25 Apr 2023 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, mimi kama Seneta wa Kaunti ya Kilifi, ninasikitika. Niko pamoja na watu wote ambao wamepoteza wapendwa wao. Tunawaombea Mwenyezi Mungu. Lakini, jambo kama hili ni lazima lichunguzwe, lifikishwe mwisho na wale watakaopatikana walizembea kwa kazi zao, Rais achukue hatua ya kuwafuta kazi.
view
18 Apr 2023 in Senate:
Bw. Spika, kwa heshima na taadhima ya hili Bunge la Seneti, hata ndugu yangu Sen. (Dr.) Khalwale ambaye ninamheshimu sana, anaweza kutanguliza hili swala. Tukimwangalia ndugu yetu, Sen. Methu, ni kijana shupavu, mdogo, pia ni Seneta katika Bunge hili na anaelewa sana jinsi tunatakikana kuvaa tukiwa ndani ya Bunge. Tukimwangalia ndugu yetu, Sen. Methu, amevaa kwa njia ambayo haina heshima, ya kushusha hadhi ya Seneti na haikubaliki kwa mtu ambaye anaiga wale wakubwa wake walio ndani ya Bunge hili la Seneti. Ukiangalia vile Sen. (Dr.) Khalwale alivyovaa na vile wale waheshimiwa wengine,
view
18 Apr 2023 in Senate:
walio kule kama Sen. Mungatana MGH na yule ndugu yangu ambaye yuko pale, na zote pia upande huu, ukituangalia vile tulivyovaa, tuko kwa hali ya kwamba tuna heshima ndani ya Bunge. Vile alivyo vaa ndugu yangu, Sen. Methu amevaa kwa njia ambayo haina heshima na ya kushusha hadhi ya Seneti. Bw.Spika, naomba umchukulie hatua unayofikiria kwa sababu ile nguo aliyovaa sio haki.
view
18 Apr 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
18 Apr 2023 in Senate:
Bw. Spika, hili Bunge la Seneti ni Bunge la heshima na tunajiheshimu tukiwa hapa. Hatuna ubaguzi. Huku kuna waheshimiwa ambao wamevaa kwa hali ya heshima zaidi na upande huu vile vile. Lakini tukiangalia upande huu, kuna doa moja ambalo ni bwana mwenyekiti wangu, ninamheshimu, ni kijana mdogo vile vile kama Sen. Methu. Sijui hii tabia wameanza lini. Vile vile, kichapo kile kile alichokula Sen. Methu, ni kichapo kile kile ambacho ndugu yangu, Sen. Thang’wa - ambaye ni rafiki yangu mkubwa na ninamheshimu sana - anapaswa kukula pia. Anafaa kuvaa kama Sen. Wakili Sigei, ndugu yangu Kiranja wa Walio wengi Bungeni, ...
view
18 Apr 2023 in Senate:
On point of order, Madam Temporary Speaker.
view
18 Apr 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
18 Apr 2023 in Senate:
Thank you, Madam Temporary Speaker. When a person rises on a point of order and is given the audience by the Speaker--- My colleague, Sen. (Dr.) Oburu, was on his feet.
view
18 Apr 2023 in Senate:
Madam Temporary Speaker, kindly can I be given a chance?
view