14 Aug 2024 in Senate:
Maseneta, ni lazima tuweze kuamua ikiwa tunataka kwenda ile njia ya kamati au Seneti nzima ambapo Maseneta wote wanachangia katika Hoja hii iliyo mbele yetu. Najua Bunge la Seneti linajulikana kwamba lipo na Maseneta majabali, maseneta ambao wanaweza kuketi wakasikiza kesi na kukata kisawasawa. Sintofahamu ni kwamba pengine kukatokea cheche za maneno kutoka nje na kunakuwa na lawama tofauti tofauti kulinganishana na Maseneta wetu. Hizo huwa ni cheche tu. Tunaelewa kwamba cheche zingine ni kama maji moto, haiwezi kuchoma nyumba. Kwa hivyo, hawawezi kutuambia maneno yanayowezafanya tukose mwelekeo na pengine tusikate kesi kulingana na zile stakabadhi zilizowekwa hapa mbele; stakabadhi ...
view
25 Jul 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika, Seneta Osotsi ni rafiki na ndugu yangu na tunasikizana sana. Hoja yangu ya nidhamu ni kwamba, ifikapo mambo na sheria za Bunge, hawezi kumtaja mtu ambaye hakuitwa na Bunge ama, hakujakuwa na taarifa fulani kwamba aje na hakuja, halafu yeye anamtaja kwa njia ambayo si ya kisawasawa. Mimi nauliza kama ni haki kumtaja mtu kabla hajaitwa katika Bunge kwa njia mbaya na hajapata nafasi ya kujitetea?
view
24 Jul 2024 in Senate:
Thank you, Mr. Speaker, Sir. First and foremost, I would like to react by saying that the amendments that we have decided to put in place in this Motion are viable and can be handled. As regards the positions of the principal secretaries, what we are saying is that the Committee on Justice, Legal Affairs and Human Rights has done these amendments, which we believe will go a long way to help the vision of what the Senator would wish to achieve. Mr. Speaker, Sir, moving on to further amendments that have been of equal opportunity to all Kenyans, we ...
view
24 Jul 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda. Kwanza, ningependa kumpatia kongole ndugu yetu, Sen. Abass, kwa kutengeneza sheria ambayo ni ya kuzima moto na kuokoa watu wakati wa janga la moto. Sheria hii inaleta mwelekeo mpya. Tumekuwa kwa muda mrefu na nafasi ambazo hazingeweza kukamilika kutengenezwa kwa sheria ambayo itahusikana sana na uzimaji wa moto. Kama tunavyoelewa, kazi ya kuzima moto hivi sasa inafanywa na magavana wa kaunti. Lakini kuna kasoro, ikiwa nitakosoa kidogo, upande wa magavana wetu wanaohusika na kuangalia jukumu hili muhimu sana. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this ...
view
24 Jul 2024 in Senate:
Magari ambayo yameletwa katika kaunti zetu ili kutumika kwenye kazi ya kuzima moto yanaonekana yalinunuliwa kitambo na kupakwa rangi kuonekana mapya. Haya magari yaliletwa na kupakwa rangi kwa ofisi za kaunti. Hakuna hata moja iliyojengewa mahali pazuri isipokuwa Mombasa ambapo wako na stesheni ya magari ya kuzima moto pamoja na staff wenye taaluma ya kupigana na moto. Wamewekwa pale ili waweze kutambuliwa mahali wanaweza kupatikana kwa kazi ambazo wanafanya. Bw. Spika wa Muda, mara nyingi tunaona - kwa mfano katika kaunti kama yangu, Kilifi - kwamba wale wanaofanya kazi ya kuzima moto lazima wawe na training. Sio training tu, lazima ...
view
24 Jul 2024 in Senate:
Magari haya huwa yamenunuliwa mamilioni ya pesa. Lakini, utapata gari limekuja mpaka pale bahari, wakijaribu kufungua, gari lenyewe halifanyi kazi na halina nguvu ya kutoa maji ya kuzima ule moto. Kwa hivyo, jambo kama hili sio la kuchekesha kwa sababu itakuwa hasara. Mimi nilipata hasara kwa kuchomekewa na nyumba. Lakini, nashukuru Mwenyezi Mungu kwani hakuna mtu aliumia. La mwisho, magari haya pia ni lazima yaangaliwe. Mara nyingi utapata katika kaunti zetu, magari ya watu kwenda kutembea au kufanya kazi zao mbalimbali za kaunti, yanapatikana. Lakini, lazima kuwe na sheria mwafaka ambayo ndugu yangu, Sen. Abass, anaweza kuangalia. Magari haya yakitengenezwa, ...
view
23 Jul 2024 in Senate:
Thank you, Mr. Speaker, Sir. I concur and second this Motion.
view
3 Jul 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Kwanza naunga mkono Hoja hii. Naunga mkono Hoja hii kwa sababu imekuja wakati unaofaa. Leo nasimama hapa Seneti nikiwa na majonzi mengi sana kama Bunge la Seneti kwa sababu kufikia sasa, Kenya imepoteza maisha ya watu 39. Vile vile, ukiangalia katika hospitali zetu zote Kenya, na sekta mbali mbali kuanzia baharini hadi Lake Victoria, ukumbi wa magharibi hadi mashariki, Kenya nzima, kuna watu waliolazwa huko sasa yamkini 361 wakipata matibabu. Wengine wamekatwa miguu, mikono, wengine wamefanyiwa operesheni za tumbo na vichwa. Hivi sasa wako na majanga ya maumivu wakiwa wamelala katika hizo hospitali. Ni jambo la kusikitisha ...
view
3 Jul 2024 in Senate:
lakini utozaji wa ushuru ukipita kiwango fulani, ama mambo yasiyofaa kutozwa ushuru yakiwekwa hapo, lazima watu waandamane ili kupata haki yao. Tunaona kabisa kwamba huu Mswada wa Fedha ulileta mushkin mkubwa nchini Kenya. Sisi hatuwezi kuwalaumu vijana wa Gen. Z kwa sababu walipokuja walisema Mswada huu unakandamiza kila mwananchi. Haukandamizi tajiri pekee, bali kila mtu nchini. Bw. Spika, sisi kama viongozi tunasema ya kwamba ni lazima tuwe na nidhamu. Hii ni kwa sababu tunaona wananchi wanaendelea kuishi maisha yasiyo mema. Maisha yamekuwa ghali na kila kitu katika nchi ya Kenya akipatikani Kumezuka majivuno na watu wanaojivunia sana ni wale ambao ...
view
3 Jul 2024 in Senate:
gari lake. Tendo hili lilifanyika kwa sababu ya makosa yake ya kuandama. Watu hawa wote, tunasema wawachiliwe mara moja.
view