16 Oct 2018 in Senate:
mafunzo, Serikali inafaa kutangaza kujumuika kwao na Wakenya na wasichukuliwe kama wagonjwa wa ukoma ya kwamba hawawezi kupata kazi. Hiyo inawafanya kubaki kama mayatima. Ikiwa siwezi kupata kazi, basi nitarudi kule nilikotoka. Kwa hivyo, sisi kama Wakenya lazima tuzingatie mambo haya. Serikali nayo inafaa kujikakamua vilivyo ili kutekeleza wajibu wake kwa Wakenya.
view
16 Oct 2018 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, naunga mkono Mswada huu.
view
16 Oct 2018 in Senate:
Asante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Ningependa kumuunga mkono Sen. Pareno katika Mswada huu ambao ameuleta kuhusu jinsi ya kuwasilisha malalamiko ya wananchi katika Bunge. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
16 Oct 2018 in Senate:
Bi Spika wa Muda, tulikuwa hapa mwaka wa 2013 katika Bunge la Kumi na Moja. Wakati huo hatukuwa na sheria ambapo wananchi wangepewa nafasi ya kutoa malalamiko yao katika Bunge. Nina furaha kuwa sheria zetu zinawezesha watu wetu katika kaunti zetu au mtu binafsi kuleta malalamiko yake mbele ya Seneti hii na kusikilizwa. Jambo hili lilikuwa limeleta joto nyingi kwa MCAs wetu katika Serikali za Ugatuzi kutosikizana. Na tulikuwa na hiyo shida katika Bunge la Kumi na Moja. Lakini hivi sasa nimeona ya kwamba mmezingatia huu Mswada ambao umeletwa na dada Sen. Pareno. Nimeona ya kwamba hii sheria ambayo itatusaidia ...
view
16 Oct 2018 in Senate:
la kaunti, ombi hilo litakubaliwa. Kipengele kama hiki kinazuia utumiaji vibaya wa mamlaka katika serikali za kaunti. Tumegundua kwamba wakati mwingi, sheria zinatumiwa vibaya, haswa katika serikali za kaunti. Sheria hii itaweza kuweka mwelekeo ama mwangaza kisawasawa kisheria ili kila mtu ambaye ana jukumu kama katibu asitumie sheria hii kukataza malalamiko ambayo yamewasilishwa na mwananchi kwa bunge la kaunti ama serikali ya kaunti kwa misingi kwamba haikuzingatia muundo wa kuwasilisha ombi hilo kwa bunge. Tunataka kupitisha sheria hii ili itumike vivyo hivyo. Pia, maagizo ya vile watu wanaweza kuja pamoja na kuongea juu ya malalamiko yao, sheria hii itakuwa nzuri ...
view
16 Oct 2018 in Senate:
ambazo zitakuwa zinaenda katika bunge za kaunti.
view
2 Oct 2018 in Senate:
Asante, Mhe. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kueleza maoni yangu juu ya Mswada huu. Kwanza, nampa heko ndugu yetu, Sen. Cherargei kwa kuleta Mswada huu mbele ya Bunge la Seneti. Imemchukua muda mwingi wa kutafakari na kuona umuhimu sisi kuwa na sheria hii. Kama mwanasheria nasema ya kwamba kusimamisha mfanyikazi wa Serikali tukianzia Rais, Naibu wake, Makatibu wa Kudumu, Baraza la Mawaziri, gavana anayetawala kaunti aliyochaguliwa na wale wanaochaguliwa na gavana kufanya kazi na yeye kama vile County Executive Committee (CECs)
view
2 Oct 2018 in Senate:
ni lazima kuwe na mashtaka ambayo yanaweza kuwa na uzito fulani. Tunajua kuwa CECs katika kaunti zetu wanajiita mawaziri. Sijui ni kwa sababu gani hatujaweza kuchukua hatua kwa jambo kama hili. Tukienda katika mikutano mbalimbali, hawa hujiita mawaziri. Sisi tunajua Waziri ni yule anayechaguliwa na mhe. Rais wa Jamhuri ya Kenya. Mhe. Naibu Spika, kando na hayo, tunajua kuwa mashtaka au madai ya kuweza kumwondoa kiongozi kutoka mamlaka kama hayo niliyotaja ni lazima kuwe na mashtaka ambayo yanaweza kuwa na uzito fulani. Mswada huu ni muhimu sana kwa sababu katika Bunge lililopita mimi nilikuwa mmoja wa Maseneta ambao tulijishughulisha na ...
view
27 Sep 2018 in Senate:
On a point of order, Mr. Speaker, Sir.
view
27 Sep 2018 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, with tremendous respect, I refer the House to Standing Order No. 96(1) on page 66. I want my colleagues to listen to me carefully. Allow me to read this paragraph, 96 (1) which states- “Neither the personal conduct of the President, nor the conduct of the Speaker or of any judge, nor the judicial conduct of any other person performing judicial functions, nor any conduct of the Head of State or Government or the representative in Kenya of any friendly country or the conduct of the holder of an office whose removal from such office is dependent ...
view