Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 421 to 430 of 2266.

  • 31 May 2023 in Senate: Bw. Spika, sijui kama jina langu ni kama la Kimaasai. view
  • 31 May 2023 in Senate: Bw. Spika, kama kuna wakati ambao familia huwa zinateseka ni wakati wa kufurushwa kiholela kutoka kwa makazi yao. Watu husema, uchungu wa mwana aujuaye ni mama. Hata hivyo, huwa ni uchungu kwa jamii yote kuhamishwa kutoka mahali wanaita nyumbani bila kujua pa kwenda. Wakaazi wa Chokaa ni Wakenya na wanaishi katika kijiji hicho. Hawakuchagua lakini hayo ndio makao yao. Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba miaka 60 baada ya Kenya kupata Uhuru, tunafurusha Wakenya wengine kutoka sehemu wanazoita view
  • 31 May 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 31 May 2023 in Senate: nyumbani, yani makazi yao. Wanabaki katika njia panda bila kujua waende mbele au nyuma. Kitendo ambacho kampuni ya KPC ilifanya kinafaa kukemewa. Kuna watoto wa shule, kina mama, wagonjwa na watu wa jamii mbalimbali ambao tunaishi nao. Hao ndio hupata tabu zaidi. Ni jambo la kusikitisha kutekeleza kitendo hicho ilhali kulikuwa na amri ya Mhe. Rais kwamba watu hao wasifurushwe. Leo hii wako nje. Hatujui watakaowalipa ni akina nani. Watoto wa shule hawajui wafanye nini. Hata wakienda shuleni, watarudi wapi? Wagonjwa walioko hospitalini hawajui watajikimu vipi. Ni hali ya mateso kule Chokaa. Namuunga mkono dada yangu kwa kuleta hii Petition ... view
  • 31 May 2023 in Senate: ambayo inahusika inafaa kuangalia maslahi ya watu hao ambao wamefurushwa kutoka kwa makao yao. Haki inafaa kutendeka kwa sababu kila Mkenya ana haki ya kuishi kwao. Jambo hili linatendeka sana hususan kule Kilifi. Tulikuwa tunafikiri ni sisi peke yetu. Waswahili husema; “Ukiona cha mwenzako kikinyolewa, chako tia maji.” Tabia hiyo pia imeanza kufanyika huku na hatujui itakuwaje. Tabia za watu kufurushwa hususan na kampuni za Serikali kama KPC zinafaa kukoma. Watu wanafaa kuongea ili kupata njia ya kuwapeleka mahali pengine badala ya kufurushwa na tingatinga na kuvunja nyumba zao maanake ni Wakenya wenzetu. Kwa hivyo, Bw. Spika--- view
  • 31 May 2023 in Senate: Nishamaliza Bw. Spika. view
  • 30 May 2023 in Senate: Asante, Bw. Spika. Kwanza, nampatia kongole ndugu yangu kwa kuleta hii Taarifa wakati huu ambao unafaa. Tunaelewa kwamba watoto wetu wengi wanaenda kutafuta mapato katika nchi za ughaibuni. Mara nyingi wakiondoka hapa, huwa tunajua anwani zao na namba za simu zao za mkono. Hata hivyo, mara tu wanapofika kule, huwa ni shida sana kuwafikia. Tumekuwa na vifo katika utendakazi wao na kupoteza maisha. Senator wa Kaunti ya Nandi; mchapa kazi, amefanya jambo jema sana kwa kuandika Taarifa yake ya kwamba ni lazima zile kampuni ambazo ziko hapa na zinachukua watoto wetu na kuwapeleka kule kwenda kufanya kazi ziajibike. Inafaa wanajue ... view
  • 30 May 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 30 May 2023 in Senate: Bw. Spika, ni muhimu kwa hii Kamati yetu, mimi nikiwa mmoja wa wanakamati, kuangazia suala hili. Namuona Mwenyekiti wangu yuko pale. Naomba kwamba suala hili liwajibikiwe isawasawa. Ikiwezekana, mpatie ruhusa Kamati hii iweze kuambatana na hata aliyeleta Hii Statement hapa ili kuangalia masuala haya kwa kina. Tunataka kujua kwa nini watoto wetu wakienda nchi za Uarabuni wanapata tabu kuliko nchi za ughaibuni. view
  • 30 May 2023 in Senate: Asante, Bw. Spika. Kwanza, ni hoja nzuri sana kwa sababu sijawahifika Kaunti ya Turkana. Kwa hivyo, nitapata nafasi ya kuweza kuonana na ndugu zetu Waturkana. Itakuwa jambo nzuri zaidi kuwa hili Bunge letu la Seneti litakuwa na kikao huko Kaunti ya Turkana. Tukiangalia katika miaka karibu 50, nchi inayoitwa Dubai ilikuwa ni jangwa; hakukuwa na rasilimali yoyote kule. Ilikuwa haijawahi kuonekana. Miaka 50 iliyopita, ukifika kule hivi sasa, siyo jangwa tena. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus