Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 621 to 630 of 2266.

  • 19 Jan 2023 in Senate: Bw. Spika, je, ni sawa kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Masuala ya Kisheria na Haki za Kibinadamu--- Ingekuwa bora kama angekuwa wa mwisho baada ya Maseneta wote kuzungumza. Amepewa nafasi ya kuzungumza. Endapo tena atapewa nafasi ya kuzungumza katika kikao cha alasiri, hilo halitakuwa jambo nzuri. Atakuwa na muda mrefu wa kutueleza vizuri wakati wa kipindi cha alasiri kwa nini anapendekeza mabadiliko haya. Kwa hivyo, ni vyema awape nafasi Maseneta wengine nafasi ya kuongea. Huo ndio utaratibu. view
  • 19 Jan 2023 in Senate: Asante, Bw. Spika. view
  • 19 Jan 2023 in Senate: Asante, Bw. Mwenyekiti wa Muda. Naunga mkono mapendekezo ya Sen. Mumma. Ukweli wa mambo ni kuwa sisi sote ni binadamu. Sen. Wakili Sigei ambaye ni shupavu katika masuala ya sheria asubuhi alipendekeza marekebisho kwa Mswada huu. Hata hivyo, amerudi hapa alasiri na akageuza mwelekeo. Tumejipata katika njia panda. Nasema hivyo kwa sababu sisi hatuwezi kuwa conveyor belt ya Bunge la Taifa. Kama wao hawawezi kufanya kazi kisawasawa, sisi tutafanya kazi yetu kisawasawa. Kamati ya Haki, Masuala ya Kisheria na Haki za Kibinadamu inaheshimiwa sana hapa Seneti. Ripoti zinazotokana na Kamati hiyo ni muhimu kwani zinaongoza sheria tunazopitisha hapa Seneti. Kama ... view
  • 19 Jan 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 19 Jan 2023 in Senate: Bw. Mwenyekiti wa Muda, tume ya utumishi wa umma au Public Service Commission (PSC) ni tume ambayo viongozi au wafanya kazi wake huchaguliwa na Mhe. Rais. Tunamheshimu Rais lakini--- view
  • 19 Jan 2023 in Senate: Sen. (Dr.) Khalwale, keti chini. Tuliza boli. Ni rahisi kwa Mhe. Rais kuwashawishi wanaofanya kazi katika tume ya hiyo kwa sababu ni wafanyi kazi wa Serikali. view
  • 19 Jan 2023 in Senate: Bw. Mwenyekiti wa Muda, ninaunga mkono mapendekezo ya Sen. Mumma kwani makamishna wa tume ya utumishi wa umma wanachaguliwa na Mhe. Rais. Hivyo, Mhe. Rais atakuwa na uwezo mkubwa juu ya tume hiyo. Sisemi kuwa Mhe. Rais atatumia mamalaka yake vibaya. Leo Mhe. Rais anaweza kuwa mzuri na kutumia sheria hiyo vizuri. Je, kesho tukipata Mhe. Rais mwingine? Tukiwa hapa kama Wabunge ni lazima tupitishe sheria ambazo zitawafaidi watoto wetu, wajukuu wetu and vitukuu wetu. Siku moja wakija hapa, waweze kusema ya kwamba, ‘wazee wetu ambao walikuwa hapa kama Sen. (Dr.) Khalwale walipitisha sheria ambayo ilidumu maisha.’ Naunga mkono mapendekezo ... view
  • 19 Jan 2023 in Senate: Bw. Mwenyekiti wa Muda, ninataka unitete. Unaona Kiongozi wa Walio Wengi katika Bunge la Seneti yuko katika mstari wa mbele kufanya vile. Unaona anaongea. Hata mimi niko na ujuzi huo. Naweza kutumia nafasi hiyo kumfanyia fujo mpaka ashindwe kuongea. view
  • 19 Jan 2023 in Senate: Point of order, Mr. Temporary Chairman, Sir. view
  • 19 Jan 2023 in Senate: Bw. Mwenyekiti wa Muda, tulipokuwa na kikao asubuhi, Sen. Wambua anayewakilisha Kitui alikuwa amevaa visivyo kulingana na taratibu za Seneti. Spika alimwambia kuwa hangemruhusu kuongea licha ya kupiga kura ambayo ni muhimu zaidi. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus