20 Aug 2024 in Senate:
Asante Bw. Spika. Gavana Kawira, swali langu ni moja tu kuhusu yule mshauri wako kwa mambo ya sheria anayeitwa Linda Gakii Kiome. Ulimuajiri kazi kama mshauri wako wa mambo ya sheria tarehe ishirini na nane, mwezi wa tatu, mwaka wa elfu mbili ishirini na tatu. Mwaka mmoja kamili baadaye, tarehe ishirini na sita, mwezi wa tatu, mwaka wa elfu mbili ishirini na nne, ulimpatia barua ya kumuachisha kazi. Je, baina yako na yeye, kulikuwa na kukosana, tabu, ama kutoelewena fulani ndio sababu akasema kwamba sio yeye aliyeandika ile barua, bali ile barua iliyoandikwa, si wewe uliyetia sahihi. Nataka kujua hayo ...
view
19 Aug 2024 in Senate:
Asante Bw. Spika. Naunga mkono Hoja hii kwa sababu ni Hoja muhimu inayoikumba Seneti. Mara nyingi baada ya kwenda likizo tunaitwa turudi kwa sababu ya mambo ya dharura yanayotendeka katika nchi na yanahitaji Seneti kupeana mwelekeo.
view
19 Aug 2024 in Senate:
Mara nyingi tumejipata baada ya kwenda likizo tunarudi hapa kwa sababu ya Hoja ambazo zinahitaji kuchukuliwa hatua. Pia ningependa kusisitiza ya kwamba position ya Seneta iko na changamoto sana. Katika positions zote zilizoko, Maseneta hawapati nafasi ya kutumia mgao wa pesa kikamilifu. Sio rahisi kupata kuwa Seneta amewekewa kitengo cha pesa anazoweza kutumia kwa miradi ya maendeleo. Mara nyingi Maseneta wanatumia pesa zao wenyewe.
view
19 Aug 2024 in Senate:
Ni jambo muhimu kuzingatia ya kwamba mambo yaliyo mbele yetu ni mambo ya kitaifa. Kwa sasa tuko hapa kwa sababu ya jambo hili la gavana kuwachishwa kazi. Ni jukumu letu kuchukua hatua ya kufanya uamuzi dhidi ya hii kesi ya gavana Kawira. Itakuwa vyema ikiwa tutaweza kugeuza kalenda ili tuwapatie nafasi Maseneta ambao wamekuja, wako hapa, waweze kurudi na kushughulikia wananchi mashinani. Naunga Hoja hii mkono.
view
19 Aug 2024 in Senate:
Can the Counsel go slowly? We are trying to catch up with these volumes as he keeps on leading the witness. We are also recording.
view
19 Aug 2024 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda. Nilikua nataka kujua jina la yule alikua akiongea.
view
14 Aug 2024 in Senate:
Asante Bw. Spika. Jina langu ni Stewart Madzayo, si kama alivyosema ndugu yangu. Amesema Mathayo kwa sababu ile “d” na “z” ameweka “t” na “h”. Ni sawa kwa matamshi ila amekosea kidogo kwa jina lenyewe. Bw. Spika, cha kwanza ninachotaka kuunga mkono ni kwamba twende kwa njia ile---
view
14 Aug 2024 in Senate:
Twende kwa njia ya kamati kwa sababu njia ya kamati au ile njia ya Bunge lote kuhusishwa, uamuzi huo utafanywa na Maseneta. Kila Seneta hapa ana usemi wake. Kuna tetesi tofauti lakini tukiwa kama The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate.
view