3 May 2023 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Sen. (Dr.) Khalwale ni mpiganaji wa ng’ombe lakini hilo ni swali la kutafakari. Bw. Spika, nakushukuru pamoja na watu wa Kaunti ya Kilifi wanaojua mimi ndiye Seneta wao. Si rahisi jambo hili kutendeka lakini kwa mara ya tatu nimeweza kurudi na kushirikiana na wenzangu ndani ya Bunge hili. Yale yote ndugu zangu kutoka sehemu hiyo watajifunza hapa wanafaa kuyaangalia yanayofaa na inayoweza kutekelezwa katika Bunge la Kaunti ya Kilifi ili wasonge mbele Asante.
view
27 Apr 2023 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Ninaunga mkono yote yaliyosemwa katika hii Hoja. Kuna uhuru wa dini. Kipengele cha 32 cha Katiba yetu kinasema kwamba kila mtu ana uhuru kujumukika kimawazo, kidini, kimafikra na pia kuomba Mungu vile atakavyo. Hivi majuzi, tumekuwa na mshikemshike ambao ulitokea Shakahola, Eneo Bunge la Magarini, Kaunti ya Kilifi. Ni jambo la kusikitisha. Ndio sababu Seneti imeona kuna umuhimu kuwa na jopo ambalo litaangalia suala hili.
view
27 Apr 2023 in Senate:
Tumeona kuwa ni wengi ambao wanaanzisha dini hizi. Imekuwa rahisi sana katika nchi yetu ya Kenya. Mtu anenda kwa Registrar of Societies kuomba kibali kuanzisha dini yake. Anatoka hapo na cheti cha kuanzisha dini yake. Kuna wengine nia zao ni safi. Lakini wengi wao, tumekuja kuona ya kwamba wanaanzisha dini zao kwa sababu ya pesa. Hizi pesa zimeanza kupita mpaka zimeingilia wale tunaowaweka mbele ya madhabahu. Wameziweka mbele pesa sana mpaka zimekuwa kama shetani. Ni muhimu sheria mwafaka zizingatiwe. Tumeona katika eneo la Shakahola, watu wengi wamepoteza maisha yao. Wengi walioathirika ni watoto wachanga. Mimi ninakubali ya kwamba, kama kuna ...
view
27 Apr 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
27 Apr 2023 in Senate:
Watu kama sisi ambao tunatoka katika sehemu hiyo, imebidi tujiweke kando kwa sababu, tuko na uchungu sana. Kwa hivyo, tunaweza kukosa mwelekeo wa fikira, mawazo ama kujadiliana. Ndio sababu niliona nikae kando ili niangalia suala hili kisawasawa. Mimi nitalivalia njuga na kuona ya kwamba suluhisho imepatikana. Mara nyingi, kuna mzaha unaofanywa na wanaojiita wakuu wa dini. Tuliona wakati fulani katika runinga, wakiweka sindano kwenye vidole vyao na kugeuza maji yaliosawasawa ya kunywana kuwa damu. Na kwa sababu mtu ni mgonjwa na hana imani, anatiwa imani ya kwamba amepozwa kwa sababu ametolewa damu chafu na kubakishwa ile safi kwenye mwili. Hayo ...
view
25 Apr 2023 in Senate:
Bw. Naibu Spika, Seneta wa Marsabit ni ndugu na rafiki yangu, namheshimu sana. Singependa kumuingilia kati, lakini ametaja pesa za America kama “dollari”. Je, pesa za America zaitwa dollari ama zina jina lingine la Kiswahili.
view
25 Apr 2023 in Senate:
Bw. Naibu Spika, unasema tu
view
25 Apr 2023 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda. Ninamshukuru dada yangu kwa kunialika niunge mkono Hoja hii. Uongozi wa dini humu nchini unaruhusiwa. Katika maeneo ninayotoka, kuna kanisa la Good News International, ambalo linaongozwa na Pastor Paul Mackenzie Nthenge. Kulingana na sheria zetu za dini, mtu yeyote anaweza kujiunga na kanisa lolote analotaka na kuomba Mwenyezi Mungu. Hivi majuzi tumepoteza zaidi ya watu 86. Hawa
view
25 Apr 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
25 Apr 2023 in Senate:
watu wamekufa wakiwa Kaunti ya Kilifi. Ni jambo la kusikitisha ya kwamba Wakenya wanapoteza maisha yao kwa sababu ya kiongozi wa dini. Jambo la kusikitisha ni kwamba, tulipoanza ugatuzi, tulikosea zaidi kwa kutomuweka gavana kwenye Kamati ya Usalama. Pastor Mackenzie amekuwa Kaunti ya Kilifi kwa zaidi ya miaka 16.
view