24 Apr 2024 in Senate:
Bw. Naibu wa Spika, nachukua nafasi hii kama Seneta wa Kilifi nikijua kwamba Waziri aliye hapa ni dada kutoka Kilifi. Sikua nimempa kongole. Kama Seneta wa Kilifi, nampa kongole rasmi kwa kuchaguliwa kama Waziri wa Gender, Culture, the Arts and Heritage. Hio ni nafasi kubwa ambayo watu wa Kilifi walipewa. Namshukuru Mhe. Rais kwa kumchagua dadangu, Hon. Aisha Jumwa. Tumetoka mbali naye. Alikuwa womenrepresentative, kabla ya kuchaguliwa kama Member of Parliament (MP). Amefanya mambo mengi. Nina uhakika anaweza kazi kwa kuwa alikuwa na ujasiri wakati wa kujibu maswali.
view
23 Apr 2024 in Senate:
Thank you, Mr. Speaker, Sir. I enjoin myself with you to welcome the delegation from Malawi, being led by my brother Kondwani. He is the Leader of the Opposition there. I have had a word with him and we had lunch together. They are here for purposes of learning and knowing how Kenyans do their parliamentary duties. I am glad that he has come to the Senate and he will see how we operate. As we were talking, he told me that they only have the National Assembly and they do not have the Senate. Therefore, he wanted to know ...
view
23 Apr 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia. Ninaunga mkono alivyosema ndungu yangu, Sen. Faki. Ni kweli kwamba michezo ina faida yake. Michezo inawezakufanyika iwapo kuna uwanja mkubwa ama uwanja wa kimataifa. Kaunti kama Nandi anakotoka Sen. Cherarkey kuna wakimbiaji na wachezaji wa mpira. Hawachezi mpira sana kwa sababu kazi yao ni kukimbia. Kukimbia kwao kunaleta sifa katika nchi yetu ya Kenya. Hiyo inachangiwa na kuwepo kwa miundomsingi ama viwanja vya kukimbilia ni jambo la muhimu sana.
view
23 Apr 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda. Katika maeneo ya former Western Province kama vile Kakamega, viwanja vya mpira ni vingi kule. Hiyo ndio sababu vijana wengi kutoka Western Province ni wachezaji wa Harambee Stars. Jambo la kusikitisha ni kwamba kwa miaka mingi, timu za Kenya zimekuwa zikipata wachezaji na wakiambiaji wengi kutoka Pwani. Hata hivyo, tangu utawala wa Rais hayati Moi, sehemu hiyo haijakuwa ikizingatiwa. Kwa sababu hiyo, ukiangalia timu ya Harambee Stars, hakuna hata mtu mmoja kutoka upande ule. Ni jambo la kusikitisha kwamba sehemu iliyokuwa ikisifika sana zamani kwa kutoa wachezaji maarufu kama Ali Kajo, Sungura, Kadir Fara miongoni ...
view
23 Apr 2024 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate.
view
23 Apr 2024 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, naunga mkono Hoja hii. Pesa inafaa kutengwa na Wizara ya Michezo, Sanaa na Masuala ya Vijana ili viwanja vitengenezwe. Uwanja wa Michezo wa Mombasa hujatengenezwa. Ni vyema shilingi bilioni moja nukta saba itengwe ili watu wa Pwani wafaidike pia. Naunga mkono Hoja hii.
view
23 Apr 2024 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, Kanuni za Kudumu za Seneti zinasema kuwa huwezi kumtaja mtu ambaye hayuko ndani ya Bunge hili kwa sababu hawezi kujitetea. Vile vile, hufai kumtaja mtu ambaye hakupewa taarifa kuwa anahitajika kujitetea. Seneta alisema kwamba Bw. Joho alionekana akibeba kitita na kuwa pesa zile hazikutumika vizuri. Je, ni sawa Seneta ambaye ninaenzi sana, ambaye pia ni Kiranja wa Walio Wengi, kusema kuwa aliona Bw. Hassan Joho akiwa amebeba kitita, ilhali hayuko hapa wala hakuulizwa aje hapa ili ajitetee?
view
20 Mar 2024 in Senate:
Bw. Spika, nasimama kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu Kipengele 53(1) kuomba Taarifa kutoka kwa Kamati ya Ardhi, Mazingira na Mali Asili kuhusu uharibifu na uchafuzi wa mazingira kutokana na uchimbaji wa madini ya chuma katika eneo la Jaribuni, Kauma, Kaunti ya Kilifi. Katika Taarifa hiyo, Kamati hiyo inafaa kuangazia yafuatayo- (1) Kuchunguza uharibifu wa uchafuzi wa mazingira na athari za afya zinazotokana na uchimbaji wa madini ya chuma katika eneo la Jaribuni, Kauma, unaotekelezwa na Kampuni ya China inayoitwa Wu Ying. (2) Ieleze hatua gani Wizara ya Madini na Uchumi Samawati na Mamlaka ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mazingira ...
view
20 Mar 2024 in Senate:
Bw. Spika, nasimama kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu Kipengele 53(1) kuomba Taarifa kutoka kwa Kamati ya Ardhi, Mazingira na Mali Asili kuhusu uharibifu na uchafuzi wa mazingira kutokana na uchimbaji wa madini ya chuma katika eneo la Jaribuni, Kauma, Kaunti ya Kilifi. Katika Taarifa hiyo, Kamati hiyo inafaa kuangazia yafuatayo- (1) Kuchunguza uharibifu wa uchafuzi wa mazingira na athari za afya zinazotokana na uchimbaji wa madini ya chuma katika eneo la Jaribuni, Kauma, unaotekelezwa na Kampuni ya China inayoitwa Wu Ying. (2) Ieleze hatua gani Wizara ya Madini na Uchumi Samawati na Mamlaka ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mazingira ...
view
20 Mar 2024 in Senate:
Asante Bw. Spika. Naunga mkono Taarifa iliyoletwa na ndugu yangu, Seneta wa Kaunti ya Meru, kuhusu kushikwa kwa Sniper. Sio kushikwa peke yake, bali kutolewa ndani ya nyumba na watu ambao hawajui, waliojitambulisha kwa familia na yeye mwenyewe, halafu wakamueka kwa gari na kupotea naye. Vitendo kama hivi vimetendeka sana na vimefanywa katika mikono ya polisi. Watu wanakuja kwa nyumba, wakishajitambulisha kwamba wao ni polisi, wanatoa mpaka vitambulisho na wanabeba mtu wanaenda naye. Hatimaye, tunaona huyo mtu anapatikana ametupwa mahali fulani baada ya siku fulani akiwa amekufa. Tabia kama hizi, hivi sasa zimeanza kuzidi kwa sababu si Meru tu ambapo ...
view