala ya wengine kuketi kule na nafasi ziko hapa ndani ya Chumba cha Seneti, ingekuwa bora The electronic version of the Senate ...
view
26 May 2020 in Senate:
ikiwa wewe ungeweza kutoa uamuzi na kusema kwamba wale waliochelewa wataketi kule na wale ambao wako ndani, wameshafika na wako kwenye ukumbi, waje waingie ndani ya Bunge la Seneti. Asante, Bi. Spika wa Muda. Kama unaweza kunifanyia uamuzi, ningeshukuru sana.
view
22 May 2020 in Senate:
Hoja ya nidhamu, Bw. Spika.
view