6 Jun 2023 in Senate:
Bw. Spika, dhambi kama hizi hatuwezi kuruhusu hapa ndani. Ninaunga mkono Sen. Cherarkey, ndugu yangu wa Nandi Kaunti, kwa kuleta swala hili hapa.
view
31 May 2023 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Pia mimi naungana na wewe kuwakaribisha wanafunzi wa KUSA, kwa kuja katika Bunge letu la Seneti. Jambo muhimu ni kuwa, mtajua taratibu tunazoenenda nazo katika Bunge la Seneti. Kanuni za Kudumu ziko na ndizo zinazoongoza Bunge hili. Bw. Spika, mkiwa hapa hapa mtajifunza mengi. Kuna uhakika ya kwamba wengine wenu wanaweza kuwa Maseneta na mkajikuta hapa. Nina hakika kwamba mnatumia wakati huu kuona viongozi wenu walioko Bunge la Seneti hivi sasa. Pia nyinyi mko na uwezo na taaluma. Mkiendelea katika maisha yenu, hadi itakapotakikana na wananchi kutoka maeneo yenu muwe Maseneta, mnaweza kujipata mahali hapa. Kwa hiyo, ...
view
31 May 2023 in Senate:
Bw. Spika, kama kuna wakati nchi hii inahitaji usaidizi ni msaada wa madaktari. Wanafunzi wanaosomea udaktari ni wa maana kwa sababu husaidia wagonjwa. Ni jambo la kusikitisha kuona kuwa wanafunzi wanaosomea udaktari--- Chuo hicho kinahusika na uchunguzi wa magonjwa tofauti tofauti. Uchunguzi huo waweza kufaidi watu. Kwa hivyo, wataweza kuokoa maisha ya Wakenya. Kuna mgawanyiko kati ya hospitali hiyo na chuo kikuu ambapo kuna wanafunzi wanaosomea udaktari. Kuna baadhi ya watu mabwenyenye ambao wameenda kuchukuwa upande mwingine. Haikuwa sawa kuwa na legal notice ambayo ilichapishwa ili kujitenga na chuo kikuu na sehemu nyingine ikachukuliwa na watu wengine. Kamati ya Afya ...
view
31 May 2023 in Senate:
hiyo inafaa kuondolewa ili wanafunzi wanaosomea udaktari wapate nafasi ya kwenda upande ule mwingine kufanya uchunguzi wa magonjwa katika taaluma hiyo. Maoni yangu ni kuwa ikiwa Petition hii itapelekwa kwenye kamati husika, ni lazima ichunguzwe kwa kina. Wanafaa kutupilia mbali hiyo legal notice ili wanafunzi waweze kuendelea na taaluma yao vizuri.
view
31 May 2023 in Senate:
Bw. Spika, ningependa kumuuliza Waziri maswali mawili.
view
31 May 2023 in Senate:
Bw. Spika, swali langu la kwanza linatokana na majibu yake ya swali la 8. Kwa hivyo, ningependa unipe muda mchache niweze kuongea na Waziri. Bw. Waziri, jina ni Sen. Stewart Madzayo. Mimi ni Seneta wa Kilifi Kaunti na Kiongozi wa Wachache katika Seneti. Swali la nane linasema kwamba kulikuwa na tani 73 za mahindi, mchele na marahagwe yaliyoharibika ambayo yalichangia matatizo katika shule hiyo. Jambo la kushangaza ni kwamba hatua iliyochukuliwa na Serikali ni kutoa chakula hicho katika shule ya Wasichana ya Mukumu iliyoko katika Kaunti ya Kakamega na kukipeleka kiwanda cha Bamburi Portland Cement kule Mombasa, chini ya usimamizi ...
view
31 May 2023 in Senate:
Bw. Spika, ningependa kumwona Waziri ninapomwuliza maswali. Sasa Seneta ananizuia.
view
31 May 2023 in Senate:
Bw. Spika, chakula hicho kilipelekwa katika kiwanda cha Bamburi Portland Cement kilichoko kule Mombasa ili kuharibiwa. Jambo la kushangaza ni kuwa Bamburi Portland Cement ni kampuni ya kutengeneza simiti ilhali chakula hicho kilipelekwa huko kuharibiwa. Ningependa kujua sababu ya kuchukua chakula hicho kutoka Kakamega kwenda kuharibiwa katika kiwanda cha Bamburi Portland Cement kule Mombasa ambayo ni kampuni ambayo inahusika na simiti. Pili, kwa nini ulipeleka chakula hicho kule kuharibiwa? Chakula hicho kilisafirishwa kutoka Kakamega. Kilipita sehemu nyingi sana kama vile Mlolongo ambapo kuna kampuni nyingi sana.
view
31 May 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
31 May 2023 in Senate:
Bw. Waziri, tafadhali nisikize. Kuna kampuni nyingi sana hapa Mlolongo zinazohusika na mambo ya saruji kama vile Simba na Rhino. Kwa nini ukawacha hizi zote, ukapeleka vyakula katika kiwanda cha Bamburi Cement kuviharibu? Si huo ni uharibifu wa pesa za Serikali kulipa pesa hizi zote kupeleka hicho chakula kiharibiwe. Hilo ni la kwanza. Bw. Waziri, ningependa ujibu swali langu sasa. Umejibu vizuri sana kuhusiana haya mambo ya Mukumu Girls’ High School. Nilivyokwambia awali, mimi natoka Kilifi Kaunti ambapo tuko na shule nyingi. Tuko na shule ambazo zinajengwa na wanavijiji wenyewe na pia za kaunti. Pia wanasiasa wanajaribu kusaidia kuinua hali ...
view