Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 391 to 400 of 2266.

  • 26 Jun 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate. view
  • 26 Jun 2023 in Senate: Maanzo, Sen. Abass, Sen. Gataya Mo Fire, Sen. Mumma, Sen. Tabitha Mutinda, Sen. Miraj na Sen. Chimera, ndugu yangu. Ripoti kama hii ikiandikwa hivi--- view
  • 26 Jun 2023 in Senate: Hii ni Ripoti mwafaka. Hii kamati imefanya kazi yake. Hawa watu kumi na mmoja wamepata kwamba kuna hatia dhidi ya naibu gavana. Hatia sio moja, bali zimepatikana hatia mbili dhidi yake. Kosa la kwanza na la pili. Kawaida, kosa likipatikana hata moja katika Kamati kama hii na walete hapa, Seneti huwa inaunga mkono Ripoti ile na yule mtu huwa anafaa kuachishwa kazi. Bw. Spika, tunaona ya kwamba tunao umuhimu kwamba katika lile shataka la kwanza ambayo ni mambo ya kununua bidhaa na utendakazi kinyume na ile sheria inayotambuliwa ya procurement. Katika viti vyote hivi vinavyo kaliwa na wakubwa, sijasikia kiti ... view
  • 26 Jun 2023 in Senate: On a point of order, Mr. Speaker, Sir. view
  • 26 Jun 2023 in Senate: Bw. Spika, tunaelewa kabisa ya kwamba ni haki ya Sen. Cherarkey kuongea vile anavyoongea. Lakini, Kanuni zetu za Kudumu katika Bunge hili zinasema ya kwamba, huwezi kuongea juu ya mtu ambaye hayuko hapa. Wewe umefanya uamuzi huo mara nyingi. Je, nauliza, ni sawa kwa ndugu yangu Sen. Cherarkey na anaelewa sheria na amekuwa kiongozi wa Kamati ya Sheria, kutaja jina la mtu ambaye hayuko hapa ndani ya Bunge kujitetea? view
  • 22 Jun 2023 in Senate: Asante Bw. Spika. Kwanza, ninataka kumpa kongole ndugu yangu Sen. Wambua kwa kuleta Mswada huu. view
  • 22 Jun 2023 in Senate: Ninatambua kwamba nchi yetu ya Kenya ni ya ukulima ama agricultural country . Maana tumetegemea ukulima wa aina mbili. Kuna wale wakulima wa Tingatinga na wale wasiojiweza wanalima kwa majembe. Kuna wale wengine wanaolima kimaskini zaidi. Kama sisi wengine tulipokuwa tukikua zamani, na hadi mpaka sasa, kilimo kama hicho kinaendelea huko Kilifi. Akina mama zetu huwa wanalima na kiserema. Yaani nguvu za mkono ndizo zitakazo kulisha. Ukilima shamba lako na upande bidhaa zako, utapata mavuno. Umuhimu wa Mswada huu ni kwamba ni lazima Serikali yetu ijukumike na ijihusishe zaidi. Tunataka walete vitu kama mbolea ili wakati wa upandaji wa hiki view
  • 22 Jun 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate. view
  • 22 Jun 2023 in Senate: chakula, tuweze kupata kwa wingi zaidi. Tuone ya kwamba chakula cha kutosha kipatikana kirahisi. Pili, hata ukienda kwa daktari, kama afya yako si nzuri, unaambiwa ule ndengu, ama mboga. Hii ni mojawapo wa vyakula ambavyo vinaweza kuleta nguvu. Kwa hivyo, ni muhimu Serikali iweze kujihusisha zaidi na kusaidia wakulima. Nina hakika kuwa hakuna mahali popote nchini ambapo ndengu haziwezi kumea. Serikali iweze kupeana mkono wake na kusaidia wakulima wa ndengu. Sio kusaidia wakulima wa kahawa na majani chai peke yake. Wakisaidika, mazao yao yatakuwa bora na watapata mafanikio, ajira na waweza kulisha taifa letu chakula kitakapotosha kwa wananchi wetu wa ... view
  • 21 Jun 2023 in Senate: Asante Bw. Spika. Kwanza nampa ndugu yangu, Sen. Cherarkey, kongole kwa kuleta hii Kauli. Wanaspoti wanapokuwa katika ujana wao, wanaleta sifa kubwa nchini, tukielewa ya kwamba kila mwanaspoti katika nchi za ulaya amewekewa insurance ambayo inaweza kumuangalia kukitokea ajali ya aina yoyote. Jambo la kusikitisha ni kwamba hapa kwetu wanaspoti hatuwapi kipau mbele. Baada ya kuleta sifa, ifikapo uzeeni wao, ni hatua gani itachukuliwa ili kuona mwanaspoti anaishi vizuri? Yule dada aliyetuletea sifa kubwa nchini, Faith Kipyego, alifanya kitendo ambacho hakuna binadamu mwingine ameweza kukifikia. Hii ni sifa kubwa sana ya Kenya. Nawashukuru Wakenya ambao walitimiza azma yake ya kununulia ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus