Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 451 to 460 of 2266.

  • 25 Apr 2023 in Senate: Hii dini yake imekuwa ikiendelea ndani ya Kaunti ya Kilifi zaidi ya miaka 16. Mtu huyu anajulikana sana na amekuwa akizunguka kila mahali. Lakini, juzi vilivyogonga vichwa vya habari ni kwamba alianza na msimu wake ya kwamba watoto wasifanye mitihani. Na security inaona. Baadaye, watu walipopiga kelele, akashikwa akapelekwa kortini, akaachiliwa kwa dhamana ya Kshs10,000. Akaja tena akashikwa kwa sababu alisema sio kufanya mtihani peke yake lakini, pia watu waanze mambo ya view
  • 25 Apr 2023 in Senate: Bw. Spika wa Muda, utakuja kuona kufikia wiki zilizokwisha, alianza kwa kuwakataza watu wasile chakula au kunywa maji ama kujisaidia kwa njia yoyote kwa sababu dini yake inasema ukienda huko, unaenda kukutana na Yesu. view
  • 25 Apr 2023 in Senate: Kuna mashirika tofauti ya kuangalia vitengo vya sheria. Kufikia hivi sasa, kuno vitengo vya Directorate of Criminal Investigations (DCI), vile vya ujasusi, kunao machifu, County Commanders, wale wa polisi na kaunti Kamishna, ambaye anaketi katika mambo ya security. Ninataka kuuliza kitu kimoja, je, kitendo kama hiki kilipokuwa kikitendeka, watu hawa walikuweko? Wanajua hiyo? Na kama wanajua, ni hatua gani walichukua? view
  • 25 Apr 2023 in Senate: Bw. Spika wa Muda, Kaunti Kamishna mwenyewe, anaketi kwa hiyo security view
  • 25 Apr 2023 in Senate: Wale waliokuweko miaka 16 iliyokwisha ndani ya Kauti ya Kilifi lazima wajukumike. Kama huyo mtu alianza dini miaka 16 iliyokwisha, basi Makaunti Kamishna wote ambao walikuwa huko, lazima waitwe na kuhojiwa. Kama walimwona mchungaji Ezekiel Nthenge akianzisha shirika lake la hili kanisa, ni hatua gani ambayo ilichukuliwa? view
  • 25 Apr 2023 in Senate: Mimi ninatoka katika eneo hili na ningependelea unisaidie uniongeze dakika fulani niweze kueleza kwa sababu niko na uchungu sana. Watu wangu wamekufa. Ni lazima taifa liweze kujua kuwa tunaongea juu ya mambo ya Shakahola. Ninataka uniongeze dakika tatu au nne ili niweze kumaliza. view
  • 25 Apr 2023 in Senate: Asante, ndugu yangu. Ni jambo la kusikitisha kuona ya kwamba hakuna hata Kaunti security team yoyote ama Kamati ambayo ilikuwa inawezakugundua hii. Swala la kujiuliza ni kwamba, huyu Kaunti Kamishna na security team yake ikiongozwa na police commander, na ofisa mkubwa wa DCI, walikuwa wapi ilhali wanaishi na sisi kila siku kwenye mitaa na kupokea mishahara yao kila siku? Lakini, wakisikia kuna maandamano, wanajua kila kitu mpaka wanatuambia ‘kesho tutatengeneza ma bomb tuweke. Lakini, hawajui saa ya watu kufa. Kifo cha mtu sio kwamba hujui ama umeharibu. view
  • 25 Apr 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 25 Apr 2023 in Senate: Tuchukue mambo kwa uzito unaofaa . Watu wamepoteza maisha yao. Watu wametoka sehemu mbalimbali kuja kutafuta wapendwa wao. Yaliyotendeka yote kumi, la kumi na moja ni kwamba kulikuwa na utepetevu wa mambo ya usalama. Watu waliotakikana kuangalia mambo haya ni Kaunti Commander, Kaunti Kamishna na waliokuwa katika Kitengo cha Ujasusi la DCI. Vilevile, tuko na machifu, wazee wa mitaa, wazee wa nyumba kumi. Kwa hivyo, mambo yetu ya usalama lazima yazingatiwe zaidi. view
  • 25 Apr 2023 in Senate: Ninajua hata Rais mwenyewe ameweza kutamka akisema huyu mtu ni terrorist. Kwa hiyo, ninamwomba afute kazi Kamishna ambaye anaketi kama Chairman wa Kamati ya National Security and Foreign Relations akifuatiwa na Kamanda wa polisi, DCI na wale wako chini wanaohusika mpaka kwenye vijiji. Wasiwe katika kazi zao. Huwezi kupata kitu kama hiki ambacho kinauwa watu na wewe usichukue hatua yeyote. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus