Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1401 to 1410 of 2266.

  • 22 May 2020 in Senate: Asante, Bw. Spika. view
  • 22 May 2020 in Senate: Bw. Spika, jambo la nidhamu. view
  • 22 May 2020 in Senate: Bw. Spika, kwa heshima, najua Sen. Kinyua anaongea na singependa kumwingilia. Hata hivyo, amesema hapa kwamba tunampaka Sen. (Prof.) Kindiki mafuta kwa mgongo wa chupa. Ni kwamba ati tunayoongea hapa, sisi tunandanganya. Tukimtia moyo, tunamdanganya. Kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa ni kumdanganya mtu lakini sio vile anavyosema. view
  • 19 May 2020 in Senate: Shukrani, Bw. Spika. Kwanza, ningependa kukupa kongole kwa uamuzi wako ambao wazungu wanauita Solomonic wisdom juu ya vile tunaweza kufanya kazi wakati huu mgumu katika Bunge la Seneti. Madhumuni ya Kanuni za Bunge la Seneti ni kusaidia utaratibu wa kuendesha kazi ama majadiliano katika Bunge na vile Maseneta wanaweza kupiga kura kuambatana na mfumo wa delegations. Wakati huu ni mgumu sana katika historia ya nchi yetu na ulimwengu mzima kwa jumla. Tunaambiwa ugonjwa kama huu ulitokea zamani kabla sisi kuzaliwa. Hivi sasa, hili janga la COVID-19 ni janga ambalo hakuna mtu yeyote aliyelitarajia kubuika. Kukabiliana na huu ugonjwa una taratibu ... view
  • 19 May 2020 in Senate: Bw. Spika, ni jambo njema sisi kama Maseneta kuona kuwa kuna udhaifu jinsi tunavyopiga kura hapa. Ni vizuri umefafanua kwa uwazi kabisa jinsi ya kushughulikia kazi hapa Bungeni. Kanuni za Bunge la Seneti zina umuhimu kuona jinsi tunaweza kujipanga kutumia teknolojia kufanya kazi wakati huu wa COVID-19. Kanuni za Bunge la Seneti zinafaa kugeuzwa ili kuambatana na wakati mgumu tulio nao sasa na siku za mbeleni. view
  • 19 May 2020 in Senate: Asante, Bi Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Jambo la kwanza nampatia kongole Seneta shupavu na mkongwe wa kisheria na aliyekuwa mwenyekiti wangu katika muungano wetu wa wanasheria katika Kenya. Ndugu yangu anawakilisha eneo la huku Nyamira, Sen. Omogeni. Nilikuwa najiuliza kama ana jina la kizungu. Tulikuwa tunajadiliana hapa na dada yangu Sen. (Dr.) Musuruve na tukaona kwamba Sen. Omogeni hana jina la kizungu. Yeye anaitwa Sen. Okong’o Omogeni. Ninamshukuru sana kwa kukubali kuchukua kesi hii na kuifanya yeye bila malipo kutoka kwa PSC au kwetu sisi Maseneta kuchanga kwa minajili ya kutaka kumlipa yeye kama wakili. Aliweza kujitolea ... view
  • 19 May 2020 in Senate: La mwisho ni kuwa kuna Kamati ya Sheria, na karibu Maseneta wote katika hiyo Kamati ni wanasheria. Kwa hivyo, tuliwapa jukumu la kufuatilia kesi hii. Wengine wetu tulipokua pamoja tulijukumika na hatimaye tumepata mazao. Ni muhimu kuangalia haya mazao na kujua mwelekeo wetu utakua vipi kuanzia sasa mpaka siku za usoni. view
  • 12 May 2020 in Senate: She is here. view
  • 12 May 2020 in Senate: Asante, Bw. Naibu Wa Spika. Pia nawapa kongole wale ambao wameleta Ombi hili kutoka Kaunti ya Machakos. Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba haki za wafanyikazi zinakandamizwa sana katika serikali za kaunti. Nilifanya kazi katika korti ya kuangalila masilahi ya wafanyikazi hapa Kenya, mfanyikazi aliye chini haheshimiwi. Ni muhimu kila mtu humu nchini aheshimiwe katika utenda kazi wake. Lazima kila mikono miwili inayofanya kazi iregeshewe asante kulingana na haki, mshahara na kazi iliyotendwa. Katika hili Ombi, tunaona kwamba hawa walifanya kazi na hawakusema kwamba wanataka kuondoka, wala hatujui ni kwa sababu gani waliachishwa hiyo kazi. view
  • 12 May 2020 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus