22 Mar 2023 in Senate:
Ahsante, Bi. Spika wa Muda. Mimi nilikuwa hapa tokea mwaka 2013. Damu ya Maseneta walioko hapa, wengi wao ni vijana. Kwa hivyo, mimi ninaelewa wakiwa na harakati hizi ya kushindana. Ndugu zangu shupavu, Sen. Chimera, Maseneta wa Nandi, Kericho na wengine ni washupavu na damu zao ni moto.
view
22 Mar 2023 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, cha kwanza ninaomba---
view
22 Mar 2023 in Senate:
Niruhusu niweze kuweka Mjadala huu kwanza katika Bunge la Seneti hivi sasa.
view
22 Mar 2023 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, sijui kama hiyo uliyomruhusu Sen. Chute aseme ni hoja ya nidhamu. Lakini, wacha niendelee. Ni maono mazuri kwa sababu vijana kama ndugu yangu Sen. Cheruiyot hawezi kupata. Bi. Spika wa Muda ungeniruhusu kuweka huu mjadala mbele ya Bunge la Senati hivi sasa ile tuweze kuhairisha kikao hiki na kujadiliana mjadala huu ambao ni wa kitaifa na hususan unahusikana na ukatili wa polisi wa kufungia Waheshimiwa na wananchi katika vituo vya polisi kote nchini pamoja na viongozi wao.
view
22 Mar 2023 in Senate:
Ngoja ninakuja. Usifanye haraka, mosmos. Chama cha Muungano wa Azimio la Umoja kilipeana taarifa kwa mkuu wa polisi wa kituo cha Nairobi, kuarifu kuhusu maandamano ya amani yaliyokuwa yafanyike katika Wilaya ya Jiji la Nairobi, tarehe 20.03.2023. Walitumia haki yao kulingana na Kipengele 37 cha Katiba kuandamana kwa amani bila kubeba silaha zozote. Siku ya maandamano ilikuwa siku ya amani sana. Mimi mwenyewe nikiwa mmoja wa wale watu, tuliweza kutoka hapa kama waheshimiwa na tukaenda tukisema ya kwamba ni haki yetu kulingana na kipengele cha 87 ya kwamba tunaweza kuandamana. Ni jambo la kushangaza. Na mimi naomba, isije ikatokea upande ...
view
22 Mar 2023 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, sisi tulikuwa tunadai haki zetu. Cha kustaajabisha ni kwamba askari waliweza kupiga teargas bila ilani yoyote na bila kukasirishwa.
view
22 Mar 2023 in Senate:
Tafadhali ndugu yangu Sen. Cherarkey, jambo hili nilalozungumzia linahusika na kitu cha kitaifa kilichotendeka upande wa upinzani. Kama hakina maana kwako, tafadhali wacha Bi. Spika wa Muda aniskize na wananchi wote katika Kenya saa hizi wananiskiza. Kwa heshima, tafadhali.
view
22 Mar 2023 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, tuko na kijana aliyeuaua huko Kisumu. Tuko na kijana ambaye alikuwa anasoma katika Chuo Kikuu cha Maseno. Hawa wawili walipigwa risasi na kufa. Sio kupigwa risasi kuumia tu, ama kuwa wagonjwa; walipigwa risasi na polisi. Kawaida katika kitengo hiki cha 87 cha Katiba--- Sasa hivi, nimesema ya kwamba Sen. Cherarkey aondoke, hivi sasa, kumekuja mwingine tena, anakuongelesha na huniskizi.
view
22 Mar 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
22 Mar 2023 in Senate:
Kitendo hicho cha kupiga risasi ni kinyume cha sheria. Askari hawaruhusiwi kupiga watu risasi. Askari hawaruhusiwi kurusha hata hiyo teargas ambayo inarushwa wakati kuna fujo. Lakini haya yalikuwa maandamano ambayo yalikuwa yanafanywa katika nchi nzima kulingana na ile barua pepe tuliyopeleka kwa mkuu hapa Nairobi ili watu waweze kufanya maandamano ya amani.
view