26 Jun 2024 in Senate:
Tunaelewa ya kwamba sisi kama Wabunge tuko hapa na haya ni maeneo ambayo yanaingia watu wa nje kwa ruhusa ya inayotolewa hapa. Tuliona maroli ya polisi ambayo yalikuwa yakiwazuia watu ili wasiweze kuingia. Ilikuwaje waliruhusiwa na mlango ukafunguliwa na wakaingia ndani? Hilo ni jambo moja ambalo tunaweza kusema ya kwamba tunataka uchunguzi ufanywe ndio sababu tunatoa nafasi hii. Yale yanayosemwa ya kwamba Bunge liliweza kuingiliwa na likaharibiwa na maeneo mengine kama maeneo ya kula chakula na maeneo ambayo walikuja wakaangusha hizi bendera zetu. Hata hivyo hao walikuwa Wakenya lakini tunasema ya kwamba, katika maeneo hayo ambayo tumesema, kama ni mambo ...
view
26 Jun 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Pia, ndugu yangu ana hoja nzuri na atapewa wakati wake wa kujieleza. Ninakubaliana tuahirishe hivi vikao mpaka tukutane tena Julai 16. Ninaunga mkono hii Hoja.
view
26 Jun 2024 in Senate:
On a point of order, Mr. Speaker, Sir.
view
26 Jun 2024 in Senate:
Every time we have something like this, we have to see them on the screen. We cannot do this. This is dangerous.
view
26 Jun 2024 in Senate:
On a point of order, Mr. Speaker, Sir.
view
29 May 2024 in Senate:
Asante Bw. Naibu Spika. Cha kwanza, naunga mkono Mswada huu ambao unahusu mageuzi ya Tume huru ya kusimamia kura na mipaka katika Kenya. Cha muhimu ni kuwa Mswada huu ulitengenezwa na Kamati ya NADCO na hatimaye, ikaletwa katika Bunge. Tulisikizana ya kwamba, ikitoka katika Bunge la Kitaifa, wataileta katika Bunge la Seneti ili iweze kujadiliwa na kukubaliana. Kwa mda mrefu sana, hii nchi yetu ya Kenya imeketi bila kuwa na Tume ya kusimamia mambo ya kura. Ni jambo la kusikitisha sana kwa sababu hakuna nchi ambayo inaweza kuwa haina tume huru ya kusimamia mambo ya kura. Kwa hivyo, naunga sana ...
view
29 May 2024 in Senate:
Kipengele cha (d) kinasema kwamba watu watatu watateuliwa kutoka kwenye kamati ya vyama vya kisiasa. Miongoni mwa watu hao watatu, mmoja atatoka katika
view
29 May 2024 in Senate:
isiyo na Wabunge wengi. Mwingine atatoka katika party ya walio wengi ndani ya Bunge.
view
29 May 2024 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika kwa kunisahihisha. Mmoja atatoka chama cha walio wengi na mwingine atatoka chama cha walio wachache. Pia Mswada huu unapendekeza Law Society of Kenya (LSK) kuteua mtu mmoja. Vile vile, kutakuwa na mtu mmoja kutoka Institute of Certified Public Accountants of Kenya (ICPAK). Pia kuna watu wawili watakaoteuliwa na Inter- Religious Council of Kenya (IRCS). Mapendekezo ya kamati ya NADCO yamejumuishwa na sasa tuna Mswada kutoka Bunge la Taifa. Kulingana nami, hii ni sheria ambayo itatoa mwelekeo mzuri katika nchi yetu. Pia Mswada unapendekeza kuteuliwa kwa katibu atakayesimamia jopo hili. Katibu huyo atafanya kazi kwa kandarasi ya ...
view
9 May 2024 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, hili ni jambo la aibu sana katika taifa kwa sababu Bunge haliwezikuwa---
view