15 Mar 2023 in Senate:
Haya yote yamesababishwa na Upande wa Upinzani. Mabadiliko yaliyoletwa yawekwe wazi ili mimi kama Kiongozi wa Walio Wachache, niwe na ndugu zangu uongozini. Hivyo ndivyo tutaweza kufanya kazi vizuri kulingana na wajibu wetu.
view
15 Mar 2023 in Senate:
Bw. Spika, unaelewa ya kwamba katika hiyo harakati, tuliambiwa kuna amri. Mimi mwenyewe sikuiona hiyo amri ambayo nilipewa. Hata hivyo, tulikubaliana kwamba kuna amri ambayo ulituambia tungoje hadi hiyo kesi iishe. Bw. Spika, jana alasiri, korti ile ya kuangalia ushaibu wa vyama, - Political
view
15 Mar 2023 in Senate:
(PPDT) - walitangaza matokeo ya wale waliopeleka zile kesi mbele yake. Matokeo hayo yako wazi. Wananchi wote nchini Kenya wanajua ya kwamba walijitoa na wakasema kwamba wao hawana haki ya kuangalia hiyo kesi. Bw. Spika, sasa, jukumu ni lako kuliweka wazi, kwa sababu taarifa hiyo si geni kwako, kwa hawa Seneta wenzangu na taifa nzima la Kenya. Politcal Parties DisputeTribunal (PPDT) walikaa na wakajitoa. Walisema kwamba wao hawana uwezo wa kuinglia ratiba yoyote inayoendelea ndani ya Bunge la Seneti. Bw. Spika, kwa hivyo, tunategemea Mawasiliano kutoka kwa kiti kikubwa ulichoketi. Katika harakati zako na hekima, najua unaweza kuona kwamba ni ...
view
15 Mar 2023 in Senate:
Bw. Spika, mimi sipingi uamuzi wako. Lakini, taratibu za Bunge la Seneti zinasema kuwa ikiwa kuna Wabunge ambao wamesema, “tafadhali Bw. Spika, niko na Hoja ya nidhamu, kwa kawaida, huwa unawapatia nafasi hawa Maseneta waweze kuweka wazi Hoja zao za nidhamu, ili ukifanya uamuzi wako, unaufanya kwa pamoja, halafu tuendelee. Hata Sen. (Dr.) Khalwale alitaka kuzungumza. Hiyo ndiyo taratibu ya Bunge la Seneti.
view
15 Mar 2023 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, jambo la kwanza, mimi pia ni Member wa hiyo Kamati. Habari hiyo ilipoletwa, mtu wa kwanza kupinga na kusema kwamba hatuwezi kuruhusu kuongelea mwenzetu ambaye ni Seneta ndani ya Kamati, ikiwa tupo na wafanyikazi na watu wengine kutoka sehemu za Kenya. Bw. Spika wa Muda, ni jambo la kusikitisha sana. Seneta wenzangu, Sen. (Dr.) Lelegwe Ltumbesi na Sen. Kinyua walikuwa hapo.
view
15 Mar 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
15 Mar 2023 in Senate:
No. Sitaki kujulishwa.
view
15 Mar 2023 in Senate:
Utapata wakati wako. Kuwa na heshima wakati ninapoongea. Bw. Spika, nisikize vizuri. Kanuni zetu za Kudumu No.111(4), inasema kwmaba: “Seneta hatatoa kizingizio kuhusu Seneta mwingine, au Mbunge wa Bunge la Taifa, isipokua kwa hoja hususan ambayo aarifa yake imetolewa angalau siku tatu kabla ya hoja ya kujadili mwenendo wa Mbunge au Seneta huyo”.
view
15 Mar 2023 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, ingekuwa bora kama ungenitetea kwa sababu hawa Maseneta wanaongea ninapozungumza ili usisikize kile ninachosema. Kanuni hizi zetu ni Kanuni za Kudumu na hizo ndio tunafuata. Lakini leo cha ajabu ni kwamba nilipopinga kwamba hatuwezi kuongea habari za Sen. M. Kajwang’, mwenyekiti aliyokuwa ameketi hapo saa hizo - na mashahidi wangu ni Sen. (Dr.) Lelegwe na Sen. Kinyua - alikiuka sheria. Ni jambo la aibu kuona Seneta mwingine anaweza kusimama hapa mbele ya watu kutoka sehemu mbali mbali za Taifa--- Ikiwa mimi ninaweza kusimama hapa na ndugu yangu wakili yuko hapa, alafu niongee juu yake kwa njia ...
view
15 Mar 2023 in Senate:
On a point of order Mr. Temporary Speaker, Sir.
view