3 Jul 2024 in Senate:
Mhe. Rais amewaajiri watu ambao wako na rekodi za ufisadi katika Serikali yake. Kuna watu wamefanya vitendo vya uhalifu ambavyo havifai kulingana na sheria za Kenya. Mhe. Rais, ikiwa hao watu wako katika Serikali yako, afadhali uwaachishe kazi mara moja. Jambo lingine ni kwamba Mswada wa Independent Electoral and Boundaries Commission (IEBC), hivi sasa uko kwenye mikono ya Mhe. Rais. Ni vizuri aupige sahihi ili kuondoa vuguvugu la kwamba hataki ama hawezi kupiga sahihi au kuna tashwishi yoyote. Hivi sasa, wananchi wanataka huo Mswada wa IEBC uwekwe sahihi na uwe sheria mara moja, ili mambo ya Kenya yaweze kuendelea na ...
view
3 Jul 2024 in Senate:
, irejeshwe mara moja ili watoto waweze kuenda shule wakijua watapata chakula. Jambo la mwisho na muhimu zaidi ni kwamba sisi kama Wabunge wa Seneti, na nakubaliana na alivyosema Kiongozi wa Waliowengi jinsi watu wanavyosema kwamba mishahara inaongezwa, mimi ninasema ya kwamba sitaki mshahara wangu uongezwe. Sitaki. Nimekataa. Bw. Spika, ninajua ndugu zangu Maseneta wako hapa na tunashida za pesa ndio. Lakini nina hakika watakubaliana na mimi ya kwamba sio wakati mzuri sasa sisi kuongezwa mishahara. Haifai na hatuitaki. Tumekataa.
view
3 Jul 2024 in Senate:
Ndugu yangu, Sen. (Dr.) Khalwale, utakubaliana na mimi ya kwamba umeshakula chumvi ya kutosha. Mshahara hivi sasa ukae kando na wapee wale ambao hawajiwezi ili waweze kuendelea na maisha yao kisawasawa. Ama ile pesa ya mishahara, ipelekwa kwa hao ambao walipata majeruhi, wale ambao wamefariki na walio na shida. Ziende uko ili tuweze kuwasaidia. Bw. Spika, hii Hoja iko na maana sana. Sisi tunajua tuna uwiano. Tunajua sote ni Wakenya na Kenya ikiharibika, itakuwa ni nchi yetu imeharibika. Hatuna nchi nyingine ya kuenda isipokuwa kubaki hapa ndani ya nchi ya Kenya. Kwa hivyo, tunatakiana kila la heri kuona ya kwamba ...
view
26 Jun 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Tunaelewa kwamba jana kulikuwa na maandamano ya amani. Vile vile, tunaelewa kwamba katika maandamano hayo, askari wetu walifyatua risasi na kuwaaua wale waliokuwa wakifanya maandamano. Waliokufa ni watoto wetu, Wakenya. Ni vyema ikiwa Bunge hili la Seneti litachukuwa dakika moja au mbili kuomboleza kwa ajili ya wale watoto waliouwawa. Ningependa tuchukuwe nafasi hii kabla ya kuendelea na taratibu za Bunge ya vitu ambavyo tunatakikana kufanya, tuwakumbuke marehemu wakenya wenzetu ambao wamelala katika mortuary na familia zao zinahuzunika kwa kuwapoteza wapendwa wao. Asante.
view
26 Jun 2024 in Senate:
Bw. Spika, tukiwa katika mkutano wa SBC, nafikiri tulikubaliana kwamba ajenda tutakayo shughulikia ni Hoja ya kuahirisha kikao hiki ili tuweze kupatiana nafasi---
view
26 Jun 2024 in Senate:
Ikiwa tutaanza kushughulikia mambo mengine, tutaharibu muda wa huu mjadala.
view
26 Jun 2024 in Senate:
Tafadhali, Bw. Spika, nakuomba. Ikiwa inawezekana, tushughulikie jambo moja pekee ambalo tulikuja hapa kujadili
view
26 Jun 2024 in Senate:
Bw. Spika, nakubaliana nawe jinsi ulivyosema. Hata hivyo, ingekuwa bora tukianza na kile tulichokubaliana kabla ya kushughulikia Hoja nyingine. Hiyo itakuwa sawa kabisa.
view
26 Jun 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Kwanza, nasimama kuunga mkono Hoja hii ya kuahirisha vikao vya Bunge letu la Seneti kwa moyo mzito sana. Tunasimama hivi leo hapa tukiwa tumewapoteza ndugu zetu na watoto wetu. Hapa sio pahali pengine katika Kenya ama mbali na maeneo ya Bunge, lakini tumeweza kupoteza watoto wetu ndani ya maeneo ya Bunge ambapo walipigwa risasi. Bw. Spika, ni jambo la kusikitisha sana. Nikisimama hapa, ninajua kuna akina mama wengi sana katika Kenya hivi leo ama ndugu zetu wa kike na kiume na Wakenya kwa jumla, wamepoteza ndugu zao na jamii zao kote katika Kenya. Hata hivyo hatujajua hesabu ...
view