22 May 2020 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Umetuambia katika uamuzi wako ya kwamba tusitumie maneno ambayo yatakuwa na madharau ama yanaweza kuudhi mtu. Ninavyoelewa ni kwamba -
view
22 May 2020 in Senate:
Tafadhali, Sen. Murkomen, kama ni mimi naongea it is only fair
view
22 May 2020 in Senate:
Bw. Spika, taratibu ni kwamba, na tunavvyoelewa, Sen. Kang’ata ni seneta wa Muranga. Tukiambiwa ya kwamba Sen. Kang’ata ni mfanyikazi ama mtumishi wa State House, hiyo hatuelewi. Kama ni hivyo, basi, hafai kuketi hapa. Kama anaketi State House amekuja kufanya nini ndani ya Bunge la Seneti na alichaguliwa na watu wa Murang’a? Ni sawa sawa ikiwa ndugu yangu ambaye ni rafiki yangu, Sen. Cherargei, kutumia lugha kama hiyo?
view
22 May 2020 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Mimi nataka kuunga mkono kwa kusema---
view
22 May 2020 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Sen. (Prof.) Kindiki ni rafiki, ndugu na shemeji yangu. Yeye amesoma vitabu mpaka akafika kiwango cha Profesa. Lakini kwa upande wa siasa, nafikiria alinoga. Lakini hayo yakijiri, mimi nataka kusema kwamba kuna mwanafalsafa mmoja aliyeishi zamani na alikua msomi, Niccolò Machiavelli. Mimi nmekua nikisema kila siku kwamba ikiwa wewe umechaguliwa au umeandikwa kazi, usiwe mwerevu kuliko bosi wako. Machiavelli alisema hayo katika mambo ya utawala na madaraka. Dhana hii inajulikana kama Principles of Power. Unaweza kuwa umesoma sana kama Sen. (Prof.) Kindiki na pengine bosi wake hakufika kiwango cha elimu kama hiyo, lakini si sababu ya kutumia ...
view
22 May 2020 in Senate:
Nampa wasia ndugu yangu kwa imani kuu. Yeye afunge huu usia wangu kwenye vidole vyake na autunze kama mboni za macho yake. Ukiangalia mbele, kama ni siasa, ni lazima ufuate mkondo wa maji. Tunaona mafuriko hapa Kenya. Yale maji yanavyoteremka yanabeba kila kitu, hata miti. Wewe sasa umejipata katika panda hiyo.
view
22 May 2020 in Senate:
Hivi sasa, utazama, lakini kuvunjika kwa mwiko sio mwisho wa kupika. Sisi kwa upande wa Muungano wa National Super Alliance (NASA) hatukukuleta hapa na hayo The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
22 May 2020 in Senate:
makosa. Makosa hayo yameletwa hapa mbele na Chama chako. Ni jukumu lako sasa kuchukua hii adhabu ambayo utapewa sasa, lakini ukumbuke kuna leo na kesho. Twakuombea kila la heri. Sina budi bali kuunga mkono Hoja hii.
view
22 May 2020 in Senate:
Bw. Spika, jambo la nidhamu, tafadhali.
view
22 May 2020 in Senate:
Bw. Spika, kwa heshima na taadhima kuu ya Seneti, nauliza tu iwapo tunaweza kutafakari kwamba tuko katika Mwezi wa Ramadhan. Tuko na dada na ndugu zetu wa Kiislamu, na hata Sen. Haji ambaye ni baba yangu. Ikiwezekena, pengine tungefupisha ama tungesema huyu awe wa mwisho. Tukifanya hivyo, watapata nafasi ya kwenda Msikitini kuomba halafu waende wachukue futari wafungue mwadhini. Ninakusihi sana tupunguze muda wa kuongea.
view