Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 201 to 210 of 2266.

  • 12 Mar 2024 in Senate: Thank you, Mr. Speaker, Sir. I second the Motion. view
  • 29 Feb 2024 in Senate: Asante, Bw. Spika. Kwanza, nampa kongole Mwenyekiti wa Kamati hii ambayo iliandika Ripoti kuhusu kaunti kukosa kupeleka pesa ambazo wafanyikazi wanakatwa katika zile pension funds ama mahali pesa za watu wanaostaafu au waliostaafu huwekwa. view
  • 29 Feb 2024 in Senate: Ni makosa na ukiukaji wa sheria kutolipa fedha katika pension funds. Ni ukiukaji wa sheria wafanyikazi kukatwa pesa kwenye mshahara kila mwezi bila kulipwa baadaye wanapostaafu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate. view
  • 29 Feb 2024 in Senate: Wafanyikazi wengi wanaofanya kazi katika serikali za kaunti wanakatwa pesa na kwenda kwenye Local Authorities Pension Trust (LAPTRUST) ama Local AuthorityProvident Fund (LAPFUND). Malipo haya yana mipangilio kwamba mfanyikazi atakapostaafu atachukua pesa zake na zikaweza kumsaidia. view
  • 29 Feb 2024 in Senate: Asante, Bw. Spika. Wafanyikazi wanaostaafu hukatwa pensheni kwenye mishahara yao wakati wana nguvu na wanapofanya kazi kwa bidi. Mwishowe, wakifika miaka ya kustaafu hawawezi kupata pesa zao. Swala hili limeleta hasara kubwa katika familia nyingi nchini. Kuna wazee ambao wamesomesha watoto wao, wanakuwa watu wazima ambao inatakiwa waende chuo kikuu na pia wajikimu kimaisha na kuishi maisha mazuri. Wanafanya kazi lakini hali ya pesa zao inakuwa kana kwamba ni wizi. Kwa mfano, ikiwa mfanyikazi aliweka pesa kwenye LAPTRUST ama LAPFUND, kaunti aliyoifanyia kazi inatakikana iweke pesa hizo kisawasawa. Mfanyikazi huyu anapostaafu, anakosa kupata pesa zake kutoka kwenye kampuni hizi. Mfanyikazi ... view
  • 28 Feb 2024 in Senate: Bw. Spika, ningependa kuunga mkono Taarifa hii iliyoletwa hapa na Sen. Wakili Sigei, Seneta wa Kaunti ya Bomet. Jambo la kwanza kabisa ni kwamba uandishi wa habari ni kitu muhimu sana katika taifa lolote la kidemokrasia. Kama ilivyoandikwa katika Taarifa hili, ni jambo la kusikitisha kwamba polisi au watu waliotumwa walichukua sheria mikononi mwao na kuwapiga, kuwaumiza vibaya, kuwafurusha na kuharibu vifaa vilivyokuwa vinatumiwa kuchukua habari. Bw. Spika, mara kwa mara, shule za chekechea katika kaunti zote 47--- Wewe ulikuwa gavana na kwa hivyo unaelewa--- Kumekuwa na shida sana kujenga shule hizo. Changamoto nyingine ni kwamba walimu wa shule hizo ... view
  • 28 Feb 2024 in Senate: Bw. Spika, kila mtu anazungumza--- view
  • 28 Feb 2024 in Senate: Bw. Spika, langu ni kwamba waandishi wa habari ambao ni kitengo muhimu sana katika demokrasia yetu tunayojivunia ndani ya Kenya--- view
  • 28 Feb 2024 in Senate: Kitendo kama hicho ni jambo ambalo linafaa kukemewa. Kwa hivyo, hatua inafaa kuchukuliwa. Tuna Kamati ya Usalama wa Taifa na Masuala ya Kigeni katika Seneti. Kamati hiyo inafaa kuchunguza sababu za kutokea kwa kitendo hicho na kuhakikisha kuwa waandishi wa habari au wale waliokuwa wakichukua picha pamoja na watu wengine ambao hawakuwa huko Bomet wamearifiwa. Watu kama hao lazima wapewe ulinzi wa kutosha. Kwa hivyo, Bw. Spika, ninapounga mkono Taarifa hii, ningependa kusema kuwa ni vyema Baraza la Wanahabari Nchini Kenya, ambao ni wakubwa wa waandishi wa habari, linafaa kupewa nafasi ya kuangalia kwa kina na kuhakikisha kuwa haki ya ... view
  • 21 Feb 2024 in Senate: I second, Mr. Temporary Speaker, Sir. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus